Naomba ushauri wa kusoma "Masters"

Naomba ushauri wa kusoma "Masters"

Project management is the best for you, kwa degree yako, hii itakufaa, ukiwa na fursa ya kusoma soma.
Hatakiwa kupoteza mwaka na usher kusoma master ya hii kozi. Yeye asome development studies ambayo ndani yake kuna elective ya project management.

Ila afanye kazi kama miaka 3 ndio atapata uelekeo wa nini asomee.
 
Ahsante mkuu nimepokea ushauri wako kwa mikono miwili
 
Mdogo wangu hongera sana, ulileta taarifa zako JF wakati umegraduate hiyo ni Sawa kabisa. Baadae ukaleta taarifa jinsi ulivyoulizwa maswali ya interview hii ni sawa pia.
Baada ya hapo tunasema Ahsante MUNGU umepata Ajira!
Kwakuwa sasa Umeajiriwa na Miongoni mwa Viapo ulivyosaini ni kutoongelea inshu za mwajiri wako yaani serikali popote nashauri ubadili mada za kuleta JF, Mambo yako ya kazi yabaki kuwa Siri yako. Narudia stori za Ofisini na Watu wa Ofisini ziache kwenye geti la Halmashauri mdogo wangu. Leo umekuja na inshu unatafuta ushauri wa kusoma wakati hata bado hujathibitishwa kazini.
Utanogewa kesho utakuja na jipya.

Ni wakati wako sasa uweke Strategies za kubadilisha elimu yako ibadilishe maisha ya Wananchi wa Halmashuri yako.

Ni wakati huuu unapaswa kuleta hoja za mikakati na njia zipi sisi Walalahoi tunaweza kujikomboa kwenye umaskini. Tumekuombea dua hapa hapa JF utoboe hebu sasa tulipe fadhira kwa Usomi wako na nafasi yako, achana na papara ka popocorn kikaangoni, tulia tuliiiiii acha mapepe Ofisini.
Ishi kama mjinga usiyejua lolote ila ukipewa kazi unaipiga kwa usahihi wa 100%.
Acha kuchangia mada za Majungu na kumponda boss wako wakati mwingine machawa wapo kazini na huenda wakakurekodi kabisaaaa.
Punguza lopo lopo na mipango miiiingi hadharani bw mdogo.
Jitofautishe kiutendaji na maafisa uliowakuta, tengeneza to do list zako za siku wiki au mwezi, na ukiweza jipe cheo cha back up ya mipango ya idara.
Kumbuka baada ya miezi 12 DSO wako ataombwa taarifa zako za upekuzi ili uthibitishwe kazini, endapo utadharau andiko hili vetting yako yaweza kutoka lkn ukiwa ratted as Rubbish and unpontential staff.
Anyway kila mtu aishi anavyotaka tusipangiane brooo. Mimi nilikua nawaza tuuu jinsi ningekuwa mimi ningeishi. Kineheeee......Kwaheri Ngosha.
📌📌🔨🔨
 
Suala la elimu katika hii nchi ni gumu sana,nimekutana na watu wengi wenye elimu za juu lakini napataga mashaka kama kweli wana elimu hizo ama walipewa ,
Elimu itakayotusaidia ni technical tu i.e zinazopatikama Arusha tech,Must,Dit,nk..
Vijana tujaribu kuondoa dhana ya kuajiriwa na tufikiri kuajiri
Ajira ni mbaya,ajira haina uhuru,ajira ni kama asali ya wizi
 
unaenda kusoma kwa ajili ya mtu, au kwa ajili yako? Km hujui unachotaka kusoma sasa kwanini utamani kwenda kusoma? Hayo ni mambo yako binafsi
Wenzetu wana category ya CAREER DEVELOPER. Kazi yake kuu ni kushauri watu juu ya caree development bila kujali status of education. Hata chuo kuna mshauri wa kitaluma.
Katka karne ya 21 ya utandawazi mambo ni mengi na unaweza kufikiri umehitimu na kujua mambo mengi kumbe una ombwe la ufahamu wa cross cutting issues kisha unabaki kizamani.
Kuna watu wanafanya tafiti na ufuatiliaji wa career mbalimbali na kuwashauri watu wa 'cope ' vipi na wakati.
Kwenye ajira penyewe kuna seminar nyingi za kujenga uwezo.
Wewe kama mzoefu mpe mwelekeo wa kitaaluma utaomsaidia ku 'ope' na mifumo ya serikali na dunia.
Makazini kwetu hakuna MENTOR WALA COUCHER wa kumkuza kiutumishi.
Asibezwe sana kisa ana digrii.
 
Suala la elimu katika hii nchi ni gumu sana,nimekutana na watu wengi wenye elimu za juu lakini napataga mashaka kama kweli wana elimu hizo ama walipewa ,
Elimu itakayotusaidia ni technical tu i.e zinazopatikama Arusha tech,Must,Dit,nk..
Vijana tujaribu kuondoa dhana ya kuajiriwa na tufikiri kuajiri
Ajira ni mbaya,ajira haina uhuru,ajira ni kama asali ya wizi
Huyu ni muajiriwa anayetaka kujiendeleza. Hana huo muda wa kufanya ufundi.
Elimu ya kijamii. nayo ni muhimu.
 
Jaribu kunitumia mimi ujumbe.

Wenzetu wana category ya CAREER DEVELOPER. Kazi yake kuu ni kushauri watu juu ya caree development bila kujali status of education. Hata chuo kuna mshauri wa kitaluma.
Katka karne ya 21 ya utandawazi mambo ni mengi na unaweza kufikiri umehitimu na kujua mambo mengi kumbe una ombwe la ufahamu wa cross cutting issues kisha unabaki kizamani.
Kuna watu wanafanya tafiti na ufuatiliaji wa career mbalimbali na kuwashauri watu wa 'cope ' vipi na wakati.
Kwenye ajira penyewe kuna seminar nyingi za kujenga uwezo.
Wewe kama mzoefu mpe mwelekeo wa kitaaluma utaomsaidia ku 'ope' na mifumo ya serikali na dunia.
Makazini kwetu hakuna MENTOR WALA COUCHER wa kumkuza kiutumishi.
Asibezwe sana kisa ana digrii.
Ahsante sana mkuu, hakika umenena vyema sana wengine humu wanadhihaki, kijembe na kejeli wakati mimi jambo langu ni kuomba ushauri utakaonisaidia kusonga mbele.
 
poleni na hongera kwa majukumu ya kila siku, naomba niende moja kwa moja kwenye mada. Kimsingi nahitaji kusoma "masters" ila sijuwi ni kozi gani itanifaa na kuleta tija kwangu.

Ndugu wadau, naomba nianze kwa kujitambulisha binafsi kielimu nina shahada ya elimu ya watu wazima na maendeleo ya jamii yaani "bachelor of education in adult education and community development (Bed-Adec) kutoka chuo kikuu cha dodoma (UDOM).

Ndugu wadau, nimepata ajira mwaka huu baada ya kupambana na saili za utumishi, bahati nzuri Mungu amenyosha mkono wake na kuamuru nipate ajira serikalini kama afisa maendeleo ya jamii dadaja ll yaani "Community Development Officer grade ll (CDO) katika halmashauri fulani hapa nchini.

Ndugu wadau, lengo langu "from day one" ni kuanza maandalizi ya kusoma " masters" ila sina ufahamu wa kutosha kuhusu aina au kozi gani ya "masters" itakayonisaidia zaidi kunipeleka mbele kulingana na "field" yangu hii ya CDO.

NB: Naombeni maoni na ushauri wenu wa kina juu ya jambo langu hili kwani imekuwa muda mrefu sasa toka nimalize shahada yangu ya kwanza mwaka 2017.

#Nitashukuru sana kwa msaada wenu wa mawazo.
Fanya masters inayoendana na taaluma ya awali... mfano hiyo community dvt itakufaa zaidi!
 
Hongera sana mkuu kwa kupata ajira.

Kabla ya kuuliza ni masters degree gani itakufaa weka juhudi kwenye kupata uzoefu wa hiyo kazi kwanza. Fanya kazi kwa ufanisi uwezavyo, kwa kuwa upo halmashauri angalia mabosi wako wana nini cha ziada(kielimu). Utaona patterns ya aina za masters degree ambazo ni relevant kwenye field yako na career yako kiujumla. Maana wapo wenye masters hapo ulipo au kwenye halmashauri nyinginezo. Wengi wao ndio hao wakuu wa Idara, But kuwa mkuu wa Idara au Kitengo kigezo sio elimu peke yake bali na uzoefu kazini (seniority) na uchawa.

Pili, kuna wadau wameshakueleza ukweli. Masters haina mchango wowote kwenye kipato kwa kazi za halmashauri. Labda kukupa connection ya kupata cheo cha kiofisi (sio cha mfanyakazi). Kwa kada yako kusoma masters ni kama patapotea.

Tatu, kwa standing order ya serikalini kama sijakosea ni lazima ufanye kazi miaka mitatu (3) kabla ya kuomba likizo ya malipo kwenda kusoma. Hivyo nashauri focus kwenye kazi kwanza wakati unausoma mchezo.

Kama una ndoto za kusoma masters degree endelea kushikilia hapo ila usije ukawa disappointed hapo baadaye.

Notable masters degree zinazoweza kukufaa.

-Project Planning Management
-Social welfare
-Sociology
-Community Development
-Humanities
-Political Science
-Diplomatic Studies
-MBA
-Public Relations
MBA....(.......)
 
Back
Top Bottom