umeshawahi kusikia msemo tembea uone mambo? basi ndio hayo sio kila unalosikia ni kweli, watu wanapenda kutia chumvi wanapohadithia maisha na mapirika ya walipo, hawasemi yote na huwezi kuyajua yote hadi pale ukienda mwenyewe na kuona kwa macho yako. Mfano ni huo ulosema kuwa hakuna wakati wa kupoteza kwa ajili ya kazi, sio kweli, mimi binafsi kwa mfano, nafanya kazi jumatatu hadi ijumaa saa tatu hadi kumi na moja na nusu, week end niko off, natumia siku hizo kupumzika, kufanya mambo yangu ya binafsi nyumbani, kwenda kuona mechi za mpira, kutembelea rafiki na jamaa pamoja na kuwasiliana na walio nyumbani. Mara chache huenda ofisini kama kuna jambo muhimu au kama niko nyuma katika moja ya kazi zangu. Sasa tu kwa kuwa wako watu wengine kwa sababu zao wenyewe hutafuta kazi za week end kuongezea na kazi ile ya jumatatu hadi ijumaa, hapo ndio tena wanapowaambia kuwa maisha ya nje hakuna kupumzika au kupoteza muda, lakini ukweli ni kuwa huo ni uamuzi wao na sio hali halisi ilivyo kwa kila mtu. Nadhani umenielewa kidogo.