Pre GE2025 Naombeni kujulishwa kifungu kinachomruhusu Rais Samia kugombea Urais 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Siyo lazima iwe miaka 10, maana inahesabiwa pamoja na ile aliyotumia Magu kwenye kipindi cha pili. Tatizo huwa mnasoma katiba vipande vipande hamtaki kufuata maelekezo. Soma hicho kipande na ukasome ibara zote zilizoelekezwa hapo!
 
Kwa wana CCM wenyewe, wanasema ni utamaduni wao.
Wenyewe hawazingatii katiba yao,wanachoangalia ni utamaduni wao unasemaje
 
Tatizo la mitanzania ni mivivu ya kusoma. Wala hilo siyo swali la kusumbua watu hapa JF!
 
Abdu Hana cheo chochote kwa ninavyojua.
Huwa kuna First Lady na pia kuna First Gentlemen labda kipo na kipengele kingine kinachojumlisha na First Son 😂😂😅 !
Mavyeo vyeo ya wakubwa yapo mengi 😀🤣😀
Msinipopoe mawe nimesema Labda !
Maana yake sina uhakika !!
 
Endapo Makamu wa Rais anashika kiti cha Rais kwa mujibu wa masharti ya ibara ya 37 (5) kwa kipindi kinachopungua miaka mitatu ataruhusiwa kugombea nafasi ya Rais mara mbili, lakini kama akishika kiti cha Rais kwa muda wa miaka mitatu au zaidi ataruhusiwa kugombea nafasi ya Rais mara moja tu.
 

Attachments

  • IMG_3238.jpeg
    289.9 KB · Views: 2
Hii ni black and white haina chenga chenga !
Imeeleweka vizuri sana !
 
Ungefanya la maana zaidi ungeonesha kifungu kishomruhusu.
 
Na wewe usidanganye watu inayosema kipindi cha kushika madaraka siyo ibara ya 37(5) bali ni Ibara ya 40(5).
 
Andika vizuri hiyo hoja yako kwa kuweka vizuri hivyo vifungu! Umekurupuka kana hujasoma! Kwa uandishi huo chuo hutoboi!
Umekurupuka iko kifungu kinapatikana kwenye ibara ya 40 ikiilezea ibara ya 37..
Ungeacha kukurupuka ungejua kimetokea wapi no need doubts na kujichoresha..
 
Ibara ya 40 (4)
 
Miaka 5 tu siyo 10.
Ukomo ni vipindi 2 vya miaka mitano mitano
Sawa, ila ikifika 2030 Bimkubwa itakuwa hajatimiza miaka 10 ya urais wake, utata bado upo pale pale!! Inatakiwa ikifika 2030 aongezewe muda itimie miaka kumi. Unless otherwise katiba ifanyiwe marekebisho!
 
Sawa ila atajua hajui
 
🤣🤣🤣
 
Sawa, ila ikifika 2030 Bimkubwa itakuwa hajatimiza miaka 10 ya urais wake, utata bado upo pale pale!! Inatakiwa ikifika 2030 aongezewe muda itimie miaka kumi. Unless otherwise katiba ifanyiwe marekebisho!
Uko sahihi. Katiba haijaweka ukomo kwa anayerithi uongozi baada ya kufariki,kuijiuzulu,nk
Itaje ukomo wa mrithi.
Kama imetaja basi ni vizuri.
 
Chuki tu zinakusumbua kijana! ... kama na wewe una kadi ya chama nenda kagombee au wamekukataza?

Mama bado yupo saanaaaa! ... meza hiyo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…