Naombeni mawazo yenu kuhusu hii ramani ya nyumba yangu

Naombeni mawazo yenu kuhusu hii ramani ya nyumba yangu

Amanitwin

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2011
Posts
1,372
Reaction score
1,628
Wakuu mambo vipi.
Nina ramani ambayo nimeandaa kwa ajili ya kujenga nyumba ya vyumba vitatu.(1 master bedroom + 2 normal rooms).
Nyumba itapauliwa kwa mtindo wa Hidden Roof a.k.a contemporary

Naombeni mawazo yenu juu ya hii ramani.

  • Nini cha kuboresha?
  • Nini kimekosewa/hakijakaa sawa?
  • Nini cha kurekebisha?
  • Nini niondoe/nipunguze?

Nimeambatanisha hapa chini ramani yenyewe.

Screenshot_20230218-181050_Adobe Acrobat.jpg
 
Wakuu mambo vipi.
Nina ramani ambayo nimeandaa kwa ajili ya kujenga nyumba ya vyumba vitatu.(1 master bedroom + 2 normal rooms).
Nyumba itapauliwa kwa mtindo wa Hidden Roof a.k.a contemporary

Naombeni mawazo yenu juu ya hii ramani.

  • Nini cha kuboresha?
  • Nini kimekosewa/hakijakaa sawa?
  • Nini cha kurekebisha?
  • Nini niondoe/nipunguze?

Nimeambatanisha hapa chini ramani yenyewe.

View attachment 2521843
Jitahidi na chumba kingine (tunapenda kukiita chumba cha watoto wa kike) kiwe self contained. Watoto wa kike kujichanganya na choo cha public ni shida kidogo.
 
..Kwa nini master bedroom inakaa uwani? Yaani watoto wakae mbele wewe mwenye nyumba ujifiche uwani! Fanya uwezavyo chumba chako kikae mbele uwe na uwezo wa kuona chochote kinachotokea eneo la mbele la nyumba ikiwezekana uone na gate kubwa la mbele.
 
Nimekupata mkuu point yako, it makes a lot of sense... Ingawa watu wengine huwa wanasema chumba cha wazazi kijifiche.... so nikaona nikifiche hapo kwa nyuma kwa staili hiyo.
 
Kutoka sebuleni hadi ufike chumbani kama umeshiba msosi wote unaishia njiani kwa safari hiyo..
Mkuu, nashukuru kwa mchango wako.
Nataka sebule ikae hapohapo ilipo.... nafikiri nikipunguza urefu wa hiyo corridor(kwa kuondoa huo ukuta wa koridor unaotenganisha dining, foyer na ofisi) labda itasaidia
 
Na hizo Kona Kona zilivyonyingi ukiwa umekunywa vitu vyetu si tutajikuta umejigonga ukutani au kupotea ndani ya nyumba yako.
 
Bedroom 1 (iliyo karibu na bedroom 2) inaweza ikawa master pia kama tu ukiifanya ifuatane sambamba na hicho chumba kingine kilichoitwa bedroom 1 pia...

Then huo muendelezo wa korido unautumia kuweka WC...
 
Huwa natamani kabla sijaanza ujenzi wa nyumba yangu ningekuwa na hii akili ya kuuliza watu kama hivi,siyo kwamba ni mbaya ila nikisoma soma nyuzi kama hizi huwa natamani kwanini kitu fulani nisingekiweka namna fulani au nisingekiweka kabisa.

By the way,aliyetangulia ametangulia (kujifariji tu kumbe nifanyeje)
 
  • Nini cha kuboresha?
Boresha washroom ya masters choo kikae kama ile public toilet kikae kuegemea ukuta wa nje
  • Nini kimekosewa/hakijakaa sawa?
Hakijakosewa wala sio hakijakaa sawa but it's more convenient
  • Nini cha kurekebisha?
Ukiweza kupunguza ukubwa wa vyumba vingine, nyumba za kisasa kila chumba ni self!.
  • Nini niondoe/nipunguze?
Kama the house is too small, kuliko kuwa na home office, fanyia kazi zako dining uongeze self.
P
 
Kwamba aongeze room nyingine? Ziwe jumla 4 badala ya 3
 
Hongera sana mkuu. Mimi naweza kusema haya kwanza:
1. Storage. Vyumbani weka au onyesha makabati ya nguo yatakuwa wapi. Kama watoto wakiwa wakubwa wataweza kusoma chumbani? Je wataweza kuwa na meza za kusomea na kufanyia hobbies zao kama coding na nyinginezo?

2. Sink za kuosha mikono. Sidhani kama unahitaji sink nje ya public bathroom kama ndani ipo pia.

3. Public bathroom ni nyembamba sana na siyo sawa sana kuwa na shower katikati ya sink na choo, yaani mtu anavuka maji kufika chooni. Ukienda haja baada ya mtu aliyetoka kuoga na umevaa soksi....

4. Kama utaratibu uko vizuri, laundry na store vichanganye viwe chumba kimoja kiwe scullery ama Butler's pantry with laundry.

5. Nadhani ulitaka mlango wa chumbani usionekane kutoka sebuleni, ila mtu kuingia office anapitia dining... Nadhani mtu aingie ofisini kupitia foyer maana unaweza pata mgeni wa kikazi ambaye unaweza kumalizana naye ofisini kabla hajafika maeneo mengine ya nyumba.

Hivyo mimi ningeua ukuta wa dining wa corridor ili dining iongezeke na kuhamisha mlango office uwe upande wa foyer. Ulitaka unaweza kuweka mlango wenye frosted glass kati ya bedroom/office/ washroom kutenga maeneo ya vyumbani na maeneo ya sebuleni
 
Wakuu mambo vipi.
Nina ramani ambayo nimeandaa kwa ajili ya kujenga nyumba ya vyumba vitatu.(1 master bedroom + 2 normal rooms).
Nyumba itapauliwa kwa mtindo wa Hidden Roof a.k.a contemporary

Naombeni mawazo yenu juu ya hii ramani.

  • Nini cha kuboresha?
  • Nini kimekosewa/hakijakaa sawa?
  • Nini cha kurekebisha?
  • Nini niondoe/nipunguze?

Nimeambatanisha hapa chini ramani yenyewe.

View attachment 2521843
Tafuta ramani nyingine ambayo chumba chako kitakuwa mashariki, chumba cha watoto wa kiume mashariki, halafu cha watoto wa kike kusini.

Haiwezekani ujenge nyumba halafu vyumba vyote viko upande mmoja. Mtajikuta muda wote mnaongea na kufanya mambo yenu bila ya uhuru.
 
Bedroom 1 (iliyo karibu na bedroom 2) inaweza ikawa master pia kama tu ukiifanya ifuatane sambamba na hicho chumba kingine kilichoitwa bedroom 1 pia...

Then huo muendelezo wa korido unautumia kuweka WC...
Asante mkuu, naona hapa nimepokea sana ushauri wa kuiondoa master nyuma na kuiweka mbele... na wewe umekazia hilo.

Nalichukua, nitalitekeleza
 
Back
Top Bottom