Naomba ushauri wa kupata simu ya nzuri za iPhone

Yaani A20 unalinganisha na iPhone 7 [emoji23][emoji23] nyie watu nyie. iPhone 7 ni flagship na A20 ni low budget phone. Ilinganishe na akina S8 huko. Size ya kioo isikuchanganye. Ingekuwa hvyo basi Infinix ndio zingekua simu zenye uwezo kuliko zote
mimi mwenyewe sijamwelewa hata.

pamoja na kuwa a20 ni lowend bado,inaweza kuchallenge iphone 7 sehemu kubwa sana.
camera no
bettry yes
display yes
durability no
 
We nawe jaribu jifikiria Samsung A series tena 10 au 20 ,iphone ikiwa ni ya mwaka 2010 basi chukua na flagship ya samsung ya mwaka huondio linganisha yaan flagship kwa flagship
 
Yaani A20 unalinganisha na iPhone 7 [emoji23][emoji23] nyie watu nyie. iPhone 7 ni flagship na A20 ni low budget phone. Ilinganishe na akina S8 huko. Size ya kioo isikuchanganye. Ingekuwa hvyo basi Infinix ndio zingekua simu zenye uwezo kuliko zote

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Mkuu takuwa nimechanganya model ya simu lakini ilikuwa na Ram 2gb na memory 32 gb
Hivo zote zinalingana Ram sawa ndo mana tukazilinganisha
 
Uzi mzuri sana. Samsung simu nzuri sana sema ikipasuka kioo bahati huna na utalia bure.
Nilikua na iphone 7,google 2xl na galaxy note 10 plus.
Galaxy note 10 plus imepasuka kioo nimeambiwa ni 720 kioo, nimeamua kuiweka ndani nimeongeza iphone 8 kwenye list na kwakweli sijutii.
Camera bomba,charge inajitahidi kulinganisha na iphone 7,napata muda vizuri wa kuedit pics,kufanya kazi za office mpaka nasahau kutumia laptop wala ipad,kwa ujumla mimi ni heavy user ila iphone 8 nimeipenda.

Nashauri anunue kama ni iphone kuanzia 8 ataona kitu,seven hapana
 

Attachments

  • IMG_0259.jpg
    114.3 KB · Views: 23
Zinaendaje kwa mtumba uliochangamka ambao ngozi nyeupe hawajauchosha sana
 
Mkuu kwa budget yako I suggest iPhone 7 plus tena uipate ile matte black aisee ni bonge moja la simu executive kimuonekano πŸ’ͺ whether refurb or used one in good condition. Kuna machimbo ya uhakika kabisa unaipata hiyo iliyotulia bila papara nakushauri utulie ufanye research kwanza. Aisee mimi ni iPhone enthusiast huniambii kitu nilishaitumia hiyo, wahuni waliipiga pale Tips mida mibovu nikahamia Samsung chap na uchumi ule wa Hayati Uncle Magu πŸ˜† Nasikilizia hizi za sasa watoe ile notch tu pale juu nirudi fasta πŸ˜‚
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Mkuu takuwa nimechanganya model ya simu lakini ilikuwa na Ram 2gb na memory 32 gb
Hivo zote zinalingana Ram sawa ndo mana tukazilinganisha
Shida sio RAM wala storage, shida ni SoC ndio inaweza kufanya simu kuwa slow au fast. Hzo simu kma a20 zina CPU weak sana ukilinganisha na flagship phone za bei ya juu zilizokua na CPU zenye nguvu. Usifikiri simu ikiwa na 8GB RAM ndio inakua fast. Kma CPU ni kimeo hata ikiwa na RAM GB 24 itakua slow tu kwenye operation. Hyo iPhone 7 unatakiwa kuilinganisha na Galaxy Note FE or S8 ndio generation za flagship zinazokaribiana nayo.
 
Hayupo siriaz huyo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kaka hebu tupeane elimu hapo kwenye SOC mana watu wengi tunajua ram kubwa ndo spid ya simu,sasa naomba tusaidiane hio SOC ni kitu gan na vip yenyewe ndo inafanya simu kuwa slow au na spid
 
Hahaa asante sana mkuu
 
Saiv natumia Samsung J5 prime ndo nataka nitafute sim nyingne nzur ambayo ni current.
 
kaka hebu tupeane elimu hapo kwenye SOC mana watu wengi tunajua ram kubwa ndo spid ya simu,sasa naomba tusaidiane hio SOC ni kitu gan na vip yenyewe ndo inafanya simu kuwa slow au na spid
SoC by definition ni System on Chip. Kwa technology ya simu ilivyo hii SoC ndio chip inayocontain CPU ya simu, Modem ya simu (kwaajili ya network), Image signal processor au ISP (hii ndio ina fanya process zote za kuchukua picha kutoka kwenye camera na kuprocess kuwa nzuri), Graphic processing unit au GPU (hii ni kwa ajili ya vitu vyote vinavohitaji nguvu ya kuprocess graphics zake kma games na baadhi ya apps), Artificial Intelligence processors, audio and video decorder zinawezesha kuplay audio na video za format mbali mbali na zingine zina hata RAM humo humo.

Sasa hapo umeona kuwa SoC ina kuwa na vitu vyote hvyo, ikiwa weak basi na hvyo vitu vyote hapo vitakua weak.
SoC za simu zinatoka kwenye company mbali mbali lakini zinazofahamika sana ni Qualcomm, Exynos, MediaTek, Spreadtrum, Apple A series na Hisilicon

Apple A series ndio the best of the best kwenye performance ya CPU na GPU. SoC ya Apple ya mwaka husika ukilinganisha na SoC ya Qualcomm kwenye mwaka huo mara nyingi za Apple zinakuwa na CPU na GPU performance kubwa kidogo kuliko za Qualcomm.

Kwa upande wa Android Qualcomm ndio wanatengeneza SoC nzuri kuliko wote wakifatiwa na Exynos ya Samsung and Hisilicon ya Huawei. MediaTek nao wanatengeneza SoC nzuri ila sio sana na wanajulikana kwa kuwa na SoC mbaya za bei ndogo ndio unazoziona kwenye Tecno, Infinix, itel, masimu ya kichina na simu za bei rahisi kutoka kwa Xiaomi na Samsung (kma hzo A10).

Lakini pia kila company ina category mbali mabli. Low end, midrange na high end. Hizi SoC zina majina yake. Kwa mfano ukichukua simu kma Samsung Galaxy S20 zinakuwa na SoC ya Qualcomm Snapdragon 865 or Exynos 990. Hizi ni flagship SoC zenye uwezo wa hali ya juu. Lakini simu kama Samsung Galaxy A10s ina SoC ya MediaTek Helio P22 ambayo ni ndogo na haina uwezo mzuri.

Kujua SoC ya simu yako tumia app ya DevCheck au Device Info HW na angalia kundi la Hardware or SoC utaona jina la SoC ya simu yako. Pia unaweza tafta SoC ya simu online kwa kuangalia specification zake.

Ukishajua jina la SoC basi unaweza linganisha na SoC ya simu nyingine kujua zinazidiana vipi uwezo. Kwa mfano mimi simu yangu ina Snapdragon 855 nataka nilinganishe na Samsung Galaxy A51 yenye Exynos 9611. Nitaingia Google kisha nitaandika Snapdragon 855 vs Exynos 9611 kisha utachagua website ya nanoreview.net au versus.com na kusoma tofauti zake na ipi inamzidi mwenzake.
 
Saiv natumia Samsung J5 prime ndo nataka nitafute sim nyingne nzur ambayo ni current.
Sawa mkuu ila kwa kuzingatia budget yako if you really need the iPhone go for iPhone 7 plus the phone is so superb performance-wise plus ule muonekano mmoja executive na amazing kama ni matte black you will feel the taste of it πŸ’ͺ hata mpunga ukate nifikirie iPhone bomba ya chap kwa low budget I will go for iPhone 7 plus specifically matte black one πŸ’ͺ kwahiyo tuliza akili babu upate chimbo la maana ukwee kitu bomba hiyo, wadau tumeshakupa options usibabaishwe na miluzi mingine isiyo na tija kwa taifa babu.
 
daaa kaka big up sn nadhan umetoa elim kubwa sn na hakika umesaidia wengi sn

Big up sn
 
Hahahaa asante sana mzee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…