Ukiendekeza hisia kwenye biashara basi ujue bado hujakomaa kibiashara,, mfanya biashara anakuwa makini na mahesabu deal na faida sambamba namuda, mfanya biashara huwa anapenda biashara inatakayo mlipa kwa muda fulani, ukiwa kama mfanya biashara unatakiwa uwe na macho ya kuona mbele, mfanya biashara anaweza kufanya biashara ya kawaida lakini anakuwa ameona mbeleni hiyo biashara haitakuwa ya kawaida, Aliko Dangote ni mfanya biashara mwenye mafanikio makubwa sana lakini mafanikio yake yametokana na uwezo wake mkubwa wa kuona fursa, sio kwa sababu alipenda kitu fulani, mfanya biashara unatakiwa kupenda biashara yenye faida,,
Kama biashara yako ya duka inakulipa unatakiwa ukomae lakini pia uwe una mitazamo ya kukua kibiashara kama huna akili ya biashara wee nenda tu katafute ajira ukilazimisha sana kufanya biasha kwa mihemko utalia sana mkuu,,
Kiwango chako cha kufanya biashara kina pimwa kwenye uwezo wa kuona fursa na bidii na subira, kaa chini fikiria vizuri ni fursa gani unaweza kuwekeza
Kama huoni fursa mimi naweza kukushauri lakini pia naweza kukupa orodha ya fursa zilizopo hapa Tanzania ni nyingi sana sana mkuu huo mtaji wako ni mkubwa sana kiasi kwamba unaweza kuanzisha hata kampuni, mimi naona fursa nyingi sana ingawa kwangu mimi natamani kufanya project kubwa, lakini sina mtaji kwahiyo nimeanza na biashara ndogo ila wewe hiyo 4M naitamani sana mkuu ningekuwa nayo mimi [emoji23][emoji23]