nimekula hela ya kula
Member
- Nov 10, 2024
- 8
- 31
- Thread starter
- #41
Uti wa mgongo ndiyo maisha mkuu, katika umri wa miaka 27 nimepata tatizo kubwa kama hili.Kauli ya maisha yaliyobaki ni kauli ya kukata tamaa,mkuu kamwe usikate tamaa na kumbuka anaejua hatma ya maisha yetu ni Mungu pekee,.
Nadhani daktari au mtu mwenye hili tatizo pekee ndiyo anaweza kusimulia maumivu yake.
Ingekuwa ni labda tuseme nimepata ukimwi ningeenda hospital nianze kutumia ARVs.
Lakini hili tatizo mimi nimekuwa mtu wa maumivu kila dakika 24 hours.
Ukijaribu kugusa matibabu yake ni kufanyiwa upasuaji wa mgongo na gharama zake hazikamatiki, na hata ukifanyiwa huo Upasuaji bado masharti ya kutofanya kazi ngumu yako pale pale na huenda yakawa masharti makali zaidi.
Sasa haya ni maisha gani?
Nina umuhimu gani mpaka sasa?
Ningekuwa nimesoma ningeomba kazi ya taaluma yangu, ningekuwa na ndugu wenye uwezo ningeomba wanisaidie chochote kitu walau nianzishe hata mradi wa ufugaji ili nikizi mahitaji yangu.
Nina mengi ya kuandika mpaka sasa lakini mpaka hapa mtu mwenye uwezo wa kunisaidia hata kibarua cha kufanya kulingana na afya yangu basi anisaidie, hata ikiwa kusafisha vyoo, kufanya kazi za usafi n.k