Naombeni mawazo yenu kuhusu hii ramani ya nyumba yangu

Kuongeza ukubwa wa chochote ni kuongeza maradufu gharama ya ujenzi. Hata kama ungekuwa na kiwanja cha 400sqm kama budget yako haitoshi huwezi kufanya kitu. Ungeuliza kwanza kama mhusika ana "unlimites budget" ndio utoe ushauri wako huo.

Jamaa yangu tulianza nae ujenzi mwaka 2016 yeye akajenga mjengo mkubwa balaa (hiyo veranda mzunguko wake pekee ni hatari na inatakiwa kumiminwa) mimi nikajenga simple/standard family house, mwaka 2017 nikahamia kwangu. Yeye mpaka leo lile jumba lake halijaisha (tunakaribia kuliita gofu/pagale) na bado amepanga mpaka leo.
Still your in assumption cause from the start hajagusia budget ameongelea ramani so we were free to put our suggestion from our exprience. Kama ushauri wako ulijali budget fine mpe huo. Wengine tulibase on essentials in moden house. Kama una uharaka wa kuishi kwako kwa budget ndogo sawa ingawa mi sikuona kama ameomba based on budget.
Pili si kweli kwamba ukifanya adjustment za dimension una double cost unless uniambie neno double limebadilishwa maana! Unaweza kuongeza ukubwa kwa kuondoa visivyo na umuhimu ndio maana ya review and dedactions. So usimtishe kwa uzoefu wako mmoja wa huyo rafiki yako. Wengine pia tuliwahi kufanya site adjustment na tunavijumba vyetu kadhaa.
 
Sawa nimekupata basi kwenye huo huo ukuta mwishoni karibu na upande wa kuta ya store weka dirisha mkuu kusaidia ventilation.
Alafu pia hapo kwenye entrance kati ya foyer na sitting room weka french doors. Hii ni kwa sababu ya ufaniai wa ac kama utaweka kwenye siting room.
Asante mkuu, French door ndio ipi tena?
 
Kuna mjumbe kashasema Baraza mbele ya master bedroom siyo poa. Bora hata iwe upande wa dining.
Toilets za 1.5*1.6 siyo mbaya, ila zipangiliwe vizuri. Mwambie mchoraji akuwekee wc, shower tray na basin na ikibidi akupe na vipimo vyake.
Jiko dogo ila kuna milango/njia tatu. Sioni likiwa practical. Mchoraji akuwekee design ya jiko- sink litakaa wapi, fridge, cooker nk. Kumbuka unahitaji prep area pia Kwa kuandaa vya kupika na pakuepulia vilivyoiva.

Vyoo na jiko huwa vinasahaulika kupangwa na wachoraji wengi. Usipokee plan isiyoonyesha mpangilio wa ndani wa vitu hivi. Bedrooms pia ni muhimu ujue kitanda na kabati au meza vitakaaje.

Mlango wa master bedroom unaweza kurudishwa nyuma kwenye hicho kicorridor chake.

Mzee wa mizagamuo mzabzab ... Asante kwa mawazo mazuri.

Nimeweka dirisha moja Sebuleni kwa sababu huwa napenda kwenye sitting room sehemu ya "Entertainment area" (ie upande wa Tv) usiwe na dirisha wala mlango, uwe plain na itawaliwe na TV, sound system, game etc peke yake. Unaonaje wazo hili kwa hii ramani?

Wazo la dirisha mbili Master bedroom nimelichukua, na nitarekebisha hapo.
Hapa naona ni vizuri zaidi kuwa na madirisha mawili sitting room. Unaweza kuamua media wall yako iwe huo ukuta wa foyer au hata wa kitchen lakini usijiruhusu kuwa na dirisha moja tu. Ukiachana na mwanga, unahitaji hewa safi na kaupepo ka kupunguza joto kapite dirisha moja na kutokea dirisha lingine. Hiyo ndiyo njia nzuri ya kupooza chumba naturally bila feni na A/C (umeme wa nchi yetu unaujua)
 
Mie nachambua kwa vipengele naanza na master bedroom toilet ambayo ni ndogo sana. master toilet inatakiwa iwe ya kujiachia sio choo chembamba kama cha bweni la shule.

Pia ukiangalia hivyo vyumba ni vidogo sana yaani 3 x 3 ni chumba ambacho ukiweka kabati la nguo hupati hata sehemu ya kuvalia au kuweka meza na kiti cha kusomea.

Kingine safari ya kutoka bedroom 1 mpk chooni ni ndefu sana kama ndio unaenda kukojoa usiku usingizi wote unaishia njiani na pia upande public toilet ilipokaa ingerudi huku kwenye upande wa vyumba ambavyo watatumia wahusika

Home ofisi sioni umuhimu wake kwa Bongo. Bora hapo ungeongezea ukubwa wa rooms na kupata chumba kimoja self contained

Sebule kubwa sana na pia hako kaukuta kulia kwa foyer kanakozuia korido kasiwepo nyumba za kisasa zinatakiwa kuwa na open floor concept sio makona kona unazuia hewa na mwanga kusambaa vizuri ndani na pia inaongeza unnecessary costs.

Nyumba ina makosa yanatakiwa marekebisho na hapo jikoni pawe open ule ukuta unaotazamana na foyer usingekuwepo
 
Mkuu funzadume asante kwa ushauri.

1. Vyoo nitaongeza upana. Nafikiri upana uwe 1.5M, una maoni gani kwa upana huo?

2. Vyumba nitaongeza ukubwa pia... Nafikiri niweke 3.2×3.3 (hii ni nyumba ya kuanzia maisha kwa kafamilia kadogo), una maoni gani kwa hizi dimensions?

3. Ukuta wa Sebule pembeni ya foyer nitauondoa kuleta space and light kama ulivyoshauri

4. Jiko nitalifanya kuwa open kitchen.

Ni kweli kabisa, nyumba za kisasa hasa kwa huko mambele ni open concept... Mimi nitaenda na Open concept(half)
 
Hakikisha pia nyumba ina mwanga wa kutosha ndani. Madirisha makubwa
Screenshot_20230224_085407_Instagram.jpg
 
Mkuu P, Kuhusu sink la choo cha master, uko sahihi.. nitaliweka kwenye hiyo position uliyoshauri.

Kuhusu kila chumba kuwa self ni wazo zuri sana... Ila hii ni nyumba ya kuanzia maisha, ( Mungu akinijalia uwezo na uhai nimepanga kujenga nyingine huko miaka ya mbeleni), hivyo nilifikiri niifanye simple.

Asante sana kwa inputs mzee baba
Ndugu, hiyo nyumba siyo simple ya kusema ya kuanzia maisha. Ni nyumba kubwa sana.
 
Nimekupata mkuu... hebu nisaidie, nyumba ya kuanzia inatakiwa iweje? Nini nikipunguze hapo ili iwe nyumba ya kuanzia maisha?
 
Wakuu mambo vipi.
Nina ramani ambayo nimeandaa kwa ajili ya kujenga nyumba ya vyumba vitatu.(1 master bedroom + 2 normal rooms).
Nyumba itapauliwa kwa mtindo wa Hidden Roof a.k.a contemporary

Naombeni mawazo yenu juu ya hii ramani.

  • Nini cha kuboresha?
  • Nini kimekosewa/hakijakaa sawa?
  • Nini cha kurekebisha?
  • Nini niondoe/nipunguze?

Nimeambatanisha hapa chini ramani yenyewe.

View attachment 2521843
Choo cha jumuiya kipo mbali mno, hapo unampa nafasi mgeni kutalii nyumba nzima wakati wa kwenda toilet,wageni wengine ni wezi, ukizubaa kidogo anapita na kitu.
Ni vizuri pia kitchen ikawa na kibaraza, itasaidia huo mlango kutoloa na maji pindi mvua inaponyesha na pia mtu anaweza akachambulia mchele huku anakula zake upepo
 
Kibaraza cha mita 4.5 ni kikubwa sana, nashauri hii nafasi bora ungeiongezea kwenye sebule kwa kubadili hii design ya mlango wa kuingilia ikawa hivi, huo ukuta niliouwekea xxx unautoa
20230228_061702.jpg
 
Choo cha jumuiya kipo mbali mno, hapo unampa nafasi mgeni kutalii nyumba nzima wakati wa kwenda toilet,wageni wengine ni wezi, ukizubaa kidogo anapita na kitu.
Ni vizuri pia kitchen ikawa na kibaraza, itasaidia huo mlango kutoloa na maji pindi mvua inaponyesha na pia mtu anaweza akachambulia mchele huku anakula zake upepo
Kwa nn kusiwe na choo nje kabisa huko?Vya ndani ni Vya wanafamilia sio muuza samaki kapita anabanwa na haja ndogo unampeleka ndani.
 
Wakuu mambo vipi.
Nina ramani ambayo nimeandaa kwa ajili ya kujenga nyumba ya vyumba vitatu.(1 master bedroom + 2 normal rooms).
Nyumba itapauliwa kwa mtindo wa Hidden Roof a.k.a contemporary

Naombeni mawazo yenu juu ya hii ramani.

  • Nini cha kuboresha?
  • Nini kimekosewa/hakijakaa sawa?
  • Nini cha kurekebisha?
  • Nini niondoe/nipunguze?

Nimeambatanisha hapa chini ramani yenyewe.

View attachment 2521843
Mlango wa kutokea jikoni siku zote unatakiwa ufungukie nje, hii ni kwa ajili ya usalama pale inapotokea hatari yoyote sana sana huwa ni moto, kusukuma mlango ni rahisi kuliko kuuvuta
Hivyo vimstatili ni nguzo za varanda
20230228_062318.jpg
 
Wakuu mambo vipi.
Nina ramani ambayo nimeandaa kwa ajili ya kujenga nyumba ya vyumba vitatu.(1 master bedroom + 2 normal rooms).
Nyumba itapauliwa kwa mtindo wa Hidden Roof a.k.a contemporary

Naombeni mawazo yenu juu ya hii ramani.

  • Nini cha kuboresha?
  • Nini kimekosewa/hakijakaa sawa?
  • Nini cha kurekebisha?
  • Nini niondoe/nipunguze?

Nimeambatanisha hapa chini ramani yenyewe.

View attachment 2521843
Kwa haraka baraka hivyo vyoo vina urefu wa 3m ambapo kiuhalisia ni kubwa sana
Mlango wa master kuangaliana na vyumba vingine pia haipendezi, kama ni mimi ningefanya hivi, hiyo wash basin niliyooneshea mshale unaweza ukaiweka hapo kwenye kona nyingine
20230228_064213.jpg
 
Back
Top Bottom