Naomba Wakenya Muelewe Hili.

Chamoto

JF-Expert Member
Joined
Dec 7, 2007
Posts
8,577
Reaction score
18,774
Naomba
Hili neno linatatiza sana watu ambao hawaijui tamaduni yetu ya Tanzania.

Unaposikia mtu akisema, "Naomba ulete bia nyingine baridi", haimaanishi kwamba unashurtishwa kusema hivyo, bali ni kuonesha ukarimu. Utamaduni wetu watanzania unasisitiza sana ukarimu, udugu, ubinadamu na umoja.

Hii inatokana na msisitizo wa Baba wa Taifa Mwl. Nyerere, kushikamana na kutanguliza utu badala ya mali au fedha. Mali asili zote za Tanzania (ardhi, mito, mbuga, madini na ukanda wa bahari n.k) vinahodhiwa na Rais wa Jamhuri wa Muungano na sisi ndiyo warithi. Hivyo tunatakiwa kuishi kama ndugu.

Hata kama mtu anapesa nyingi kuliko mwengine bado anategemewa kutanguliza utu wake badala ya pesa zake. Ndiyo maana muhudumu anaombwa aongeze bia badala ya kuamriwa, "leta bia nyingine".

Wakenya wengi huwa wanashangaa sana hili neno na kuliona kana kama ni la kujishusha. Nafikiri hii hutokana na utamaduni wa wakenya kupenda kujikweza, sasa wakiona mtu anajishusha wanashtuka! Kwa Tanzania kujikweza ni mwiko, sio kama hatuwezi lakini jamii haikubali, hatukulelewa hivyo!

kwa hiyo ukisikia hata Mh. Rais anasema, "naomba muache uchochezi" ujue siyo ombi, ni amri. Hivyo basi, usijidanganye kudhani "naomba" ni ulegevu, la hasha; ni njia tuu ya kuwasiliana.
 
Naomba ubaki kimya tu. Punguza pumba.

Jana Prof Kabudi, akiwa anaongea na Wakenya amerudia maneno yale yale niliyoyasema miaka miwili iliyopita kuhusu neno hili la naomba. Alisema, "sisi watanzania tunaposema naomba iko naomba kweli naomba lakini iko naomba ikimaanisha lazima unipe".
 
Jana Prof Kabudi, akiwa anaongea na Wakenya amerudia maneno yale yale niliyoyasema miaka miwili iliyopita kuhusu neno hili la naomba. Alisema, "sisi watanzania tunaposema naomba iko naomba kweli naomba lakini iko naomba ikimaanisha lazima unipe".
Nidunge Konyagi moja na niskuitishe change.
 
Chamoto umekuja na moto leo.
 
Kweli we mbumbumbu sasa kwasababu umeoa tena ndo command tu kwahiyo mkeo ubamwambia kaa hapo nikufanye eee ? Hahahhaha hata hiyo ndoa cjui kama itadumu
Mme pia anaomba mke amtimizie haki ya ndoa? Dah dunia ina mambo.
 
Wai Tusker mbili baridi na usundie yule ngeus ako na haga guarana zile atamada.
Hahaa! 😀 Na ngeus ikiteshateveva na guarana usiombe kama mwere wa kibongo budaboss. Cheza kama wewe mzeiya, mpeleke narieng hadi burungo ishike nare!
 
Hapa Kenya;
Customer: Waiter leta ugali samaki na uharakishe.
Waiter: kabisa Buda Kwanza Leo nakuletea Kama umeme.
Customer: Harakisha wacha maristo za abunuasi.
Waiter: Kwenda uko najua Leo uko na kakitu ndio maana unapan'ang'a hivo( both laugh in unison).
Hiyo ndi style ya Kenya and doesn't mean we are rude but we are just being real in a funny and honest way.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…