Naomba ushauri wa kamera nzuri itakayonifaa

Naomba ushauri wa kamera nzuri itakayonifaa

Bwana BANGO JEUPE mie nnaungana na Mad Max kupendekeza kamera za NIKON maana ndiyo ninayotumia.

Wanasema kama unapenda video chukua Cannon.

Na kama unapenda picha tu chukua NIKON.

Na kama uwezo upo basi kuna ambazo zipo na uwezo wa picha na video kama hii D7500(ilikiwa 2.5M) ni wewe tu kuchagua
View attachment 2941716
Hiyo napata mpya au used
 
Hii ni imani tu. Kwa kiwango simu zilipofikia. Ukichukua simu unakuwa umepata 2 in one.

Ni nzuri kwa maana ya utility

Camera yenyewe ni kama una mapenzi ya kumiliki pia kamera kama hobby pia.

KWa kazi yako ukipata simu kali inatosha
Hii imekaa kimkakati zaidi kama simu inatosha kwa ubora Ninaoutaka acha nijipange
 
Hata ukiwekeza kwenye simu kali bado utaonekana uko serious na kazi yako na utafanya kazi yako kwa haraka zaidi tofauti na ukitumia Camera.
Hapa nijipange mkuu napenda sana picha yaani ukinipita kwenye picha sina Aman kabisa
 
Kwa kazi hiyo sidhani kama unahitaji kamera. Nadhani ungetafuta tu simu yenye uwezo mkubwa wa kamera. Samsung s series kuanzia 21 plus au ultra, pixel kuanzia 7 au iphone kuanzia 13
 
Kwa kazi hiyo sidhani kama unahitaji kamera. Nadhani ungetafuta tu simu yenye uwezo mkubwa wa kamera. Samsung s series kuanzia 21 plus au ultra, pixel kuanzia 7 au iphone kuanzia 13
Ushauri huu inaonekana ndo the best watu mnaona mbali
Shukrani mkuu
 
Chukua iPhone 13Pro Max kama uko vizuri ina cinematic mode na picha nzuri, hyo Google pixel 7Pro au 8A uongo mkuu.
 
Chukua iPhone 13Pro Max kama uko vizuri ina cinematic mode na picha nzuri, hyo Google pixel 7Pro au 8A uongo mkuu.
Naona wadau wengi wanashauri IPhone
Vipi kuna trick ya kuweza kutumia unauthorized apps mfano GBWATSAP,?
Maana nasikia wana apps zao
 
Bei Sijajua mkuu, ila ushauri wangu nenda na simu za android mana zitakupa wigo mpana kufanya mambo yako tofauti na IOS. Samsung S23 S24 pixel 7 8 n.k
Hapo kwenye android Sipingani na ww mkuu maana hao IOS Sijawahi kuwaza nasikia wana zuia baadhi ya apps na mimi apps zangu nyingi sio Official
 
Mimi ni mpiga picha, ukitaka camera nzuri, yenye quality nzuri lazima itabidi ujifunze na kuedit hizo picha. Kwa shughuli yako hiyo 2m iweke kwenye simu mkuu, utaokoa muda mwingi sana.
 
Naona wadau wengi wanashauri IPhone
Vipi kuna trick ya kuweza kutumia unauthorized apps mfano GBWATSAP,?
Maana nasikia wana apps zao

Kwanini utumie WhatsApp GB? Wewe deal na WhatsApp business na WhatsApp ya kawaida.
App Store ina application zote za kutumia na ni free kitu utakacholipa ni Apple Music na sio lazima.
 
Asanteni Wakuu kutokana na mashauri yenu nadhani iphone 13 pro max itanifaa
 
Back
Top Bottom