Naomba ushauri na muongozo wa ujenzi

Naomba ushauri na muongozo wa ujenzi

Hivi kwanini ujenge guest house?
Kwanini mtu usijenge vyumba 3 vinatosha, mgeni akija atalala anapojua yeye
 
Msingi ni m5.
Kupandisha vyumba viwili ni m2 mpaka kuezeka tuu.
So ikitokea umefeli itakua ni mwishoni. So usiache kuanza. Bora pesa ifeli ila ukiwa umeshaanza.

Me nilijenga nyumba ya uwani servant quarter kwa 7m
Sebule, vyumba viwili na choo na nikahamia.

Ubaya toka wiki iliyopita cement zimepanda bei. Twiga plus 16000
Twiga extra 15500
Nondo 12mm 22,000
Tofali la nchi 5 1100 mpaka site.

Pia nna hardware madale -mbopo.. ukiweza karibu tufanye kazi. Ikiwa huna fundi ntakupa fundi pia..
 
wakuu habar zenu
nina kiwanja cha 20*20 hapa hapa dar maeneo ya tegeta madare plan yangu ni kujeng Nyumba kubwa ya vyumba vinne sebule daining jiko store. lakini kwa sasa nipo na 7,000,000 nnataka nipige msingi wa nyumba nzima kisha ni pandishe viwili na kueka bati niweze kuamia kisha nijenge taratibu je kwa hiyo milion saba naweza kutoboa mba kuamia kwa maana ya msingi wote na kupandisha vyumba viwili pakiwemo na madilisha ?

Ahsanteni sana naitaji msaada wenu nyumba ninayo tarajia kujenga ni HIDENROOF
Kwa uzoefu wangu milion 7 labda ujenge chumba kimoja tu...nyumba ya vyumba vi4 kama ipo complicated sio chini ya milion 90 au ujenge mgongo wa tembo..kujenga sio kazi rahisi
 
Hapo labda upige msingi, uinue chumba kimoja upaue kabisa, kisha kitakachobaki ndio uinue kozo nyingine mpaka utakapoishia
Kwa nyumba ya vyumba vi4 milion7 hata msingi haitoshi

Piga hesabu ya tofali za msingi

Malipo ya fundi

Maji

Cement

Nondo

Mfano


Fundi kwa msingi ni TZS 1.5 m

Tofali 2500* TZS 1,100

Nondo tuchukue *54 mara 26,000

Sehemu kama ina bonde kifusi chake

Mchanga trip TZS 70,000

Kokoto trip 2@ kwa 350,000

Kukodi mbao 150,000 TSZ

Cement mifuko kama 50 @ 15,500

Ukipata jibu..mimi nimejenga mwaka jana lakini gharama nilizokutana nazo kwa nyumba ya room 4 sina hamu nilipo
 
Kaka
Kwa nyumba ya vyumba vi4 milion7 hata msingi haitoshi

Piga hesabu ya tofali za msingi

Malipo ya fundi

Maji

Cement

Nondo

Mfano


Fundi kwa msingi ni TZS 1.5 m

Tofali 2500* TZS 1,100

Nondo tuchukue *54 mara 26,000

Sehemu kama ina bonde kifusi chake

Mchanga trip TZS 70,000

Kokoto trip 2@ kwa 350,000

Kukodi mbao 150,000 TSZ

Cement mifuko kama 50 @ 15,500

Ukipata jibu..mimi nimejenga mwaka jana lakini gharama nilizokutana nazo kwa nyumba ya room 4 sina hamu nilipo
Kaka tunatofautiana.. Kwa hizo bei zako sijui uchumi wako na huko ulipo ila kuna vitu unaweza kufanya vikapunguza bajeti.

Hiyo 1.5 mafundi wengine unaongeza kidogo tu anajenga kuanzia msingi mpaka juu(boma lote)
Hata mimi mwaka jana nimejenga, fremu tu sio nyumba ya kuishi.

Nilifanya hivi kupunguz gharama.

Kwanza huku tofali mpaka site ni 1000 si hiyo 1100, ukilinunulia pale site unauziwa 800, pale unaenda kama mtu wa kati, hivyo muuzaji atakupozea bei atakuuzia hata 750/700 kwa wingi wa tofali, kisha tafuta gari kubwa yenye kubeba tofali nyingi kwa mkupuo. Jitahidi kwenye tofali na site kuwe pua na mdomo ili gharama ya usafiri isiwe kubwa, huyu unahakikisha unapatana nae gharama icheze 50/70 kwa tofali badala ya ile 100 yao, site ikiwa pua na mdomo na tofali kkisha ikiwa trip moja, hawakatai.

Kisha unakuja kwa washushaji(wapakizi) hawa nao huwa bei yao ni 100 kwa tofali (kupandisha na kushusha) patana nao vizuri kuna pesa utajikuta umesave.

Jitahidi unaponunulia tofali nunua na cement na nondo kabisa kupunguza gharama za usafiri.

Kama sehemu ardhi ngumu kimasikini hakuna haja ya kuweka nondo(zege) kwenye msingi. Kama ardhi sumbufu hakuna namna,zege haiepukiki, ila sehemu nyingi hakuna haja. ((sikupiga zege) hiyo 56*26000 futa hiyo hesaBu.

Fundi
Tafuta fundi mzuri mnajuana mpe ukweli huna vyako, akusaidie tu, mara nyingi tofali za msingi wanajenga kwa 250 mpaka 200. Muombe awe kama fundi mkuu, yeye tofali utamuuzia kwa 250/300 ila wengine 200 hachomoi hapo.

So kwenye msingi ufundi haufiki hata milioni

Msingi na chumba kimoja anaweza inua fresh tu,kish huko kwingine atainua kama kuna kaakiba katakuwepo
 
Itategemea na ukubwa wa nyumba vyako, tafuta mtaalamu wa makadirio au Engineer mpe ramani akupe rough estimate. Mimi ni Mtaalamu wa Ujenzi 7m ukijitahidi sana ni msingi tu na penyewe upate mafundi wenye bei za chini sana na wapunguze materials
 
Wakuu habari zenu

Nina kiwanja cha 20*20 hapa hapa Dar maeneo ya Tegeta Madare plan yangu ni kujenga nyumba kubwa ya vyumba vinne sebule daining jiko store. Lakini kwa sasa nipo na 7,000,000 ninataka nipige msingi wa nyumba nzima kisha ni pandishe viwili na kueka bati niweze kuamia kisha nijenge taratibu je kwa hiyo milioni saba naweza kutoboa mba kuamia kwa maana ya msingi wote na kupandisha vyumba viwili pakiwemo na madilisha ?

Ahsanteni sana naitaji msaada wenu nyumba ninayo tarajia kujenga ni HIDENROOF
Kwa mbagala inatosha kabisa, ila kwa hayo maeneo uliyoyataja nina mashaka kidogo

Sent from my TECNO KC6 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom