Naomba ushauri nifanyeje, Kutatua tatizo?

Naomba ushauri nifanyeje, Kutatua tatizo?

Jamaludin

Member
Joined
Apr 26, 2024
Posts
48
Reaction score
40
Habari za Leo wanajamii forum, naombeni nisaidiwe kwa hili.

Nina kazi ya kukaa muda mrefu kwenye kompyuta (Coding Developer), na katika kipindi kifupi kilichopita, nimeanza kusumbuka na maumivu ya mgongo upande wa kushoto, chini kidogo. Hali hii inanipelekea kutoshika vizuri kwa muda mrefu; mpaka napenyeza mgongo au nigemee, lakini bado siwezi kubaki katika hali moja kwa muda. Maumivu nayasikia hasa nikikaa kwa muda mrefu au nikilala, na nashindwa kujua ni jinsi gani ya kulala vizuri.

Nimejaribu kutumia baadhi ya vidonge nilivyonunua kwenye duka la madawa baada ya kutoa maelezo, lakini nimeona havifui dafu. Pia, nimesoma baadhi ya makala mtandaoni na nikaona huenda ni kuchanika au kukakamaa kwa mgongo.

Nifanyeje? Uafadhali hutokea pindi ninapokuwa natembea. Nisaidieni wajuzi na wakunga tafadhali.

Ahsabteni sana.
 
Ukikaa mda mrefu sana sehemu ngumu pingili zako zinabonyea kwenda chini zinaleta mgandamuzo.kwenye nerve zinazopita kati yake pia ndo mana maumivu jitahidi kukaa Kwa usahihi,ukipata mda free jilaze sakafuni Mgongo unyooke,ukilala usiku usilale chali,lala kiupande au kifudidi.
Ingia YouTube andika exercise for lower pack pain,Kisha karirir uwe unafanya Kila usiku na asubuhi..ukipuuzia hili kadri mda utavyoenda pale kwenye pingili zako kunakuwakuwaga na visahani vinavyotenganisha,Kwa kingereza tuziite disc,hiziz zikibanwa mwisho utaanza kupata maumivu makali maisha yako yote,na itaathiri viungo vingine.na ikiendelea kubanwa utaanza kusagika,ikisagika na kuisha yote ndipo mfupa wa juu na WA chini utaanza kugusana nao kusagika.utapata tabu sana mkuu
Itabidi upelekwe hospital ufanyiwe surgery ya kuwekwa vyuma na disc bandia.nazo zitaendelea kukupa maumivu.

Tafuta mazoezi uyaone YouTube,fanya,utapata nafuu.ukikaa kutwa nzima basi usiku mazoezi jilaze tu sakafuni kabla ya kitandani.dawa hazisaidii Bali lifestyle yako ndo inachangia badilisha
 
Unahitaji matibabu yaitwayo physio therapy. Jaribu kuulizia kwenye hospitali za huko ulipo kama wanatoa. Kama hakuna hospitali fanya namna uje Dar kwaajili ya matibabu. Huku kuna hospitali kama Muhimbili na Bochi ambazo kwa ufahamu wangu wanatoa hiyo tiba.
 
Kwanza angalia aina ya kiti unacho kalia masaa mengi kama back side ipo kwenye proper position.
Baada ya hapo nenda ukawaone wataalamu wa mofupa mkuu, temana na vidonge hizo
 
Kwanza angalia aina ya kiti unacho kalia masaa mengi kama back side ipo kwenye proper position.
Baada ya hapo nenda ukawaone wataalamu wa mofupa mkuu, temana na vidonge hizo
Ahsante, kuna point nimeichukua hapa, nashkuru mkuu.
 
Usije ukawa unakalia viti vya bar, nunua kiti cha kueleweka!
 
Back
Top Bottom