Mwamuzi wa Tanzania
JF-Expert Member
- Apr 7, 2020
- 15,486
- 45,256
Habari!
Mimi ni mwajiriwa wa serikali ofisi X kwa kada ya ulinzi.
Nina miaka 7 sasa tangu niajiriwe. Nimejenga nyumba ya kawaida sana. Na nina second hand car, namaanisha namiliki gari ya kuungaunga. Ninapenda sana magari.
Nimechoka kulinda. Yaani nimechoka sana maana ni kazi ambayo hata mke wangu nashindwa kumwambia nafanya kazi gani. Nimemdanganya tu kuwa mimi ninafanya kazi fulani. Ofisini amewahi kuja siku moja ila hajui kuwa nalinda.
Akiona maisha yetu kila siku nyama, samaki basi hawezi kufikiri kuwa ni mlinzi maana walinzi wamekaririka kuwa huishi maisha ya dagaa na tembere.
- Nina cheti cha driving na leseni naweza kubadili kada nikiamua tu . Ila changamoto ni kwamba taanza na mshahara wa chini kidogo ukilinganisha ninaolipwa sasa.
- Nimepata sehemu ya kuhamia kwa kada yangu hii ya ulinzi na mshahara kidogo utaongezeka ila nitakuwa busy sana hata masomo yangu ya chuo kikuu naweza kusimama kwaajili ya ubize wa kazi na nitaendelea mpaka nitakapozoea mazingira ya huko ofisi Y, sijui itachukua muda gani kupata mpenyo.
- Au nikomae na huu ulinzi hapa ofisini kwetu mpaka nimalize masomo yangu ya university maana napata nafasi ya kusoma kwa uhuru?
Nifanye lipi hapa wakuu nimechoka kuwa mlinzi, nikienda bank kukopa nikiulizwa kada najibu nikiwa mnyonge na sometimes wananichana kabisa warembo wa bank kuwa sifanani na kuwa mlinzi. Basi nacheka kidogo kuwazuga maisha yanaendelea.