Naomba ushauri wenu wadau. Mechi za ugenini nipo vizuri, shida nyumbani

Naomba ushauri wenu wadau. Mechi za ugenini nipo vizuri, shida nyumbani

Kwani yeye hana wivu? Mbona wewe umechepuka na wanawake zaidi ya 4, na wengine umewazalisha, ila yeye hajafa?
Nimechepuka ili kujua kama nipo vizuri ama ninashida katika afya yangu ya kiume?
Kwasababu kila nikijisi nahitaji nafail kila nikikutana nae. Hilo tu mkuu
 
[emoji23][emoji23]kwa hiyo watoto anawapeleka msikitini. Kweli wanaume wachache
Tatizo la upole wangu na hofu ya mungu, katika imani ya kusema, "kama mnagombani hawa ni heri ni wanyang'anye tuone mtaringia nini tena "
Je wewe kama wewe huna hofu kama Mimi?
 
1. Unachepuka sana kiasi kwamba huwezi kuwa na hamu wala kutamani nyumbani

Kama sivo

2. Wewe na mkeo hakuna amani kati yenu kiasi kwamba inawavurugia hisia, uchu na kufubaza matamanio ya tendo la ndoa

3. Kufanya tendo bila breaks wala utaratibu kiasi kwamba inapoteza kabisa hamu ya kile ukionacho mbele yako

4. Uliyenaye anamazingira yanayokuudhi/maumbile yanayokutoa ham na hamasa. Tafadhali mnapo tafuta wenza zingatieni sana mfanano au maumbile na vigezo mnavovipenda.... compatibility or else mtaishia kuzichukia sehemu za siri za wenzi wenu na kupoteza kabisa hamu ya tendo.... ukitoka nje unakuwa fiti.

Wasalaam.
Sikuwa na michepuko tangia hapo,lakini yeye amesababisha kwa kunifanya nijihisi labda uwenda ninashida kwangu. Ndiyo maana nimejaribu kutafuta nje kujipima uwezo wangu upoje.
Ndipo nimejikuta nimejikuta nimezanao,sijapenda maisha yangu yapite hivi.
Kiukweli nimepitia kipindi kigumu, hakuna mwanaume anayependa awekewe vikwazo juu ya watoto wake. Kwa upole naomba rudia kunisoma tena mkuu
 
Dah kosa lako ni kuishi na MTU mwenye dini tofauti japo wataniona mbaguzi ila gharama yak ndio hio watoto wanakua wanang'inia hawajui waende wap .
Lakini mapenzi hayachagui mkuu, Pia nilihisi itakuwa rahisi kumshawishi anifuate mimi kama mume wake.
 
Habari wanajukwaa!

Moja kwa moja kwenye Mada. Binafsi ni family ya Mke na watoto 4, Pia tupo kwenye mahusiano kwa muda mrefu kidogo takribani miaka 12. Nasikitika hatujafunga ndoa, lakini tunaishi pamoja miaka yote hiyo. Tatizo ni dini zetu ni tofauti ( Mimi ni mkristo yeye ni muislam),lakini tayari nimekwisha mposa na mahali nimemtolea. Pia tunashirikiana vizuri kwenye swala la maendeleo.

Tukija kwa Mada iliyonifanya nije kwenu kuomba ushauri ni baada ya kukosa kuwa na hamu ya kushiriki naye tendo nikiwa naye. Imenitokea mara nyingi kidogo niwapo na yeye faragha, hatakama nitakuwa nina uhitaji wa kushiriki lakini nikianza kutaka kumuanda naniiii inanywea inakosa nguvu. Kiukweli ninaumia sana.

Pia, naomba niwafahamishe ya kwamba mimi na yeye tumekuwa kwenye mivutano kwa muda mrefu kiasi aswa kuhusu ndoa, dini na watoto kwenye kuwapa majina. Naamini ndipo tatizo langu la kukosa hamu nae kwenye tendo lilipoanzia. Kiukweli limekuwa likinikosesha raha kwa sababu Nahofia masela wanaweza kupita na Mke wangu especially kazi kwake.(kiukweli nampenda mama watoto wangu).

Pia naomba kukili kwenu nimenza kuchepuka ndipo nilipo kuja kugundua tofauti iliyopo kwangu dhidi yake. Dhumuni ya kufanya hivyo kutaka kujua kama Mimi ninashida gani hadi kushindwa kutoa huduma vizuri kwa mwenzangu?

Nilichokifanya nimejikuta nafanya vizuri kuliko kawaida. Si mara moja nimefanya hivyo,pia nimefanya kwa wanawake 4 tofauti, wa wili wanawatoto wangu copyright na Mimi Pia wanafanana na watoto wangu wanyumbani tofauti rangi. Kiukweli Nimeshindwa kuwakataa kwa jinsi tulivyo fanananao.

Pia mwingine ni mjamzito amekwisha niambia amegoma kutoa, ingawa na mimi sikutaka itoke kimoyo moyo lakini nilimuhada kuitoa. Kwa sasa inamiezi 7 yupo mbioni kujifungua, huyu nimekwisha mwambia ninafamilia lakini ameniambia nisihofu wala hatonisumbua lakini ameniamba atamtunza mtoto wake, lakini ameniomba siku ya kujifungua niwepo.

Kiukweli najuta kuwemo kwenye kadhia hii lakini yote amesababisha Mke wangu kwa kuwa mgumu na kuendekeza ushindani ambao ahuna kichwa wa miguu kwa faida na usalama wa mahusiano yetu.

Kiukweli nimekuwa muanga kila ninapogombanae itanilazimu kumtafuta mwanamke (uwenda naweza kumtokea mwanamke ambae uwenda nilitokea kuvutiwa nae), nipoe kwa kushiriki tendo lakini si na yeye, hapa ndipo idadi inapozidi kuongezeka nje ama narudi nje kwa wale wa mwanzo niliozaa nao.

Pia nakili mwanzoni hawakujua kama ninafamilia,kwa sababu Mke wangu hapendi niwe natoka na watoto sababu anahofia naweza kuwapeleka kanisani.

Naomba ushauri wenu wadau wa jamiiforums.
Zinaa haijawahi kumuacha mtu salama...
 
Sasa hujioni una shida? Mbona hutulii hata na huyo mchepuko mmoja? Ina maana nao Wana matatizo? We ni Malaya tu na hata Kinga hutumii utakufa kifo kubaya usababishie wanao shidaa
Na akijua hayo Mambo ya michepuko ndo balaa
Najua umeongea kwa hisia sana,lakini tambua nimeathirika kisaikorojia. Kitu peke Nilichokifanya nikujihisi nalipiza kisasi kama vile kutaka kumfanya aumie. Na ikiwezekana abadilishe muelekeo wake, nakuja kuniomba radhi maisha yaendele. Lakini natambua hayatakuwa kama zamani.
 
Nimechepuka ili kujua kama nipo vizuri ama ninashida katika afya yangu ya kiume?
Kwasababu kila nikijisi nahitaji nafail kila nikikutana nae. Hilo tu mkuu
Hata yeye atachepuka ili aone kama anakasoro au la? Haiwezekani mumewe achepuke ilhali yy ni mzima.
 
Jamaa ni mpumbavu sanaa alafu anasema ni Baba wa wa watoto wanne???? Shame shame yani unakojoaa kojoaa huko nje tuu as if una uwezo wa kulea kumbe unatengeneza watoto wa mtaani na masingle maza tu mtaani..


Tatizo sio kuwa dini tofauti na mkeo tatizo WEWE NI MALAYAAAA NA HUJIELEWII. Imeishaaa hiyoo
Nashukuru kwa mchango wako mkuu,Lakini usiombe yakufike.
 
Hata yeye atachepuka ili aone kama anakasoro au la? Haiwezekani mumewe achepuke ilhali yy ni mzima.
Nimekuelewa mkuu ngoja niaze kufikiria kuachana ili tusije kuumizana zaidi
 
Nimechepuka ili kujua kama nipo vizuri ama ninashida katika afya yangu ya kiume?
Kwasababu kila nikijisi nahitaji nafail kila nikikutana nae. Hilo tu mkuu
Mkuu kuzalishaaa sio kwamba unaweza kumridhishaa mwanamke...!! Unaweza kuwa unamwaga mbegu lakini ngoma haisimami muda mrefu au haina nguvuu sasa hapo utazidi kuzaa ovyo ovyoo tuuu ukidhani ndo kipimo cha kumridhisha mwanamke...
 
Kiukweli Sipendi kuvutana kuhusu swala la watoto, nakuwa na hofu ya mungu. nahofia asije kuja kukasilika nakisha Kuamua kutunyang'anya ili tukose wote. Ndiyo maana naongea pasipo kutumia nguvu, najitahidi kutumia busara na hekima lakini hataki kunielewa.
Pole mkuu
 
Mkuu kuzalishaaa sio kwamba unaweza kumridhishaa mwanamke...!! Unaweza kuwa unamwaga mbegu lakini ngoma haisimami muda mrefu au haina nguvuu sasa hapo utazidi kuzaa ovyo ovyoo tuuu ukidhani ndo kipimo cha kumridhisha mwanamke...
Hilo nalo neno mkuu, lakini vyote nimezingatia ndiyo maana nimekuja kwenu nakujieleza kipinikipi mkuu. Binafsi nimeangalia nimerudia mara ngapi pia ametoa mara ngapi. Kwanza kitendo cha kumfanya aende mara 2,kwangu nikipimo tosha. Binafsi siwezi kuanza kutoa mimi kabla ya yeye,nitajitahidi kujizuia ilimladi atoe kwanza.
 
Najua umeongea kwa hisia sana,lakini tambua nimeathirika kisaikorojia. Kitu peke Nilichokifanya nikujihisi nalipiza kisasi kama vile kutaka kumfanya aumie. Na ikiwezekana abadilishe muelekeo wake, nakuja kuniomba radhi maisha yaendele. Lakini natambua hayatakuwa kama zamani.
Poleee
Matendo yako mapya yatachangia Sana maisha kurudi Kama zamani kwa kiasi kikubwa, afu muoe kabisa apate Aman ya roho
 
Nimechepuka ili kujua kama nipo vizuri ama ninashida katika afya yangu ya kiume?
Kwasababu kila nikijisi nahitaji nafail kila nikikutana nae. Hilo tu mkuu
Msome jamaa mmoja anaitwa Idd Makengo Facebook au Instagram atakusaidia Sana.
Wewe una insecurity ndo inakusumbua lakin huna shida yoyote Ni hujiamin tuu
 
We ni mzinzi mkuu, achana na visingizio vya unajaribu kuona una tatizo gani.

Ushauri: kuwa mwislamu oa mama watoto wako wote, dini inaruhusu au acha uzinzi utapona.
 
Hapo ndo napooonaga Dini miyeyusho yaani Mungu huyu huyu mmoja lakini hataki muislam amuoe mkristo mpaka abadili dini..
 
Back
Top Bottom