Naomba ushauri na kujuzwa bei za mabati ya Alaf

Mimi nimepaua bati kigae alaf nimetumia almost 13m kwa kila kitu ,nakushauri ukitaka paa lichongoke sana kwenda juu utatumia bati nyingi kwahivyo kua makini na mapaa marefu kwasababu hii bati inauzwa ghali sana, bati ya alaf kigae inacheza 23140 kwa mita moja ili upate bei ya bati moja unatakiwa uizidishe mara 3 ,nilitaka kutumia Ando ila sikupata rangi nzuri ninayoitaka.nakutakia upauaji mwema
 
Tena ukienda kiwandani kuna punguzo kidogo kuliko kwa wakala sijui na nasikia ukitumia wakala bei inaongezeka
 
"MATAPELI"!!!

Kwa nini huweki wazi hapa ili kila mtu aone, na kama yupo muhitaji mwingine yeyote anayehitaji aone kama nyie sio wa kuuza?

Kama wa kurahisisha mawasiliano Kwa nini usimshauri aende moja kwa moja kiwandani?

Kwa nini Iwe siri wakati unajua atakapo chukulia mabati ni kiwandani?



#ogopamatapeli#tamaambaya
 
Kama hela zako za kuunga unga nenda kiwanda cha Dragon

Nilitembea viwanda vitatu Dsm kupata bei
1. Sunshare hawa bei zao juu kuliko viwanda vyote

2. Alaf bei juu, wako nafasi ya pili baada ya Sunshare
3. Dragon hawa ndo niliona nafuu

Uchaguzi ni wako namba hizi hapa

0716 600 800 Alaf mtu wa marketing

065 229 1297 Sunshare mtu wa marketing

065 229 1297 Dragon mtu wa marketing
Hizo ni namba za Dsm
Chagua mwenyewe
 

Dragon Mabati call:0753535935/0785033500
 
Kwa hyo dragon na sunshare wanashare mtu wa marketing [emoji1] [emoji1787]?
 
Hizo bei za Alaf zilivyokuwa juu,wacha tu nipauwe na hizi za kampuni nyingine,ntakuwa napiga rangi kila zikipauka...
 
Hizo bei za Alaf zilivyokuwa juu,wacha tu nipauwe na hizi za kampuni nyingine,ntakuwa napiga rangi kila zikipauka...
Mi kilichonishinda ni nyodo zao, iyo siku nimefika kiwandani kidada kipo kwenye gari kinaniangalia tu, kimekaa kama dk 5 ndo kinakuja,

Nikaenda zangu dragon
 
pale alaf kuna ujinga mwingi lakini ndiyo bati bora ukilinganisha na hao wengine angalau ando nao wanajitahidi sana kwa ubora.
 
Na Mimi naomba kujua bei ya bati chapa alaf gauge 30.Kabla sijapigwa na kitu kizito kichwani.Asanteni
 
Na Mimi naomba kujua bei ya bati chapa alaf gauge 30.Kabla sijapigwa na kitu kizito kichwani.Asanteni

Uko wapi mkuu, kuna bei mbili kwa agent ie muuzaji na ukienda kiwandani. Au ofisini kwao kuweka order.

Nimekujibu hivi kwa sababu maalum.
 
Amina Juma Yusufu *Versatile na Romantile
Bei zake ni sawa pia
Aina hizi kwa ALAF ni Gauge 28 pekee
Urefu wa meter 1 ni tsh 23,938

Ambapo bati la kawaida urefu wa meter 3 sawa na urefu wa futi 10 ni tsh 71,800.

Bati zima linakua na upana wa cm 110

#Yanayoitwa
*Royal Versatile na Royal Romantile(Rangi zake sio za kuteleza ni Rough surface)

Bei zake ni sawa pia
Aina hizi kwa ALAF ni Gauge 28 pekee
Urefu wa meter 1 ni tsh 24,611

Ambapo bati la kawaida urefu wa meter 3 sawa na urefu wa futi 10 ni tsh 73,800

Bati zima linakua na upana wa cm 110
 
Iyo attachment ya kwanza ni bati 65 za gauge 30
Iyo ya pili ni kofia 15
NB: nilinunulia kiwandani
 

Attachments

  • Screenshot_20230129-133113_WhatsApp.jpg
    112.2 KB · Views: 113
  • Screenshot_20230129-133150_WhatsApp.jpg
    55.1 KB · Views: 94
Iyo attachment ya kwanza ni bati 65 za gauge 30
Iyo ya pili ni kofia 15
NB: nilinunulia kiwandani
Hizi ni bei za resincot

Maxcover (28g) mita 1 ni 21,350tsh
Covermax ( 30g) mita 1 ni 12,800tsh
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…