Naomba ushauri wowote kuhusu safari yangu ya muziki, sikutegemea itakua ngumu kiasi hiki

Alexido jz instagram

JF-Expert Member
Joined
May 5, 2026
Posts
4,686
Reaction score
10,018
Asee ndugu zangu mnaweza ona nazingua lakini si kweli wakuu, inafika hatua nashindwa kabisa, nilifikiri ni sana lakini mambo nayaona tofauti MNO.

Nahitaji kushare mawazo na nyie ndugu zangu labda kwa chochote mana naona naelekea kushindwa.

Payments za kurekodi na video shooting, zilikua sawa sasa changamoto zingine zikaibuka kuangalia mbele mtiti ukaanzia hapo, just imagine sikua na media tour yoyote, influencer yeyote wa kupromote kazi YANGU, yani nilikua nafanya sijui hata Kwa lengo lipi.
 
Asee ndugu zangu mnaweza ona nazingua lakini si kweli wakuu, inafika HATUa nashindwa kabisa, nilifikiri ni rahisi sana lakini mambo nayaona tofauti MNO.

nahitAji kushare mawazo na nyie ndugu zangu labda Kwa chochote mana naona naelekea kushindwa.

Payments za kurekodi na video shooting, zilikua sawa sasa changamoto zingine zikaibuka kuangalia mbele mtiti ukaanzia hapo, just imagine sikua na media tour yoyote, influencer yeyote wa kupromote kazi YANGU, yani nilikua nafanya sijui hata Kwa lengo lipi.
Sindikiza na wimbo wako mmoja ili ushauri uendane na kile unachofanya...
 
Ndugu yangu, sidhani kama unazunguka. Unachopitia ni sehemu ya safari ambayo watu wengi huiona baada ya kuanza kuwekeza muda na pesa kwenye kitu wanachokiamini. Kitu muhimu ni usione changamoto za sasa kama ushahidi kwamba umeshindwa. Kwanza jiulize ulianza kwa lengo gani, umefika wapi, na ni kitu gani hasa kinakuzuia kusonga mbele.

Kuhusu kutokuwa na media tour au influencer wa kupromote kazi zako, hiyo nayo ni changamoto lakini si mwisho wa safari. Watu wengi wameanza bila connections kubwa. Kinachotakiwa sasa ni kubadilisha mfumo, usiendelee kutumia pesa kwenye kurekodi na video pekee bila kuwa na mpango wa namna kazi hiyo itawafikia watu na kukuletea matokeo.

Kama unaamini bado hii ndiyo njia yako, kaa chini tengeneza mpango upya: bajeti, malengo, namna ya kupata audience, matangazo, ushirikiano na watu wengine, na muda wa kupima kama mambo yanaenda. Usijione umeshindwa; labda tu ulikuwa unafanya kazi kwa bidii bila ramani ya kutosha. 💪🏾
 
Pole sana. Mi mwenyewe ni msanii wa muziki. Nilianza harakati hizi 2007 nikiwa Form II, nimekaa kidogo Kenya, na mwaka 2014 nilienda studio kwa mara ya Kwanza huko Mbeya City, nikarekodi wimbo unaitwa "Am Very Busy". Baadae 2015 na 2016 nikarekodi "Never" na "No Money" na baadae "So Different". Mwaka 2016 nilifika Radio Free Africa na zilinitoka kama laki mbili hivi kwa ajili tu ya nyimbo zangu kupigwa redioni. Baada ya kutoa hiyo hela ni kweli nilivuma kiasi, jina la kisanii ni JO AFRICA, na hata ukiingia kwenye Music Platforms mbalimbali utanikuta. Wimbo wa AM VERY BUSY ulikuwa ukipigwa kila mara na akina Zuberi Msabaha (RIP) na kuna muda ulishika chati Top 10, mpaka kushika nafasi ya Kwanza kwenye Power Breakfast ya Vodacom enzi hizo, category ya REGGAE.

Kila mara nilipigiwa simu na kuambia wanapiga wimbo wangu, na kweli waliipiga kwa takribani mwaka mzima, na kila mara walihitaji kitu kidogo ili waendelee kuupiga wimbo, na kumbuka sikuwa hata na Video yake. Ilikuwa ni Audio tu. Waliniambia nitoe video ili waniunganishe na Star Tv, na mpaka muda huo nilikuwa nimetumia kama laki sita hivi juu ya wimbo mmoja tu, niliupeleka Bomba FM huko Mbeya, nikaupeleka na Zambia pamoja na Kenya, na nikapata kuperfom kwenye stage mara kadhaa. Nakumbuka mwaka 2015 walikuja akina Mzee Charles Magali kwenye uzinduzi wa Filamu ya Black Valentine, na nikafanya show hapo Mbeya...

Kipindi najipanga kufanya video, mama yangu mzazi akafariki, na baada ya hapo nikaondoka nchini kwenda kuishi Zambia, niliporudi Tanzania nikaingia kwenye mambo ya Sales and Marketing, nikajiunga na DSTv, baadae mwaka 2017 nikapata shule huko Simiyu, nikaingia kwenye Teaching Industry maana nina Degree (Bachelor of Arts with Education) ya English na Literature. Nikasema nifundishe kwa miaka 5 then nirudi kwenye game, Kumbuka muda huo nina mke na mtoto mmoja. 2018 nikampata mtoto wa pili, 2021 mtoto wa tatu, na sasa niko Mwanza hapa na jumla ya watoto wanne, watatu wanasoma English Medium ada nalipa zaidi ya Milioni 4 kwa mwaka. Kazi yangu mwalimu na siko Serikalini, vipi kuhusu mziki?

Ni zaidi ya miaka 8 nafundisha na wanafunzi wangu wamemaliza vyuo vikuu na wako na ajira na wengine wamejiajiri. Nimeandika nyimbo kibao tu, ila tangu 2016 sijawahi kurudi Studio. Nyimbo zangu niliamua kuzitupia Mdundo, Mkito, na nikajiunga na Anti-Joy kwa ajili ya kupromote nyimbo zangu, lakini mpaka leo sijawahi pata pesa kutokana na muziki. Pesa nilizotumia kurekodi na kutangaza ni nyingi kulinganisha na posho za show nilizopiga enzi hizo.

Nimejaribu lakini nimeona na majukumu ya sasa na kuwa na vipaji vingine vimechangia kupotea kimuziki. Licha ya kuwa Mwalimu, mimi pia ni POET, AUTHOR na WEB DEVELOPER. Mara nyingi natumia muda wangu wa ziada kuandika vitabu, mashairi ya kiingereza na kufanya blogging. Niko mtandaoni kama THE MYCROPOST UNIVERSE. Ukitafuta jina hilo Google utaona website yangu.

Sijakata tamaa kuhusu mziki na wala sijachelewa. Na nikushauri tu ndugu yangu, kama una kipaji kingine mbali ma mziki basi kiendeleze, na unaweza pata pesa nyingi huko kuliko hata kukomaa na muziki. Kama hauna familia bado, hauna watoto, unaweza komaa huko, ila hakikisha uko sana na uungwaji mkono na watu wa kwenu, marafiki na uwe na bidhaa hitajika sokoni. Mimi pia nilipata changamoto ya lugha. Nyimbo zangu nimeziandika kwa kiingereza, na niko Tanzania... Na nilikua naimba Reggae. Ila upande wa Ualimu si haba pia, na uandishi wangu unanilipa pia, na napata pesa kutokana na kutengeneza website, na hizi zote ni kipaji na utundu tu wa kucheza na computers. Na kwa sasa kuna Artificial Intelligence, kuna SUNO na kadhalika... Kuandika wimbo mzuri ni kutaka kwako tu... Je, uko tayari kuishi kama msanii?
 
Ushauri Bora sana huu mkuu Kwa kweli nilipiga karenda siku ya KUTAMBULISHA nyimbo lengo nilitaka nijitahidi kwanza walau niweke msingi imara nijaribu kuanda watu kwanza na si kukurupuka
 
unautambulisha kwa kina nani?
Wimbo ni mmoja tu huna mashabiki bado
Ulimwengu umebadilika mkuu...Michael Jackson au Matonya walifanya media tour walitumia hao influencers
Leo tuna tiktok insta JF nk unaweza dharau hapa lkn huwenda hapa ndo ukachipua mwisho tukakuita msanii wa JF ...ndo sisi tupo tiktok insta na fb
ndo sisi sisi tunaangalia Tv na Kuskiliza redio
anzia small step weka wimbo hapa omba kina MshanaJr kina britanica na Makebo wapush hapahapa ndani utaona sio sawa na kulalamika

wewe hata jina lako hapa jukwaani haliakisi sanaa unategemea nini?

utajua mwenyewe ushauri sio sheria
 
Asee mkuu nashukuru sana ushauri wako, ni mzuri lakini napata shida kumshirikisha mshana jr, Britannica nk kama unavo shauri sababu mi naimba nyimbo za ujana zaidi, nakosa Imani kama hao unao wataja watafurahia kazi zangu mkuu
 
hao nliowataja ni msahafu ama biblia kwamba huwezi jiongeza ukawabadili?

The Mountain is You
 
Pole sana. Mi mwenyewe ni msanii wa muziki. Nilianza harakati hizi 2007 nikiwa Form II, nimekaa kidogo Kenya, na mwaka 2014 nilienda studio kwa mara ya Kwanza huko Mbeya City, nikarekodi wimbo unaitwa "Am Very Busy". Baadae 2015 na 2016 nikarekodi "Never" na "No Money" na baadae "So Different". Mwaka 2016 nilifika Radio Free Africa na zilinitoka kama laki mbili hivi kwa ajili tu ya nyimbo zangu kupigwa redioni. Baada ya kutoa hiyo hela ni kweli nilivuma kiasi, jina la kisanii ni JO AFRICA, na hata ukiingia kwenye Music Platforms mbalimbali utanikuta. Wimbo wa AM VERY BUSY ulikuwa ukipigwa kila mara na akina Zuberi Msabaha (RIP) na kuna muda ulishika chati Top 10, mpaka kushika nafasi ya Kwanza kwenye Power Breakfast ya Vodacom enzi hizo, category ya REGGAE.

Kila mara nilipigiwa simu na kuambia wanapiga wimbo wangu, na kweli waliipiga kwa takribani mwaka mzima, na kila mara walihitaji kitu kidogo ili waendelee kuupiga wimbo, na kumbuka sikuwa hata na Video yake. Ilikuwa ni Audio tu. Waliniambia nitoe video ili waniunganishe na Star Tv, na mpaka muda huo nilikuwa nimetumia kama laki sita hivi juu ya wimbo mmoja tu, niliupeleka Bomba FM huko Mbeya, nikaupeleka na Zambia pamoja na Kenya, na nikapata kuperfom kwenye stage mara kadhaa. Nakumbuka mwaka 2015 walikuja akina Mzee Charles Magali kwenye uzinduzi wa Filamu ya Black Valentine, na nikafanya show hapo Mbeya...

Kipindi najipanga kufanya video, mama yangu mzazi akafariki, na baada ya hapo nikaondoka nchini kwenda kuishi Zambia, niliporudi Tanzania nikaingia kwenye mambo ya Sales and Marketing, nikajiunga na DSTv, baadae mwaka 2017 nikapata shule huko Simiyu, nikaingia kwenye Teaching Industry maana nina Degree (Bachelor of Arts with Education) ya English na Literature. Nikasema nifundishe kwa miaka 5 then nirudi kwenye game, Kumbuka muda huo nina mke na mtoto mmoja. 2018 nikampata mtoto wa pili, 2021 mtoto wa tatu, na sasa niko Mwanza hapa na jumla ya watoto wanne, watatu wanasoma English Medium ada nalipa zaidi ya Milioni 4 kwa mwaka. Kazi yangu mwalimu na siko Serikalini, vipi kuhusu mziki?

Ni zaidi ya miaka 8 nafundisha na wanafunzi wangu wamemaliza vyuo vikuu na wako na ajira na wengine wamejiajiri. Nimeandika nyimbo kibao tu, ila tangu 2016 sijawahi kurudi Studio. Nyimbo zangu niliamua kuzitupia Mdundo, Mkito, na nikajiunga na Anti-Joy kwa ajili ya kupromote nyimbo zangu, lakini mpaka leo sijawahi pata pesa kutokana na muziki. Pesa nilizotumia kurekodi na kutangaza ni nyingi kulinganisha na posho za show nilizopiga enzi hizo.

Nimejaribu lakini nimeona na majukumu ya sasa na kuwa na vipaji vingine vimechangia kupotea kimuziki. Licha ya kuwa Mwalimu, mimi pia ni POET, AUTHOR na WEB DEVELOPER. Mara nyingi natumia muda wangu wa ziada kuandika vitabu, mashairi ya kiingereza na kufanya blogging. Niko mtandaoni kama THE MYCROPOST UNIVERSE. Ukitafuta jina hilo Google utaona website yangu.

Sijakata tamaa kuhusu mziki na wala sijachelewa. Na nikushauri tu ndugu yangu, kama una kipaji kingine mbali ma mziki basi kiendeleze, na unaweza pata pesa nyingi huko kuliko hata kukomaa na muziki. Kama hauna familia bado, hauna watoto, unaweza komaa huko, ila hakikisha uko sana na uungwaji mkono na watu wa kwenu, marafiki na uwe na bidhaa hitajika sokoni. Mimi pia nilipata changamoto ya lugha. Nyimbo zangu nimeziandika kwa kiingereza, na niko Tanzania... Na nilikua naimba Reggae. Ila upande wa Ualimu si haba pia, na uandishi wangu unanilipa pia, na napata pesa kutokana na kutengeneza website, na hizi zote ni kipaji na utundu tu wa kucheza na computers. Na kwa sasa kuna Artificial Intelligence, kuna SUNO na kadhalika... Kuandika wimbo mzuri ni kutaka kwako tu... Je, uko tayari kuishi kama msanii?
Dah kaka imebidi nikae chini kwanza noma sana ila hustle zako mkuu, zilikua kiboko kaka na ndo mana mi nimeghaili kuanza sasa badala yake nimepanga kuanza April huo msoto wako ni kiboko binafsi media tour moja tu labda ndio tafanya inshallah ila wadau humu wanahisi nazingua hawajui kile unacho kitoa kwenye MZIKI kinaweza kisirudi
 
Back
Top Bottom