Naombeni kibarua cha kusogeza siku za maisha yangu yaliyobaki hapa duniani

Kauli ya maisha yaliyobaki ni kauli ya kukata tamaa,mkuu kamwe usikate tamaa na kumbuka anaejua hatma ya maisha yetu ni Mungu pekee,.
Uti wa mgongo ndiyo maisha mkuu, katika umri wa miaka 27 nimepata tatizo kubwa kama hili.
Nadhani daktari au mtu mwenye hili tatizo pekee ndiyo anaweza kusimulia maumivu yake.
Ingekuwa ni labda tuseme nimepata ukimwi ningeenda hospital nianze kutumia ARVs.
Lakini hili tatizo mimi nimekuwa mtu wa maumivu kila dakika 24 hours.
Ukijaribu kugusa matibabu yake ni kufanyiwa upasuaji wa mgongo na gharama zake hazikamatiki, na hata ukifanyiwa huo Upasuaji bado masharti ya kutofanya kazi ngumu yako pale pale na huenda yakawa masharti makali zaidi.
Sasa haya ni maisha gani?

Nina umuhimu gani mpaka sasa?
Ningekuwa nimesoma ningeomba kazi ya taaluma yangu, ningekuwa na ndugu wenye uwezo ningeomba wanisaidie chochote kitu walau nianzishe hata mradi wa ufugaji ili nikizi mahitaji yangu.
Nina mengi ya kuandika mpaka sasa lakini mpaka hapa mtu mwenye uwezo wa kunisaidia hata kibarua cha kufanya kulingana na afya yangu basi anisaidie, hata ikiwa kusafisha vyoo, kufanya kazi za usafi n.k
 
Ya ulinzi utaweza?
 
Mkuu samahani kidogo unaposema hujasoma ina maana hujawahi kuingia darasani kabisa au ni nini maana yako?

Una uandishi mzuri ambao haushawishi kuwa haujasoma. Kama una elimu sema kiwango cha elimu yako na sio kusema haujasoma. Unaweza kukosa msaada kwa kuleta mashaka madogo madogo kama haya.

Sema kiwango cha elimu yako achana na habari za haujasoma na kutia huruma ukidhani ndio utasaidika Mkuu.
 
Duuuu miaka 27 umekata tamaa ndugu
Omba ushaur wa afya yako mkuu kuliko kukata tamaa kumbuka kwa umri wako taifa linakutegemea wew ndio nguvu kaz
 
Mkuu situation unayopitia naielewa ila jua majobless tupo wengi sio wewe tuu Sema tofauti sisi ni wazima wa afya, ila usikate tamaa mzee baba. Nikushauri kwa tatizo ulionalo jaribu kupita kwenye hizi media kama upo dar nenda clouds fm mtafute doctor issack Malo Hua anakipindi sijui kinaitwaje ila hua kinadeal na watu wenye matatizo nenda na makaratasi yote kuhusu ugonjwa wako huwezi jua kupitia kipindi hivyo unaweza kupata msaada wa kimatibabu kutoka kwa wasikilizaji pia usisahau tunaelekea kwenye uchaguzi FISIEM wanataka kura so pindi unajieleza muombe na mama SAMIA msaada huwezi jua kupitia chawa zake wanaweza kumfikishia taarifa ukasaidiwa mkuu. Ni mawazo yangu hayo.
 
Njoo KKKT KImara
kuna vijibarua si haba
 
Nimependa avatari Yako mkuu
 
Ukisoma comment ya 6 utagundua huyu ana kiwango Fulani cha elimu ila anshindwa kuweka wazi unaonekana huyu ana taaluma Fulani ila hajagraduate huenda ndo maana anshindwa kuweka wazi
 
Maisha ni safari na hata mbuyu ulianza kama mchicha hatuwezi fanana maisha huyo graduate muomba hela ya kula n kuishi leo kesho hatokua hivo tena.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…