Naombeni majibu ya maneno haya

Naombeni majibu ya maneno haya

TAI DUME

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2014
Posts
9,748
Reaction score
26,238
1. Haki ya nani
Watu wamekuwa wakiapiza Sana kutumia haya maneno. Nimezoea sana kusikia watu wakiapiza kwa maneno ya yanayohusisha Mungu mfano " haki ya Mungu naapa, Maasafu ya Mtume, Yesu Kristu naapa, nk". Sasa hii kuapa kwa maneno "haki ya nani/nane" source yake ni Nini?

2. Ukistaajabu ya Musa utayaona ya firauni

Kikubwa Musa alichofanya ni Nini na kikubwa alichofanya firauni ni Nini? Angalizo: Watu wengi hapa wanahusisha jina firauni na vitendo vya ufiraji, si kweli, firauni ni cheo Cha pharaoh ambacho kwa kiswahili kisicho rasmi NI firauni na walikuwa wengi tu kwa nyakati tofauti. Niambieni Sasa kikubwa walichofanya mafarao Hawa ni Nini mpaka tuyastaajabie.

3. Utakiona cha mtema kuni
Hapa napo pananipa shida. Huyo mtema kuni ni Nani na kutema kuni ni kufanyaje. Na kipi kikubwa kilichompata mpaka mtu akitaka kukupiga mikwara akutishie masaibu yaliyomkuta huyo bwana aliyetemeshwa kuni.

Tafadhali waungwana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cha mtema kuni ni shoka,
ukiwa mwizi lazima ukipate cha mtema kuni.
Firauni waislamu wanamjua vyema.
 
Firauni aliita wachawi wote wa Misri kumsaidia kuwafunga wana wa Israel wasiondoke. Musa kwa uwezo wa Mungu aliweza kuigawa bahari na wana wa Israel wakapita salama.
 
Firauni aliita wachawi wote wa Misri kumsaidia kuwafunga wana wa Israel wasiondoke. Musa kwa uwezo wa Mungu aliweza kuigawa bahari na wana wa Israel wakapita salama.
Hill la Musa kweli lilikuwa kubwa. Lakini la firauni bado sijaona ukubwa wake
 
Back
Top Bottom