Naomba ushauri wenu wadau. Mechi za ugenini nipo vizuri, shida nyumbani

achana na uyo mwanamke wa dini tofauti uliyemuoa afu oa kati ya uliozaa nao njee asiwe dini tofauti pia hutojutia...
 
Wajumbe 7;17-28, "Naye mjuba atajitwalia mke kutoka imani nyingine, watazaa wana wanne, na kwa kuwa mjuba ana vina saba vya ubaharia basi hataacha kuchepuka, hivi, ili litimie lile andiko la kuwa BAHARIA HATAISHI KWA UGALI TU, BALI KWA MADIKO DIKO MBALIMBALI" Mwisho wa kunukuu, kwa hiyo mzee mwenzangu hii ni fate yako, huwezi kuiepuka, mi nikushauri tu kitu kimoja, PIGA MITI MZEE!
 
kiukweli nilimpenda sana na bado nampenda sana mkuu. Pia anapokuwa mbali na mimi kama vile kwenda safari kusalimia wazazi,nikibaki pekee nakonda. Nasema hivyo ili uwelewe kiukweli nampenda.
Sasa hujioni una shida? Mbona hutulii hata na huyo mchepuko mmoja? Ina maana nao Wana matatizo? We ni Malaya tu na hata Kinga hutumii utakufa kifo kubaya usababishie wanao shidaa
Na akijua hayo Mambo ya michepuko ndo balaa
 
Sasa hujioni una shida? Mbona hutulii hata na huyo mchepuko mmoja? Ina maana nao Wana matatizo? We ni Malaya tu na hata Kinga hutumii utakufa kifo kubaya usababishie wanao shidaa
Na akijua hayo Mambo ya michepuko ndo balaa
Jamaa ni mpumbavu sanaa alafu anasema ni Baba wa wa watoto wanne???? Shame shame yani unakojoaa kojoaa huko nje tuu as if una uwezo wa kulea kumbe unatengeneza watoto wa mtaani na masingle maza tu mtaani..


Tatizo sio kuwa dini tofauti na mkeo tatizo WEWE NI MALAYAAAA NA HUJIELEWII. Imeishaaa hiyoo
 
Mimi ni muislam nina mpenzi Rc tupo kwenye mahusiano muda mrefu tunapendana namuomba Mungu atufanyie urahisi tufikie malengo yetu dini sio kigezo kaa chini na Mzazi mwenzako mtatue matatizo yenu
Subiri mtakapo anza kuishi wote na kuzaa ndio utaona dini ilivyo kigezo, hiv unais utajisikiaje kwenda msikitin mwenyewe wanao Wanaenda kanisani? Ama yeye atajisikiaje kwenda kanisan peke ake watoto wanaenda msikitini?

Swala la dini lazma mlichukulie serious kwenye mahusiano yenu
 
Pole sana. Tatizo ni kuwa akiri yako haipo sawa unapo kuwa na mkeo.
Jaribu kukaa na mkeo mtatue changamoto zenu zote mrudishe aman mliyokuwa nayo wakati wa uchumba wenu.
 
Kwanza mnavutana kuhusu majina ya watoto ilhali wewe mwanaume upo! Simama kama mwanaume la sivyo utaisambaratisha io familia.
 
Ndiyo na kadhu amewanunulia na ushungi amewanunulia wa kike. Nimeziona Jana walipo niaga wanakwenda msikitini kusali eid
[emoji24][emoji24][emoji24][emoji24] weee unahitaji maombi wallah, hivi una umri gan?
 
Yaan nimesoma hii rhread nimejikuta natoa chozi, sion uanaume wako kabisaaah.

Ndani ya mahusiano halisi kuna matatizo makubwa, ukiwa km kiongozi wa familia umeshindwa kusolve, watoto wanapata usumbufu ktk majina, hadi kuabudu ktk dini, wee km mwanaume unatoa taswira ipi?

Haya umekimbia ndani kwenda nje nako pia unaongeza matatizo, tena sio kwa m1 bali ni wengi, unategemea uje kufanikuwa kwa mlolongo huo?

Nakupa poleeeh sana tena mnooh, nakuomba shirikisha wazazi wako, wazee wenye busara, na viongozi wa dini, nina amini utapata uvumbuzi wa matatizo yako, na kuwa ktk misingi bora ya maisha kwa familia yako.

Jah awe nawe na akafanikishe utatuzi wa matatizo yako.
 
Aseeeeeeeee! We mwanaume kama hujarogwa na mkeo basi we ni mwanaume wa aina yke
 
Jibu langu la kitaalamu japo huenda likakukera

Nyinyi wote na ni watu msio na maamuzi na hamna muelekeo mnaoufahamu katika dini haswa haswa

Amua kuachana nae oa utakaye landana nae kwa yale upendayo

Unatengeneza bomu kubwa kwako baadae na mzozo utakao uacha utasababisha uhasama kwa watoto hao unaozaa amua kuoa uanze kuzaa ndani ya ndoa
 
Hiyo point no 03 itolee ufafanuzi [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

One love
 
Mimi ni muislam nina mpenzi Rc tupo kwenye mahusiano muda mrefu tunapendana namuomba Mungu atufanyie urahisi tufikie malengo yetu dini sio kigezo kaa chini na Mzazi mwenzako mtatue matatizo yenu
Tatizo amekwisha jua udhaifu wangu ni watoto ndiyo maana ananifanyia vitimbi vya kuniweka nao mbali. Ananiambia dini yake inasema uisilamu unawatambua watoto ni wa kwake kwa sababu tumezaa nje ya ndoa.
 
Mkeo ana nguvu kuliko wewe ndio maana swala la watoto limekushinda kuhusu wasimame na imani ipi
Kiukweli Sipendi kuvutana kuhusu swala la watoto, nakuwa na hofu ya mungu. nahofia asije kuja kukasilika nakisha Kuamua kutunyang'anya ili tukose wote. Ndiyo maana naongea pasipo kutumia nguvu, najitahidi kutumia busara na hekima lakini hataki kunielewa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…