naombeni kueleweshwa kisheria juu ya hili

leirilwa

Senior Member
Joined
Sep 18, 2015
Posts
118
Reaction score
22
nina miaka miwili kazini sijawahi kuutumia mshahara wangu kwa matumizi yangu binafsi zaidi ya mwanaume kuupigia bajet na sometimes kuwatumia ndugu zake wanasheria wa jf naomben mnisaidie mwanaume ana haki yoyote juu ya mshahara wangu? Na wajibu wa kutunza familia ni mke au mme?
 
sheria ya ndoa haijaandika bt mahakaman huangalia makubaliano yenu na sikingine. sas km han kaz kwqn kuudumia kuna ubaya best
 
Ninavyo mimi tatizo lako ni la kifamilia, unahitaji kuzungumza na mumeo juu ya hilo uone response yake kabla hujachukua hatua zaidi. Ingawa kuna vitu vya kuangalia pia au ungetujuza ili hata huyo mwanasheria akija alielewe hili kwa upana naaa kukupa ushauri muafaka. Mumeo kama hana kazi pengine, au anayo ila kipato kidogo kulinganisha na chako au anacho cha kutosha sawa na wewe au hata kukuzidi ila tu ndo anafanya hivyo. Labda ungelielezea zaidi mpendwa
 
Uliolewa na handsome eeeh? Kazi hana huyo.

Kwa mujibu wa Mtume Paulo, mumeo anayo mamlaka juu ya mwili wako, lakini si juu ya talanta. Ila kwa kukusaidia, kaa naye chini muende sawa. Baba ndio kiongozi wa nyumba, YES anayo haki na mamlaka ya kuratibu kila senti na kila hali ndani mwenu, lakini JE, ni mtu mwenye haki?

Vunja ukimya, zungumzeni. Sheria inaweza ikakudisappoint usiamini kama ilitungwa na watu wenye akili timamu
 
hahaha sas kwanin asiamin bt pia mumeo hn kitu so utamuacha kisa han hela ya kukulisha
 
Mumeo ni Mario? Mi navyojua mume lazima ajue wajibu wake katika familia. Ila sasa kama uliolewa na mwanaume suruali unategemea nini?
 
Ninavyo mimi tatizo lako ni la kifamilia, unahitaji kuzungumza na mumeo juu ya hilo uone response yake kabla hujachukua hatua zaidi. Ingawa kuna vitu vya kuangalia pia au ungetujuza ili hata huyo mwanasheria akija alielewe hili kwa upana naaa kukupa ushauri muafaka. Mumeo kama hana kazi pengine, au anayo ila kipato kidogo kulinganisha na chako au anacho cha kutosha sawa na wewe au hata kukuzidi ila tu ndo anafanya hivyo. Labda ungelielezea zaidi mpendwa
mme wangu ana kazi na kipato chake ni kikubwa kuliko changu ni anataka tu kucontrol na nikilalamika juu ya mshahara wangu ni ugomvi unaanza
 
Ukipata mshahara af ukakaa nao usipeleke kwake inakuaje?
 
Mwanaume ndiyo kichwa cha familia. Ila siyo wanaume wote wamepewa uwezo. Kama ulamua awe mume wako wa hali na mali, wa kufa na kuzikana. Kuvumilia tu.
 
Kuna screw zimeloose.huyo sio bure. Mmewahi kulizungumzia hili kifamilia? kama kuwaelezea wazazi wake au wako?
 
Kama sheria inasema mkiachana mnagawana sawa na akifa we na watoto ndo warithi wa mali za marehemu, tatizo likowapi akitumia mshahara wako as long as sio kwa starehe.
 
Mimi nipo tayari kutoa msaada bure kabisa japo kwa sasa huna kesi leirilwa. Ukitaka kesi mnyime hela hadi afungue yeye hiyo kesi halafu uniite. Bure!!
 
Last edited by a moderator:
Kuna screw zimeloose.huyo sio bure. Mmewahi kulizungumzia hili kifamilia? kama kuwaelezea wazazi wake au wako?
tulishawahi kuvutana mpaka tukapeleka kwa wazazi wake but wazazi hawakuonesha kunisapoti na kinachoniuma zaidi ni kwamba ndugu yangu akiwa na shida hakubali kumsaidia lkn ndugu yake akiwa na shida anamtumia hela
 
Okay, kama utaona inafaa fanya hivi.. usimpe mshahara wako kuanzia sasa hata aanzishe ugomvi simamia haki yako, kazi unafanya wewe, pesa ni yako isipokua mwenyewe utake kuitoa kwa hiyari kwa matumizi ya kifamilia. Akikupiga au kukutukana ndio ukamfungulie mashtaka sasa, kosa sio kuchukua mshahara ila liwe udhalilishaji ikitokea amekupiga au kukutukana. Hapo sasa ndo unamtafuta kaka hapo juu aliyeoffer kukusaidia.
 
asante kwa mawazo
 
Samahani....
Ila wewe ni kiazi haswa....

Mshahara ni haki yako...
Matumizi ni majadiliano kati yako na mumeo...

Wewe huna ndugu wanaohitaji msaada ukawasaidia kwa huo mshahara???

Kwa kuanzia....fungua akaunti benki nyingine...mshahara upitie huko kaa na password kichwani karatasi tupa
 
tulishawahi kuvutana mpaka tukapeleka kwa wazazi wake but wazazi hawakuonesha kunisapoti na kinachoniuma zaidi ni kwamba ndugu yangu akiwa na shida hakubali kumsaidia lkn ndugu yake akiwa na shida anamtumia hela

Uzembe wako mwenyewe
Ukimkatalia atakupokonya????
Ulidhani wazazi wake watakutetea???
 
Back
Top Bottom