Ndama Jeuri
JF-Expert Member
- Jul 9, 2015
- 1,520
- 1,504
Habari za asubuhi wana jukwaa la sheria,
Kama kichwa cha mada kinavyojieleza hapo juu. Nipo kwenye mahusiano na binti mmoja wa miaka 23, nilifanikiwa kwenda kwao kujitambulisha na nikawa kwenye mpango wa kupeleka posa mwezi January mwaka huu, lakini ukatokea mvutano baina ya mama yake binti na mimi kuhusu suala la imani, mama yake binti akitaka nifuate imani ya mwanawe ili nimuoe binti yake, nilimwambia binti tubaki marafiki na uhusiano uvunjike kwa kuwa sitaweza kabadili imani yangu.
Baada ya kumwambia hivyo tulikaa siku kadhaa bila mawasiliano, lakini baadae alinitafuta kwa njia ya simu na kuniambia kuwa mama yake ameridhia yeye kubadili imani kunifuata mimi. Nikamuelewa mapenz yakarudi na ghafla akanasa ujauzito kipindi kile kile kifupi tangu aniambie mama yake hana tatizo Tena kwenye imani.
Nikamueleza kwa kuwa tayari una ujauzito mueleze mama yako unaenda kubadili Imani ili nilete posa tufunge ndoa haraka before huo ujauzito haujafika hata mwezi,binti akaanza kupiga chenga kumueleza mama yake, baada ya kumsumbua sana kwa wiki kadhaa akanipa jibu kuwa nimuoe Kwanza then atabadili dini akiwa kwangu, nadhani hakuna imani yoyote inaruhusu hilo iwe ya kikristo au kiislamu, yafaa umkili kristo ni bwana na muokozi wa maisha yako ndipo uoelewe na mkristo au ukili Mungu ni mmoja (Allah s.w) na Muhammad ni mjumbe wake ndipo uolewe na muislamu.
Hapo nikagundua kuwa binti aliongopa kuwa mama yake ameridhia abadili imani. Ikabidi nimtafute mama yake mdogo ambaye yeye imani yake inaendana na ya kwangu, kwani hata mama yake na huyu binti alibadili imani kumfuata mwanaume aliyemuoa sasa. Nikamueleza hali halisi na yule mama yake mdogo akanambia kuwa atamueleza dada yake ambaye ni mama yake na binti kuwa binti abadili dini ili posa iletwe,japo aliniambia kuwa mama yake hataki mwanawe abadili imani ila atazungumza naye.
Alimpigia simu na kumueleza suala hilo,lakini cha kushangaza usiku wa saa 4 siku hiyo aliyozungumza na mdogo wake, mama wa yule binti alimleta kwangu yule binti, kwa bahati mbaya sikuwepo nyumbani nilikuwa kazini, akamuamsha jirani mmoja na kumkabidhi yule binti, nikirudi kazini nikabidhiwe. Nilipopigiwa simu usiku na yule jirani nikamuambia amfungulie mlango yule binti kwa kuwa alikuwa na ujauzito wangu na sikuwa tayari kumtelekeza,nakumbuka ilikuwa tarehe 02/01/2020.
Niliporudi asubuhi toka kazini sikutaka kwenda kwao binti nikaa kimya tu kwa vile mama yake alikuja kwa uhasama. Mama yake baada ya kuona kimya akamwambia binti yake arudi, Binti akagoma kurudi ikabidi niletewe wito wa kwenda pamoja na mshenga wangu, nikaenda ukweni lakini nilipofika shutuma za kwanza nimemtorosha binti yao, hivyo nipigwe fine ya laki 2 pamoja na posa ya laki 2 na nikaambiwa wao wanahitaji mahali tu.
suala la nani,wapi tutafunga ndoa, tutajua wenyewe, kweli nilikaa siku kadhaa nikawapelekea hiyo laki 4 ,wakatoa majibu ya posa siku hiyo na waliorodhesha vitu vingi kweli kwa ujumla vilifikia 2,174,000. Baada ya siku kadhaa kupita nikapela pesa yote hiyo,walipo fikishiwa hiyo pesa wakasema kuna baadhi ya mambo hayajakamilika hivyo ni vizuri mshenga wangu afanye utaratibu wa kunichukua mimi pamoja na binti tuende kwa wazazi wake, hilo suala nikamgomea mshenga.
From there nikawa sina ushirikiano na familia ya binti na binti amenigeuka ananilazimisha kuwa lazima niwe Na ushirikiano na familia yake na sasa binti amebakisha miezi 2 ajifungue. Nataka kuvunja uchumba,na binti nimemwambia kuwa suala la kumuoa nimeshalifuta.
Amewaeleza kwao,na kwao wamemuambia kuwa aniambie nimtafutie pa kukaa kwavile itakuwa aibu kwake, kukaa kwa mwanaume muda mchache then akaachika. Nilikaa naye na kumvumilia kutokana na hali yake ujauzito lakini nimegundua kuwa hajihurumii.
Nataka nimtoe kinguvu nimpeleke kwao.
Na nikawaeleze wazazi wake kuwa nimevunja uchumba. Naomba msaada wa kisheria kama kutakuwa na sehemu nitakosea juu ya uamuzi wangu?.
Au Kama kutakuwa na utaratibu mzuri wa kisheria wa mimi kuufuata ili wasiweze kuutumia ujauzito na mtoto anayetazamiwa kuzaliwa kama mgodi wa kuchimba hela.