Father of All
JF-Expert Member
- Feb 26, 2012
- 7,672
- 9,039
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hapo kwenye utatu mtakatifu ndio uwongo unapoanziaUsipouelewa utatu mtakatifu hutaelewa ukatoliki hivyo tulia
Ushirikina mtupu hamna lolote......Usipouelewa utatu mtakatifu hutaelewa ukatoliki hivyo tulia
MenuHapo kwenye utatu mtakatifu ndio uwongo unapoanzia
MenuUshirikina mtupu hamna lolote......
Utatu hauna ushahidi popote kwenye bibulia ni uzushi na ushirikina Yesu hajawahi kufanya ujinga huoMenu
Chagua lugha yako
Tafuta
Tafuta
MISA KWA KILATINI: MUBASHARA
RatibaPodcast
Fumbo la Utatu Mtakatifu sana ndilo Fumbo la Msingi la imani na la maisha ya Kikristo. Ni Fumbo la Mungu ndani yake mwenyewe.![]()
KANISA
Fumbo la Utatu Mtakatifu Ni Msingi wa Imani na Maisha ya Kikristo
Fumbo la Utatu Mtakatifu sana ndilo Fumbo la Msingi la imani na la maisha ya Kikristo. Ni Fumbo la Mungu ndani yake mwenyewe; ni chemchemi ya mafumbo mengine yote ya imani, nuru inayowaangaza. Hili ni fundisho la kweli ya imani. Imani Katoliki ndiyo hii: Tunamwabudu Mungu Mmoja katika Utatu na Utatu katika Umoja, bila kuchanganya nafsi, wala kutenganisha uwamo; kwani ni Nafsi ya Baba, nyingine ya Mwana na nyingine ya Roho Mtakatifu, ni umungu mmoja!
Na Padre Paschal Ighondo, - Vatican.
Tafakari ya Neno la Mungu katika Sherehe ya Fumbo la Utatu Mtakatifu. Kipindi cha cha Pasaka kimehitishwa kwa Sherehe Pentekoste. Tuko kipindi cha kawaida cha mwaka wa kiliturujia. Hivyo sherehe hii ya Utatu Mtakatifu tunaiadhimisha jumapili ya 8 kipindi cha kawaida na Jumapili ya 9 tutaadhimisha Sherehe ya Ekaristi Takatifu. Hii ni kwa sababu tulipofika juma la 6 kipindi cha kawaida tulianza kipindi cha kwaresima siku 40, majuma 5, na baadae Juma Kuu lilifunguliwa kwa dominika ya matawi kikifuatiwa na kipindi cha Pasaka majuma 7. Kumbe masomo ya jumapili ya 7, 8 na 9 kipindi cha kawaida mwaka B, 2024, hatutayatafakari kwa sababu masomo ya sherehe hizi yanachukua nafasi yao. Mababa wa Kanisa wanasema, Fumbo la Utatu Mtakatifu sana ndilo Fumbo la Msingi la imani na la maisha ya Kikristo. Ni Fumbo la Mungu ndani yake mwenyewe. Kwa hivyo ni chemchemi ya mafumbo mengine yote ya imani, nuru inayowaangaza. Hili ni fundisho la kweli ya imani. Imani Katoliki ndiyo hii: Tunamwabudu Mungu Mmoja katika Utatu na Utatu katika Umoja, bila kuchanganya nafsi, wala kutenganisha uwamo; kwani ni Nafsi ya Baba, nyingine ya Mwana na nyingine ya Roho Mtakatifu, ni umungu mmoja, wa Baba, na wa Mwana na wa Roho Mtakatifu; utukufu ulio sawa, ukuu wa pamoja wa milele. Rej. KKK 222-266. Utatu Mtakatifu ni Fumbo la imani kuwa katika Mungu mmoja kuna nafsi tatu, Mungu Baba, Mungu Mwana na Mungu Roho Mtakatifu. Kwa Utatu Mtakatifu tunafunuliwa upendo, wema, ukuu, mamlaka na huruma ya Mungu katika Nafsi hizi tatu. Ndiyo maana wimbo wa mwanzo unaofungua maadhimisho ya sherehe hii unasema wazi; “Asifiwe Mungu Baba na Mwana na Roho Mtakatifu; kwa sababu ametufanyizia huruma yake.”
![]()
Fumbo la Utatu Mtakatifu kiini cha imani ya Kanisa
Hili ni fumbo la imani kuwa hizi nafsi tatu za Mungu mmoja, zote ni sawa katika uasili na imani tu, yaelewa. Ndiyo maana Mama Kanisa katika sala ya mwanzo anakiri kuwa Mungu ndiye anayetufunulia hili fumbo na anazidi kumuomba atujalie ufahamu wake zaidi akisali; “Ee Mungu Baba, uliwafumbulia watu fumbo lako la ajabu, hapo ulipompeleka Neno wako na Roho Mtakatifu ulimwenguni. Utujalie kuutambua utukufu wa Utatu Mtakatifu wa milele katika kuungama imani ya kweli na kuabudu Umoja wa Mungu katika enzi ya fahari yake”. Ni katika Utatu Mtakatifu ndimo tunamopata ufupisho na simulizi la asili yetu tangu kuumbwa hata ukombozi kwa njia ya Yesu Kristo nafsi ya pili ya Mungu, ndimo zinamolala sala zetu na matumaini yetu kufikia utimilifu wa upendo kwa kuungana na Mungu aliye asili ya upendo. Somo la kwanza ni la kitabu cha Kumbukumbu la Torati (4:32-34, 39-40). Katika somo hili Musa anataja matendo makuu ya Mungu aliyolitendea taifa lake teule, Israeli. Hivyo anawakumbusha watu wake wawe waaminifu kwa Mungu wao. Maana Yeye ndiye aliyewatoa utumwani Misri na kuwaongoza katika nchi ya Ahadi. Aliwatoa katika tope la dhambi nakuwatakasa, hivyo wasirudie tena matapishi ya dhambi kwa kuabudu sanamu. Bali wazishike amri zake ili wapate kufanikiwa wao na watoto wao. Ni katika muktadha huu mzaburi alipotafakari makuu ya Bwana aliimba maneno haya ya wimbo wa katikati akisema; “Heri taifa ambalo Bwana ni Mungu wao. Kwa kuwa neno la Bwana ni adili, na kazi yake yote huitenda kwa uaminifu. Bwana huzipenda haki na hukumu, nchi imejaa fadhili za Bwana. Kwa neno la Bwana mbingu zilifanyika, na jeshi lake lote kwa pumzi ya kinywa chake. Maana Yeye alisema, ikawa; Na yeye aliamuru, ikasimama. Tazama, jicho la Bwana li kwao wamchao, wazingojeao fadhili zake; Yeye huwaponya nafsi zao na mauti; Na kuwahuisha wakati wa njaa. Nafsi zetu zinamngoja Bwana, Yeye ndiye msaada wetu na ngao yetu. Ee Bwana, fadhili zako zikae nasi. Kama vile tulivyokungoja Wewe (Zab. 33:4-6, 9, 13, 18, 20, 22).
![]()
Utatu Mtakatifu ni Fumbo la Imani katika Mungu mmoja Nafsi
Utatu hauna ushahidi popote kwenye bibulia ni uzushi na ushirikina Yesu hajawahi kufanya ujinga huo
View attachment 3232774
Eloi Eloi Lama sabakhtani " Mungu wangu. Mungu wangu mbona waniacha." Je alipokuwa mimba ina maana dunia haikuwa na Mungu? Je Mungu hakuwa na namna ya 'kuwakomboa' hao waliopotezwa na shetani aliyemtengeneza? Je Mungu asingemtengeza shetani, hawa watu wetu wangepotoshwa na nani? Je alimtoa kwa Mungu gani wakati yeye ndiye alikuwa baba yake? Maswali ni mengi kuliko majibu.
Usiseme kuwa ni uongo, sema ni ugumu (kwa baadhi lakini). Ndio maana likaitwa 'fumbo la Utatu Mtakatifu'Hapo kwenye utatu mtakatifu ndio uwongo unapoanzia
Yesu hapo alinena kwa Lugha hakuna ajuaye alimaanisha nini?