Jibu la swali lako lipo kwenye Katiba ya Tanzania.
* Ibara ya 37 (5) ya Katiba ya JMT inaeleza kwamba endapo Rais atafariki, Makamu wa Rais ataapishwa kuwa Rais ili kuendeleza na kukamilisha awamu ya miaka mitano ya huyo aliyefariki.
* Ibara ya 40 (4) ya Katiba ya JMT inaeleza kuhusu 'Haki ya kuchaguliwa tena' huyo Rais aliyerithi urais, kwamba:
🔷 Endapo amerithi huo urais kwa kipindi kinachopungua miaka mitatu (kabla ya uchaguzi mkuu wa Rais), basi mrithi huyo ataruhusiwa kugombea Urais kwa AWAMU MBILI zijazo za Uchaguzi Mkuu.
🔷 Endapo amerithi huo urais kwa muda wa miaka mitatu au zaidi (kabla ya uchaguzi mkuu wa Rais), basi mrithi huyo ataruhusiwa kugombea Urais kwa AWAMU MOJA tu ijayo ya Uchaguzi Mkuu.
For the case of Rais Samia, alirithi Urais mwaka 2021, ambapo ni miaka MINNE kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2025. As such, pursuant to the Katiba ya sasa ya JMT, na endapo Chama chake CCM kitampitisha, Mh Rais Samia anaruhusiwa kugombea nafasi ya Urais MARA MOJA tu uchaguzi ujao 2025. Hivyo, uchaguzi mkuu wa 2030 Rais Samia haruhusiwi kugombea tena, unless Katiba ifanyiwe mabadiliko.
Reference: KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.
✅ Ibara ya 37 (5)
View attachment 3073468
✅ Ibara ya 40 (4)
View attachment 3073472
-Kaveli-