Mnazi hadi uje kuanza kutoa nazi nyingi ni baada ya kupita miaka kadhaa(siwezi kutaja miaka,kwa sababu inategemea na aina ya mnazi)pamoja na kwamba kuna minazi inaweza kuanza kuzaa ikiwa na miaka 3,lakini inakuwa midogo/umbo dogo kwahiyo haiwezi kubeba nazi nyingi .Ni mpaka iwe mikubwa,yaani iwe na shina kubwa/Nene, na makuti mengi ili uweze kushikilia mzigo wa nazi.Ni sawa na mtoto mdogo anaweza kula kutembea nk lakini hawezi kubeba mzigo mzito lakini mtu mzima anaweza.
Kwahiyo uwe mvumilivu utaanza kuvuna nazi kwa uchache huku unaendelea kukua na kuwa mkubwa,kwa kifupi fanya uwekezaji,usitegemee kupata fedha nyingi ndani ya miaka 4-7,labda baada ya miaka 10.
Nakushauri fanya huo mradi ,utafaidika nao baadaye,pia bei ya nazi Ni 500-600, ukiwa na nazi usipeleke sokoni,ingia nazo mtaani,( kwa Dar na Pwani)sokoni bei ni kuanzia 600 na kuendelea wewe uza 500 fasta unamaliza hata zikiwa nyingi.Kwenye masoko kuna dhuluma zinafanyika watakuambia nazi ndogo,hazijakomaa nk,maneno yatakuwa mengi ili ushushe bei.
Naongea kutokana na uzoefu ,mzee wangu alipanda minazi miaka ya 1989,1990 na 1993,bado anavuna.
Kwa ushauri vijana tuwekeze kwenye kilimo kama cha minazi,korosho,michikichi nk uzeeeni tuishi maisha mazuri,vijana wa wakati huo watuite Freemason utasikia "huyu mzee hafanyi kazi, amestaafu lakini ana pesa nyingi, atakuwa Freemason"
Uzuri wa kilimo cha aina hii hakihitaji usimamizi mkubwa,unafanya kazi zako mjini , weekend unatembelea shamba lako.