Mkuu, kazi nyingi zisizohitaji elimu ni za kutumia nguvu. Kwa matatizo yako ni ngumu kufanya kazi hizi.
Naweza kukushauri jichange wewe na ndugu zako ipatikane angalau laki 5.
Nenda kachukue short course ya computer ya mwezi mmoja, ujue basics za computer tu. Mara nyingi course ya mwezi au miezi miwili haizidi 150k
Tafuta computer used ya 200k na tafuta sehem iliyochangamka kidogo hapo mtaani kwako, omba sehem kidogo ya baraza ya kuweka meza na computer yako.
Weka bundle la kutosha, pakua nyimbo za bongo flava na gospel za kutosha. Pita kwa wale maDJ wa movies, kusanya movies za kutosha. Baada ya hapo, hapo kibarazani weka bango la kuuza miziki na movies, huwezi kosa hela ya kula na kuishi kwa siku.