Chamoto
JF-Expert Member
- Dec 7, 2007
- 8,577
- 18,774
Naomba
Hili neno linatatiza sana watu ambao hawaijui tamaduni yetu ya Tanzania.
Unaposikia mtu akisema, "Naomba ulete bia nyingine baridi", haimaanishi kwamba unashurtishwa kusema hivyo, bali ni kuonesha ukarimu. Utamaduni wetu watanzania unasisitiza sana ukarimu, udugu, ubinadamu na umoja.
Hii inatokana na msisitizo wa Baba wa Taifa Mwl. Nyerere, kushikamana na kutanguliza utu badala ya mali au fedha. Mali asili zote za Tanzania (ardhi, mito, mbuga, madini na ukanda wa bahari n.k) vinahodhiwa na Rais wa Jamhuri wa Muungano na sisi ndiyo warithi. Hivyo tunatakiwa kuishi kama ndugu.
Hata kama mtu anapesa nyingi kuliko mwengine bado anategemewa kutanguliza utu wake badala ya pesa zake. Ndiyo maana muhudumu anaombwa aongeze bia badala ya kuamriwa, "leta bia nyingine".
Wakenya wengi huwa wanashangaa sana hili neno na kuliona kana kama ni la kujishusha. Nafikiri hii hutokana na utamaduni wa wakenya kupenda kujikweza, sasa wakiona mtu anajishusha wanashtuka! Kwa Tanzania kujikweza ni mwiko, sio kama hatuwezi lakini jamii haikubali, hatukulelewa hivyo!
kwa hiyo ukisikia hata Mh. Rais anasema, "naomba muache uchochezi" ujue siyo ombi, ni amri. Hivyo basi, usijidanganye kudhani "naomba" ni ulegevu, la hasha; ni njia tuu ya kuwasiliana.