Naombeni mnipe ujasiri wa kuthubutu nisiwe muoga

Doh! this world has never been fair at all! Mkuu is this what you can advice this little gal?
 
Shika hii mdogo wangu, kamwe usijidharau wala kujiona upo nyuma ya wakati kwa kuangalia mazingira ya wanaokuzunguka na mitandao itakupa stress na depression na kutaka mkato.

Anza na hiyohiyo uliyonayo kama ni online shop fanya ila jitahid usponsor ili uweze kureach watu wengi,kama ni wakala anza usikae kwenye maswali na kujidharau.

Badili mindset yako jiamini na jikubali, maana usipofanya ivyo hata biashara ukianza itayumba kutokana na hiyo mindset.

Maana kile unachokiamini (kibaya au kizuri) ndio haki yako ila kile unachokiri kwa kinywa chako kinatokea.
 
Ahsante sana
 
Doooh....Kwan ndoa ni Ajira ?
.wakati wa Mungu ukifika atanipatia mume na nitaolewa
 
Shukran sana
 
OLEWA.
 
Kwa mtaji huo unaweza anza na 1.duka la mangi
2.mtumba nenda ilala sokon point nguo nzur uza
3.uwakala wa pesa(asubuhi anzia magufuli stend)
4.nguo za ndani
5.pika chakula home panda gari kauze kkoo(mchana) + asubuhi pika uji kauze hukohuko so utakua unapiga hela asbh na jion
6.kauze vitu vidogovidogo stend jittoe aibu
7.jifunze cherehan shona make sure unakua fundi mzuri sana ili usipoteze wateja
8.tafuta soko la kuku wa nyama(chips) fuga ila make sure unapata kwanza soko
9.tafuta kijiwe uza mayai kua mtu wa kati
10.nunua vitanda uza anza kwanza kufungua insta page post vitanda ukianza kupata wateja uza ongeza cha juu isizid elf 50

Nb
Vipodozi ni biashara nzur ila inahitaji mtaji hasa kwa hapa dar ushindan ni mkubwa unless upo mkoani ila kama unaipenda sana anzia ktk kachumba kadogo sana ili kajae au kiosk
 
Kiufupi, tumia akili nyingi sana kujua Cha kufanya na kiwe ni kitu Cha chini kabisa hata Cha mtaji wa laki 5 tu, na ukiwa kwenye mzunguko huko mjini utakutana na mambo mengi kiutafutaji, kidogo kidogo utajua Cha kufanya chenye faida na ndipo utakianzisha na kufungua hizo 2M baadaye, hao wadada unao waona Wana maduka yao, wengi wamepita njia mbovu hata kama si wote, lakini wengi wao ni wamehongwa na wanaendelea kuuza utu wao, baadhi ya maduka yao na biashara zao ni kama magoli ya kudakia wanaume, unaweza Dhani ni utani au ni dharau lakini huo ndiyo ukweli, usiwaige Wala usitazame maisha yao, fuata sauti yako ya ndani juu ya unacho kipenda kufanya kiutafutaji, na ukifuate hicho pole pole, utakifikia.

Siku njema.
 
ungempa na soft copy kabisa
 
Sijaenda hata nilikua busy na mechi ya Yanga [emoji23][emoji23][emoji23]. Niko mjini naondoka baadae
😂😂 Haya mwana yanga. Nitakucheki nikija huko next month. Dar imebishinda Bora nirudi zangu huko nipunge upepo wa bahari
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…