Naomba ushauri wako nasaha juu ya kufikia malengo ya kuku elfu 5 ndani ya mwaka mmoja na miezi sita

Hukumsikiliza (kumsoma) vizuri huyo uliyemjibu hapo.
Jibu lako hili halitatui tatizo aliloligusia.
Hilo tayari ni kosa lako namba moja katika kazi unayotaka kuifanya.

Mchanganyiko wa chotara na kienyeji halifuti tatizo la ufugaji wa hao kuku.
Nafahamu mkuu kuku wakienyeji ukuaji wao niduni nakuwafungia ndani Kwa muda mrefu nihasara, lakini Hawa namna nilivyoliweka Banda langu Hawa watakua wachache nawatakua nachumba chao , lakini pia hawa muda mwingine ntakua nawaachia wazurule wenyewe nakuwapa chakula Cha ziada pindi warudipo. Lengo hasa lahawa nikupata Mbegu mchanganyiko kati ya kienyeji na chotara Kisha nione ukuuaji wao.

Nafahamu ningumu Kwa kuku wakienyeji ufugaji wao lakini pia ntapenda zaidi kuwaona japo Kwa uchache .

Pia lengo hasa lamada hii nikuomba ushauri Kwa wazoefu kama nyinyi wapi niboreshe na wapi niache.

Asantee mkuu Kalamu
 
Adui mkubwa ni 'muda'.
Ningetamani sana kuchambua andiko lako toka mwanzo hadi mwisho nikuonyeshe makosa utakayoingia kwa namna unavyopanga kufanya hiyo kazi.

Kwa mfano tu: Huwajui vizuri hao kuku wa SASSO. Hao kuku hawaatamii mayai vizuri kama anavyofanya kuku wa kienyeji. Kwa hiyo hilo wazo tayari ingefaa uwe umeliondoa akilini mwako, na ufuate ushauri aliokupa mkuu 'Fursa' wa kununua mashine ya kutotolesha.

Funzo hapa ninalotaka kukupa ni hili: Katika biashara/kazi yoyote ile, kabla hujaianza, inafaa ujiandae angalau uwe na kiasi fulani cha elimu juu yake.
Hapa inaonyesha huna 'basic knowledge' kuhusu ufugaji wa kuku, na wala kuku wenyewe unaotaka kuwafuga huwajui tabia zake.
Miezi sita ya wao "kudondosha mayai", akama alivyokushauri mkuu'Fursa' na wewe kufurahia ushauri huo; mambo kama hayo ndiyo yatakayokufanya ushangae kulikoni, ukishafika huko.
 
Haya sasa!

Kumbe upo kwenye mpango wa kufanya "UTAFITI"? Huku ukitegemea unafanya biashara?
Huwezi kufanya biashara namna hiyo.

Kuku wa kienyeji na Chotara, usitegemee matokeo yenye ufanisi zaidi ya hao wazazi wao.
 
Hesabu za excell hizi!..... jipe miakà hata 5 uje utoe ushuhuda wa kuku 5000!....
Weka na haya
.kuibiwa mayai
.Kuibiwa kuku,
Vifo vyà kuku kutokana na magonjwa ya milipuko,
Chakula kutokua bora na vikuku kudumaa.
Wafanyakqzi kuacha kazi ghafla🤯
Kupanda bei za chakula ..
 
Nikuambie tu hayo mabanda uliojenga sio mabanda ya kuku na kama hujawahi fuga usiweke malengo makubwa hivyo kwanza usome mchezo alafu uingie mchezo kuku wakiwa wengi kitakachowafanya wasiendelee ni hewa bandani umejipangaje kwa hilo.

Umejifunza ufugaji wa cages? Umejifunza utawalisha kiasi gani cha chakula hao kuku 1500 au wakifika 5000 umejifunza ni aina gani ya chakula u ahitajika uwape na malengo yako mbali na kuwa na kuku kuku 5000 unazijua figisu za soko la kuku. Una mganga au unamtegemea Mungu.

Hili swali la mwisho lisikufikirishe moyo wako ulipo ndipo hazina yako ilipo
 
📌kuna michitara inagomaga kbs kuatamia...kufupi kaiandika as story not real kbs
 
Mko
Mkuu hiyo point ya mwisho mbona kama inatutia hofu Sisi ambao tuna malengo ya kuja kuwa wafugaji wakubwa.
 

Pitia huo uzi mdogo wangu,utajifunza mengi zaidi labda. Mwenyezi Mungu akujalie heri,nakutia moyo ufike utakapo na zaidi.
 
Mko

Mkuu hiyo point ya mwisho mbona kama inatutia hofu Sisi ambao tuna malengo ya kuja kuwa wafugaji wakubwa.
Point ipi ya mganga au ya ufugaji wa cages? Kama ni ya mganga natania tu japo hayo mambo yapo na kama ni cages ukitaka kufuga kuku wengi kwenye nafasi nzuri ni cages na wanakua sehemu salama na safi na hutapata gharama ya kujenge maukuta mengi kama jela
 
Hakuna hesabu za Excell mkuu wangu, nimejiandaa nabahati nzuri najifahamu hulka yangu sijawahi kufeli jambo labda hua nachelewa tu kufikia malengo. Niko tayari kukabiliana nachangamoto zitakazojitokeza.

Tusubiri huu Uzi utakua hai ntakua naleta mrejesho Kila baada ya mwezi mmoja au miwili.
 
Asante Boss wangu nashukuru Sana Kwa kujali kwako.
 
Haya sasa!

Kumbe upo kwenye mpango wa kufanya "UTAFITI"? Huku ukitegemea unafanya biashara?
Huwezi kufanya biashara namna hiyo.

Kuku wa kienyeji na Chotara, usitegemee matokeo yenye ufanisi zaidi ya hao wazazi wao.
Mkuu unapoanza biashara ambayo huifahmu kiundani, kunakua na darasa ambalo utaruhusu kufanya makosa nakujirekebisha nandio maana naamua project kuipeleka polepole. Ninauwezo wakufanya kama Jamaa anachosema lakini nafahamu changamoto zakuzalisha kuku wengi Kwa pamoja ambo soko lake nachangamoto zake sijazijua vizuri. Kwahio nahitaji mradi ukue polepole na nikabiliane na changamoto zinazojitokeza huku nikiendelea kupata uzoefu. Hata wewe mkuu wangu naamini hukuanza na kuku elfu 2 Kwa pamoja.
 
Mkuu Banda halina shida, kwasabau nibanda latofali na kuku niwachache kulifanyia mabadiliko inawezekana kadri kuku watavyoongezeka.
 
Asantee Kwa mawazo yako mkuu wangu.
 
Kuku 100 watakuchelewesha;Anza na mia 300 angalau. Bajeti ulioitaja hapo inatosha Hadi kuku 500 Kwa mwezi.

Usitake kujifunza utaumia. Tumia wataalamu hakikisha vifaranga vinapata chanjo zote nitakuwekua list hapa ya chanjo na mda wa kuchanja
 
We jamaa sijamtia Mori; ni kitu milikwisha kufanya tena Kwa kuku wa kienyeji matikeo yakawa mazuri kilichoniangusha ni msimamizi.

Naanza tena awamu hii naingia ubia na mwangalizi wa kugawana nae faida
 
Mkuu Banda halina shida, kwasabau nibanda latofali na kuku niwachache kulifanyia mabadiliko inawezekana kadri kuku watavyoongezeka.
Kuna muda wataongezeka hutahitaji mabadiliko utahitaji nafasi hebu piga hesabu zako vizuri
 
We jamaa sijamtia Mori; ni kitu milikwisha kufanya tena Kwa kuku wa kienyeji matikeo yakawa mazuri kilichoniangusha ni msimamizi.

Naanza tena awamu hii naingia ubia na mwangalizi wa kugawana nae faida
Nipo paleee utapigwa za kichwa hutaamini bongo hii hii ubia
 
Hapo pa wafanyakazi kuacha ghafla palisha nipiga na kitu kizito[emoji3]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…