Habari za asubuhi wana jukwaa la sheria,
Kama kichwa cha mada kinavyojieleza hapo juu. Nipo kwenye mahusiano na binti mmoja wa miaka 23, nilifanikiwa kwenda kwao kujitambulisha na nikawa kwenye mpango wa kupeleka posa mwezi January mwaka huu, lakini ukatokea mvutano baina ya mama yake binti na mimi kuhusu suala la imani, mama yake binti akitaka nifuate imani ya mwanawe ili nimuoe binti yake, nilimwambia binti tubaki marafiki na uhusiano uvunjike kwa kuwa sitaweza kabadili imani yangu...
Hakuna sheria yeyote hapo serious ya kukufunga, ukiishi na mwanamke kwa miaka 2 (I think) bila ndoa ana Kuwa conaidered mke kisheria!
Huyo ni muasherati mwenzako mmepeana mimba, ila issue hapo ni hiyo mimba, ambayo it will drain you kifedha!
Cha kufanya, muache huyo Mtoto hapo wewe kaa kwingine ila mhudumie kila kitu maana ni majukumu yako!
Usiendelee kula utamu wa watu, hapa ndo huwa utalogeka na hautatoboa nakuhakikishia!
Akijifungua mnunulie makorokoro kibao aone raha, ataenda kwao kuhudumiwa na mama yake, toa Support nzuri kabisa!
Akishaenda kwa Mama yake kuhudumia, wewe hamisha Nyumba kusikojulikana, ila usimwambie mtu!
Endelea kumpa some amount monthly akiwa kwao, fanya kwa mpesa na wema record kabisa itakusaidia baadae!
Usije ongelea au kukubali tena kuishi naye, wataenda ustawi wa jamii, wewe nenda waambie huna mpango naye, onyesha Support yahela na receipt zote za kuhudumie Mtoto!
Sasa kama wewe ni muhuni na utakuja kukwepa gharama za Mtoto usije fuata Huu ushauri, Mtoto ni jukumu lako na ni lazima umlee’