Naomba ushauri namna ya kuhama kozi chuo cha udom

Naomba ushauri namna ya kuhama kozi chuo cha udom

Jr nakshboy

New Member
Joined
Sep 21, 2024
Posts
1
Reaction score
2
Samahani viongoz wangu!Nilikuwa naomba mnisaidie je naweza kuhama kozi katika chuo cha udom kutoka nursing kwenda pharmacy au md nanabidi nifuate hatua zp? Na itakuaje kuhusu mkopo? Naomben
msaada wenu nilikuwa pcb ufaul wa CBC
yan points 8
 
Samahani viongoz wangu!Nilikuwa naomba mnisaidie je naweza kuhama kozi katika chuo cha udom kutoka nursing kwenda pharmacy au md nanabidi nifuate hatua zp? Na itakuaje kuhusu mkopo? Naomben
msaada wenu nilikuwa pcb ufaul wa CBC
yan points 8
Ndio unaweza kuhama kama una vigezo vinavyotakiwa.

Huwa kuna aina mbili za kuhama/transfer.

Moja ni Inter-university transfer hapa ni kuhama kutoka chuo kimoja kwenda kingine na

Pili ni Intra-university hapa ni kuhama kutoka kozi/program moja kwenda nyingine ukiwa ndani ya chuo kimoja. Hiki ndicho unachotaka kufanya.

Vigezo vinavyotakiwa:
Kwanza kabisa dirisha la kuhama (Transfer window) liwe limefunguliwa na TCU, huwa linafunguliwa baada ya zoezi la waombaji kupangiwa vyuo (admissions) kukamilika.

Kwa wewe unayetaka kuhama/kubadilisha kozi (Intra-university transfer) hakikisha kwamba

(1). una ufaulu unaotakiwa (cut off points) kwa kozi husika mfano kama ni MD labda cut off points zake ni 11 nk, je unazo?

(2). kuna nafasi ktk kozi unayotaka kuhamia mfano kama unataka kwenda MD na pengine chuo kinatoa nafasi 200 tu na zimejaa tayari. Kwa hiyo unaongea na admission officer kuhusu nia yako ya kutaka kuhama/kubadilisha kozi ili kama nafasi zipo uweze kuandika barua nk.

Kuhusu mkopo:
Kama utafanikiwa kuhama/kubadilisha kozi taarifa zako zitapelekwa bodi ya mikopo (kama ulipatiwa mkopo) ili jina lako liwekwe kwenye orodha ya watu wa kozi uliohamia au kubadilisha tu data zako ziwe sawa kwenye mfumo wao. Hata hivyo kiasi ulichopewa cha mkopo hakitabadilika, itabadilika tu kama utakata rufaa au utaomba kuongezewa au vyovyote vile utakavyoshughulikia lenyewe. Kwa sababu kiasi hakibadilishwi inaweza ikakuathiri mfano kama kozi uliohamia ada yake ni kubwa kuliko ile ya kozi ya awali. Hapo itakulazimu labda kuongezea kiasi fulani kwenye ada au kukata rufaa bodi kuomba kuongezewa mkopo. Vinginevyo kama ada za kozi zote ni sawa basi itakuepusha hiyo changamoto.

Kila lakheri!
 
Subiri chuo kifunguliwe kuna kuwaga na dirisha la intra transfer univresity utaomba ila jiandae maana kuna kukosa pia, ila muhimu andaa elfu 50 ndio ada ya kuomba kuhama programme.
 
Samahani viongoz wangu!Nilikuwa naomba mnisaidie je naweza kuhama kozi katika chuo cha udom kutoka nursing kwenda pharmacy au md nanabidi nifuate hatua zp? Na itakuaje kuhusu mkopo? Naomben
msaada wenu nilikuwa pcb ufaul wa CBC
yan points 8
Muone HOD wako atakusaidia
 
Inawezekana kuhama kozi mradi tu uwe na sifa za kuhamia kozi unayotaka na iwepo nafasi. cha kufanya unaandika barua ya kuomba kuhama kozi na kuiwasilisha kwenye Ndaki/Shule Kuu au Taasisi husika ukiwa chuoni. Utajibiwa
 
Back
Top Bottom