Konki kichaa
Senior Member
- May 18, 2018
- 102
- 74
vikoba watu inabidi wapate elimu ya kutosha ili kujiunga;akili za watu wengi wanawaza kujiunga vikoba kwaajili ya kukopa tu hapo ndo shida pia mkopo wa vikoba hauhitaji uchukue kwaajili ya pesa ya matumiz au starehe vikoba ni kwaajili ya kujiinua binafsi siwez kuacha kucheza vikoba kwa sababu zifuatazo nakopa mala3 ya hisa zangu riba ya mkopo ni ndogo na mwisho kuludisha mkopo miez3 Hua Nina tabia ya kuchukua mkopo vikoba kwaajili ya kuboresha biashara zangu yaani nachukua 1 million baada ya miez mi3 naludisha million moja na elfu50 hapo hiyo elf50 ni faida yangu nitaichukua mwisho wa mwaka baada ya kuvunja vikoba hivyo nikichukua hiyo 1 million baada ya miez mi3 inanipa faida zaidi ya laki 5 kwahyo naludisha pesa yao na riba ya mkopo kisha nabaki na faida zangu nafanya hivyo kila mala na hakuna kikomo cha kukopa Hua nalipa deni na kukopa papo hapo ninavyofanya hivi napata faida zaidi ya mala1 faida ya kwanza biashara zangu haziyumbi yaani mtaji unasimama hauyumbi wakati huo nazalisha faida lkn pia napata faida ninavyokopa mala kwa mala faida hiyo napata mwisho wa mwaka pindi twavunja USHAURI WANGU vikoba husaidia wajasiliamali kuboresha vibiasha vyao na sio watu wasiojishughulisha kutegemea pesa ya mkopo wa vikoba kwaajili ya kulipa pango,ada,kuhonga au starehe ndio mana watu huona vikoba havifai