Napenda dagaa wa Mwanza ila wale wasio na michanga wanakua na vimajani kidogo
1. Pasha maji yawe ya vuguvugu kwa ajili ya kuoshea dagaa, osha mpk wawe wasafi
2. Km mpenzi wa tangawizi na limao, kwangua tangawizi changanya na dagaa kamulia na kimao
3. Andaa carrot, nyanya za kutosha, kitunguu na hoho
4. Weka mafuta jikoni yapate moto, weka kitunguu kikikaribia kuiva weka dagaa wakaaange vizuri wawe wanaelekea kukauka halafu weka nyanya na carrot
5. Zikikaribia kuiva weka hoho, acha zichemke mpk nyanya ziive (ile shombo ya nyanya mbichi iishe kabisa)
NB. Dagaa inataka nyanya na mafuta ya kutosha ya kukaangia
Sent from my CPH2015 using
JamiiForums mobile app