Naombeni msaada, kuhusu barua ya kuthibitishwa kazini na namba ya TSD

Naombeni msaada, kuhusu barua ya kuthibitishwa kazini na namba ya TSD

CK Allan

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2013
Posts
2,781
Reaction score
6,139
Tafadhali naombeni msaada, nimeajiriwa april mwaka jana.. hadi muda huu sijapata tsd no. wala barua ya kuthibitishwa kazini.. je kuna vigezo gani vinatumika? maana nimeona wengine tumeajiriwa wote wameshapata...

na je nikitaka mkopo nmb hadi niwe na hiyo barua ya kuthibitishwa??

tafadhali sitaki kejeli kama hujui pita tu.
 
Kimsingi ili uweze kupata baarua ya kuthibitishwa kazini ni mpaka pale utakapokuwa umekamilisha mwaka mmoja kazini! lakn kwa upande wa tsd si lazma ufikishe mwaka 1, ila kwa maeleza zaidi nenda ofisi ya tsd wilaya watakupa maelekezo zaid!
kuhusu kupata mkopo nmb, ni kweli kwa sasa masharti yanataka mpaka mtu awe na barua ya kuthibitishwa kazini!
 
Hiyo barua kweli inatakiwa uipate baada ya walau miezi sita,na inategemea sana ushapu wa wilaya yako,wilaya zile zinafanya kazi ipasavyo basi ndani ya miezi sita unatakiwa uwe umeshapata barua hio ya tsd,
Barua ya kuthibitushwa kazini lazima uwepo kazini kwa mwaka mmoja na bado pia inategemea sana uharaka wa wilaya unayoihudumia!!!,ba kingnine ni ufuatliaji wako mwenyeweee!!!!
 
aisee tafuta kazi ya umoderator..

kisheria tsd number/letter ni ndani ya miezi mitatu tu!..
probation time (confirmation letter ni baada ya mwaka mmoja).
kuhusu mkopo nmb wanataka tsd letter na sio confirmation letter. mwalimu
kukaa mwaka bila barua rasmi ya ajira (tsd letter) ni uzembe wa idara husika,....shame upon you Tanzania
 
Nafikiri sijaona umuhimu wa baadhi yetu kuilalamikia mamlaka huyu jamaa kasema AMEAJIRIWA APRIL 2014 sasa MWAKA HAUJATIMIA malalamiko yanin serikalini hawaangalii nani kapata ndo mwingine apewe its matter of time na regulations.
 
cha kulalamikia sio uthibitisho kazini ambao kweli ni baada ya mwaka. cha kulaumu ni tsd letter (barua rasmi ya ajira) ambayo ki sheria ni miezi mitatu tu! sasa sijui kama tangu april 2014 hadi sasa haijaisha miezi mitatu?????!!!!!!!
 
Sorry kama ckuelewka kiasi, kuna kitu tunaita LETTER OF APPOINTMENT ON PERSONABLE TERMS hii kitu ndo inakua na TSD namba na ndo barua ya ajira na ndo kila kitu ktk utumishi wako nnacho jua mim after 8-12 months unapewa hiyo na copy ya mkataba wako wa ajira, hakuna barua nyingine itakayo kuthibtisha kazin zaid ya hyo. Sorry ka kunanilicho kiacha wengine watusaidie.
 
Back
Top Bottom