Naomba Ushauri: Nataka kuacha kubeti

Naomba Ushauri: Nataka kuacha kubeti

Habari za muda,

Mimi ni kijana wa miaka 23 nimekuwa na uraibu mkubwa sana wa kamari (kubeti). Nilianza kubeti tangu 2015 kipindi nipo Form 2 kipind Primier Bet inaanza wale wa vikaratasi then nilistop kwa muda ila wakati nipo form 5 nikarud na uraibu ulianza.

Japo nilishawahi kushinda nilibetia mpaka pesa ya michango kama Tsh. 90,000/- nikala Tsh. 180,000/- but nilikua sibet sana sababu shuleni unabanwa kutumia simu.

Nilivyofika chuoni ndio uraibu ukazidi baada ya kumiliki smartphone, nikawa mraibu sana wa kubeti nikahamia kwenye virtual bet mpaka Aviator la Sportybet nako nilipoteza tu.

Naombeni ushauri namna gani niweze kuacha kubeti maana najitahidi nashindwa.
Betting ni biashara ya kitapeli kwa asilimia 100, wanapata wachache wanapoteza wengi.. Pesa unayodhani umeshinda ni yako na ya wengine waliopoteza. Akili kichwani mwako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vipi na sisi tunao nunua utelezi, hela yetu haina kazi pia ?
Utelezi ni furaha ya masaa tu...mnunua utelezi pia ni mnunua stimu...utamu wa jambo lake haudumu milele ni tukio la wakati tu...

Mnunua utelezi na mnunua kilevi ni sawa sababu wanajaribu kutibu kiu ambayo kesho itarudi tena...

Haya mambo ya utelezi,kubeti na pombe ni magonjwa ya furaha kama magonjwa mengine....

Binadamu anatafuta furaha...so mara nyingine anafanya kile anacho hisi kitamsaidia kumfanya ajione anaishi...na kufurahi....
 
Acha utani wewe.
Kubeti ndio mradi pekee unaohitaji mtaji mdogo Sana. Isitoshe, unajua mikionea ndani ya dakika chache
Kwanini matajiri na wanauchumi wanapambana katika shughuri nyingine...Kwanini Bhaharesa asibeti anahangaika na kuuza Juice..na Ice cream
 
BETTING NI BIASHARA YA UTAPELI ILIYO HALALISHWA....Kwasababu tu kati ya 100 waliopoteza pesa zao kuna mmoja atashinda pesa....
 
Utelezi ni furaha ya masaa tu...mnunua utelezi pia ni mnunua stimu...utamu wa jambo lake haudumu milele ni tukio la wakati tu...

Mnunua utelezi na mnunua kilevi ni sawa sababu wanajaribu kutibu kiu ambayo kesho itarudi tena...

Haya mambo ya utelezi,kubeti na pombe ni magonjwa ya furaha kama magonjwa mengine....

Binadamu anatafuta furaha...so mara nyingine anafanya kile anacho hisi kitamsaidia kumfanya ajione anaishi...na kufurahi....
Umeeleweka mkuu
 
Mtu anayetaka kujua jinsi hizi site zinavyofanya kazi na kupiga pesa aseme nimuokoe na janga lake...ODDS wanazotoa hazina 50% kwa 50%... ya probability...

Labda kama wewe ni mwanamichezo wa mechi husika na umeamua kubeti na kufanya au kuuza FIXED OUTCOME...na mara nyingi wachezaji ndio wanaweza kubeti fixed match hasa magolikpa...Golikipa anaweza kubet na akatoboa....
 
We jamaa muongo sana..wamiliki wa timu,wachezaji na referees wa mchezo husika hawaruhusiwi kubeti
 
Mtu anayetaka kujua jinsi hizi site zinavyofanya kazi na kupiga pesa aseme nimuokoe na janga lake...ODDS wanazotoa hazina 50% kwa 50%... ya probability...

Labda kama wewe ni mwanamichezo wa mechi husika na umeamua kubeti na kufanya au kuuza FIXED OUTCOME...na mara nyingi wachezaji ndio wanaweza kubeti fixed match hasa magolikpa...Golikipa anaweza kubet na akatoboa....
Umetishaa
 
Najilaumu kwa nn nimechelewa kujua hii kitu Yan unalala masikini unaamka tajiri no mchezo was kujikula
 
jaribu fanya ivi futa apps zote ambazo zinahusiana na betting mfano meridian bet, cjui betika au gal bet na nyingine kama live score ili kupunguza mihemko utakuja kunishukuru
Ushauri mbovu tangu niingie hapa jukwaani almost 8 years;
Unamshauri mtu aache shughuli halali za kiuchumi na kulipa kodi akafanye biashara gani?
 
Betting ni ajira kama ajira nyingne kwann uache au ushapata kazi ....kama una kazi acha ila kma huna itumie kama fursa ya maendeleo ....watu tunamiliki magari na magorofa kwasababu ya betting
Naona unazidi kugongelea tu!
 
Kuacha ni mpaka nafsi yako iamue kwanza kisha uchukue hatua madhubuti kutokurudi nyuma....Nlikuwa Muhanga wa uraibu wa kamari kwa miaka kadhaa lakini niliamua kufuta kila kitu kinachohusiana na kamari katika simu yangu . Kisha nikahakikisha nakuwa busy sana na shughuli za kiuchumi ili mawazo yasirudi kwenye kubeti.

Namshukuru Mungu nimeweza kuondokana na arosto ya kubeti na pia msongo wa mawazo unaotokana na kupoteza sana pesa. Toka niache kubeti nimeona manufaa mengi sana.
 
Naomba mnifundishe kubet pliz Kila naye muomba hataki kunifundisha ila wao wanabet au ni wivu?
 
Iambie nafsi kuwa kuanzia sasa kubeti basi....binafsi sijabeti kitambo!!

Nlifuta kila kitu kinachohusiana na kubeti ktk electrinic devices zangu.Nilikuwa compulsive gambler yaani naweza kaa siku nzima sifanyi kazi yoyote zaidi ya kubeti tu. Mpaka ikafikia stage niko radhi ni-skip kula ili pesa yake nikaibetie. Siku moj niliamka nikasema bye bye kubeti maana ilishaniletea athari za waziwazi kisaikolojia,kihisia,kiuchumi na kijamii.

Mpaka sasa namshukuru Mungu kwa hatua niliyofikia, Niliiambia nafsi yangu kuwa naacha kubeti, nikajiforce kujiweka busy sana kiasi nikawa sina muda wa kuwaza kuhusu kubeti...na kweli nimefanikiwa kwa kiasi fulani kwani hata nikikuta watu wanabeti mimi sina hamu nayo kabisa. I lost its taste na nikiri wazi kuwa hakuna uraibu mkali na wenye athari mbaya kama uraibu wa kamari
 
Back
Top Bottom