Sitasahau Mwaka 2017- 2018 ulikuwa Mwaka mchungu sana kwenye maisha yangu Baada ya kukutana na hii fursa ya forex. Nilipoteza pesa nyingi sana na muda. Nilitumia akiba ikaisha, nikauza gari labda nitarejesha hasara zangu, unapata leo profit ya $ 500 unafurahi kesho napoteza $ 2000, Mwisho gari ikaondoka, nikakopa benki dhamana nyumba, nilikopa Milion 10 pesa ikaondoka yote, Kuna shamba nilinunua huko Bagamoyo kama heka 5 nikauza kwa bei ya kutupa milion 9 nikawapa madalali Milion 1 nikabaki na 8 nikaenda, nikapigwa.
Nikafikia hatua mbaya hasa ya kuanza kuuza vyombo vya ndani, nikauza flat, nikauza set sofa nzima hahahaha jamani acheni ndugu nilichanganyikiwa. Mke ananishangaa tu. Mwisho nikasema yatosha, siwezi kuendelea kumfuraisha broker.
Bahati nzuri nilikuwa na pangale halijaisha Kigamboni, nikafanya mpango nikatafuta mteja kabla benki hawajaja kufanya yao, nikauza hii nyumba niliyokopea bei nzuri tukaenda benki Mteja(alikuwa mteja muelewa) akalipa deni la benki tukapewa hati tukaja tukamalizana. Pesa nikapeleka kumalizia pangale nikahamia nikawa nimebaki na kama milion 25 mkononi nikakimbilia kwenye korosho maana ndio ilikuwa biashara yangu kubwa, kilichotokea naamini mnakijua, Mpaka leo ninavyoandika Hapa pesa yangu haijarudi, Vitu ninavyofichukia kwenye maisha yangu kwa sasa ni Magufuli na Forex Mungu awatie lawana hawa mbwa. Leo kula yangu ya mashaka, napigania dadalala?????
Sent using
Jamii Forums mobile app