Naombeni mawazo yenu kuhusu hii ramani ya nyumba yangu

Naombeni mawazo yenu kuhusu hii ramani ya nyumba yangu

Wakuu mambo vipi.
Nina ramani ambayo nimeandaa kwa ajili ya kujenga nyumba ya vyumba vitatu.(1 master bedroom + 2 normal rooms).
Nyumba itapauliwa kwa mtindo wa Hidden Roof a.k.a contemporary

Naombeni mawazo yenu juu ya hii ramani.

  • Nini cha kuboresha?
  • Nini kimekosewa/hakijakaa sawa?
  • Nini cha kurekebisha?
  • Nini niondoe/nipunguze?

Nimeambatanisha hapa chini ramani yenyewe.

View attachment 2521843
Hakikisha master bedroom haikai jirani na vyumba vingine vya kulala
Utakuja kunishukuru baadae

Masta ikae kona nyingine huko for privacy purpose kama vile simu, ugomvi mdogo mdogo na yale mambo
Otherwise uweke milango ambayo haitaruhusu sauti kupenya
 
Wakuu mambo vipi.
Nina ramani ambayo nimeandaa kwa ajili ya kujenga nyumba ya vyumba vitatu.(1 master bedroom + 2 normal rooms).
Nyumba itapauliwa kwa mtindo wa Hidden Roof a.k.a contemporary

Naombeni mawazo yenu juu ya hii ramani.

  • Nini cha kuboresha?
  • Nini kimekosewa/hakijakaa sawa?
  • Nini cha kurekebisha?
  • Nini niondoe/nipunguze?

Nimeambatanisha hapa chini ramani yenyewe.

View attachment 2521843
Store na laundry vihamie mahali ilipo dining na dining ichukue nafasi ya store na laundry
 
Boresha washroom ya masters choo kikae kama ile public toilet kikae kuegemea ukuta wa nje

Hakijakosewa wala sio hakijakaa sawa but it's more convenient

Ukiweza kupunguza ukubwa wa vyumba vingine, nyumba za kisasa kila chumba ni self!.

Kama the house is too small, kuliko kuwa na home office, fanyia kazi zako dining uongeze self.
P
Mkuu P, Kuhusu sink la choo cha master, uko sahihi.. nitaliweka kwenye hiyo position uliyoshauri.

Kuhusu kila chumba kuwa self ni wazo zuri sana... Ila hii ni nyumba ya kuanzia maisha, ( Mungu akinijalia uwezo na uhai nimepanga kujenga nyingine huko miaka ya mbeleni), hivyo nilifikiri niifanye simple.

Asante sana kwa inputs mzee baba
 
Kwanza sijajua ukubwa wa kiwanja chako ili kushauri dimension za vyumba.
3x3 ni tu vyumba tudogo sana atlist 4x4 na master walau 5x6 pia umeweka kuta nyingi ambazo zinakaba space mfano kweny entrace kushoto huo ukuta unakaba space ya sebule... hata hiyo uliyoita ofisi ni kadogo mno 2x2.8m ni kama choo? Iliyochangamka. Kingine vyumba vinavyo share public toilet vinakuwa mbali na toilet yenyewe, pia master iwe mbali kidogo na vyumba vya watoto.

Then angalia pia budget na uharaka wako wa kuwa na nyumba uamue kwa usahihi.
 
Hiyo raman haijazingatia faragha za master bedroom, haijazingatia matumiz sahihi ya ardhi hata kama una eneo kubwa ramani upana tu sio chini ya mita 14 urefu mita 12, ramani itaku cost si chini ya matofali 4,000 wakat hayo matofali ungepata raman nzuri yenye hivyo vitu na ungeongeza chumba cha 4. Inshort raman itakugharimu pesa nyingi kama unajenga kwa pesa za vikoba
 
Wakuu mambo vipi.
Nina ramani ambayo nimeandaa kwa ajili ya kujenga nyumba ya vyumba vitatu.(1 master bedroom + 2 normal rooms).
Nyumba itapauliwa kwa mtindo wa Hidden Roof a.k.a contemporary

Naombeni mawazo yenu juu ya hii ramani.

  • Nini cha kuboresha?
  • Nini kimekosewa/hakijakaa sawa?
  • Nini cha kurekebisha?
  • Nini niondoe/nipunguze?

Nimeambatanisha hapa chini ramani yenyewe.

View attachment 2521843
Mkuu mbona umeniwekea hapa ili niikwapue?😜 Just kidding, fuata ushauri wa wataalamu hapo juu
 
Asante mkuu, naona hapa nimepokea sana ushauri wa kuiondoa master nyuma na kuiweka mbele... na wewe umekazia hilo.

Nalichukua, nitalitekeleza

Wazo langu lilikuwa ni kuongeza master ya pili bila kutumia nafasi kubwa....

Sio kuhamisha iliyopo, nisome vizuri...
 
japo sina ujuzi sana wa hii kitu ila hapo kwenye hidden roof nakushauri tafuta mtaalamu hasa maana wengi kutokana na mafundi wasio na weledi kuwapaulia isivyo sahihi, wamejikuta katika vilio visivyo na kikomo
 
Hakikisha master bedroom haikai jirani na vyumba vingine vya kulala
Utakuja kunishukuru baadae

Masta ikae kona nyingine huko for privacy purpose kama vile simu, ugomvi mdogo mdogo na yale mambo
Otherwise uweke milango ambayo haitaruhusu sauti kupenya
Labda ataweka soundproof 🤣🤣🤣
 
1. Hii kitu inaitwa "foyer" imenikera!! sijui ni ushamba?. Ondoa huo ukuta kati ya sebule na hiyo foyer sebule iwe kubwa na iwe wazi (utakuja kunishukuru). Sebule ndio maana inaitwa "living room" inatakiwa iwe kubwa isibanwe banwe, pia kuta zinaleta giza tu ndani unakuta nyumba saa nane mchana mmewasha taa!!. Hata hiyo foyer itakuwa na giza ni busara kuondoa huo ukuta.
2. Hivi vitu vinaitwa "office" au "study room" pale kwangu zimeishia kuwa store[emoji23][emoji23] Tumeweka makorokoro kibao hata hakuingiliki. Wageni wakija tunaongelea sebuleni kama kuna issue itahitaji documentation au kufanya kazi kwenye laptop kuna meza simple ya juu iko hapo pembeni sebuleni tunahamia hapo tunamalizana (otherwise sijui nature ya shughuli zako kama ni 24/7 unafanyia home).
Watoto wanasomea kule chumbani kwao kuna vimeza vidogo vya kusomea. Ni ngumu kumuhamisha mtoto akasomee "study room" kwanza wanaogopa kukaa huko peke yao hawajapazoea.
 
Back
Top Bottom