Kaka
Kwa nyumba ya vyumba vi4 milion7 hata msingi haitoshi
Piga hesabu ya tofali za msingi
Malipo ya fundi
Maji
Cement
Nondo
Mfano
Fundi kwa msingi ni TZS 1.5 m
Tofali 2500* TZS 1,100
Nondo tuchukue *54 mara 26,000
Sehemu kama ina bonde kifusi chake
Mchanga trip TZS 70,000
Kokoto trip 2@ kwa 350,000
Kukodi mbao 150,000 TSZ
Cement mifuko kama 50 @ 15,500
Ukipata jibu..mimi nimejenga mwaka jana lakini gharama nilizokutana nazo kwa nyumba ya room 4 sina hamu nilipo
Kaka tunatofautiana.. Kwa hizo bei zako sijui uchumi wako na huko ulipo ila kuna vitu unaweza kufanya vikapunguza bajeti.
Hiyo 1.5 mafundi wengine unaongeza kidogo tu anajenga kuanzia msingi mpaka juu(boma lote)
Hata mimi mwaka jana nimejenga, fremu tu sio nyumba ya kuishi.
Nilifanya hivi kupunguz gharama.
Kwanza huku tofali mpaka site ni 1000 si hiyo 1100, ukilinunulia pale site unauziwa 800, pale unaenda kama mtu wa kati, hivyo muuzaji atakupozea bei atakuuzia hata 750/700 kwa wingi wa tofali, kisha tafuta gari kubwa yenye kubeba tofali nyingi kwa mkupuo. Jitahidi kwenye tofali na site kuwe pua na mdomo ili gharama ya usafiri isiwe kubwa, huyu unahakikisha unapatana nae gharama icheze 50/70 kwa tofali badala ya ile 100 yao, site ikiwa pua na mdomo na tofali kkisha ikiwa trip moja, hawakatai.
Kisha unakuja kwa washushaji(wapakizi) hawa nao huwa bei yao ni 100 kwa tofali (kupandisha na kushusha) patana nao vizuri kuna pesa utajikuta umesave.
Jitahidi unaponunulia tofali nunua na cement na nondo kabisa kupunguza gharama za usafiri.
Kama sehemu ardhi ngumu kimasikini hakuna haja ya kuweka nondo(zege) kwenye msingi. Kama ardhi sumbufu hakuna namna,zege haiepukiki, ila sehemu nyingi hakuna haja. ((sikupiga zege) hiyo 56*26000 futa hiyo hesaBu.
Fundi
Tafuta fundi mzuri mnajuana mpe ukweli huna vyako, akusaidie tu, mara nyingi tofali za msingi wanajenga kwa 250 mpaka 200. Muombe awe kama fundi mkuu, yeye tofali utamuuzia kwa 250/300 ila wengine 200 hachomoi hapo.
So kwenye msingi ufundi haufiki hata milioni
Msingi na chumba kimoja anaweza inua fresh tu,kish huko kwingine atainua kama kuna kaakiba katakuwepo