Naombeni msaada wa eneo la kufanyia biashara jamani

EveningStar

JF-Expert Member
Joined
Nov 14, 2018
Posts
262
Reaction score
162
Habari zenu wakuu,

Mimi ni kijana wa kiume nina umri wa miaka 28, nina elimu ya shahada ya kwanza katika sayansi ya chakula na teknolojia kutoka SUA. Ni hivi tokea nimalize masomo nimeangaika kutafuta kazi sehemu mbalimbali pasipo na mafanikio yoyote yale huku muda ukizidi kwenda. Kutokana na hayo nimepata wazo la kufanya biashara huku nikiendelea kutafuta kazi taratibu kuliko kukaa kusubiri ajira hali ya kuwa muda unazidi kwenda.

Sasa katika wazo langu la biashara nimefanikiwa kupata kiasi cha Tsh.300,000/= kama mtaji. Nimepanga kufanya biashara mojawapo kati ya hizi, nafaka, nazi,maharage,matunda n.k ili niweze kupata fedha za kujikimu huku nikisubiri ajira maana hali yangu ni mbaya. Kwahiyo kutokana na mtaji wangu huo kuwa mdogo nimejikuta nikipata changamoto ya kupata eneo la kufanya hiyo biashara hapa Dar es salaam, pia sina uzoefu katika masuala ya biashara maana sijawahi kufanya biashara yoyote hile hapo kabla.

Kwahiyo naombeni msaada wenu jamani ili niweze kujikwamua kiuchumi, kwa yoyote mwenye kutaka kunisaidia husisite kunitafuta kwa namba hizi 0758 106 501, Nipo Dar es salaam. Kwa upande wangu mimi ni mwaminifu, muadilifu na mchapakazi mzuri.

Ahsanteni sana na MUNGU awabariki wote wadau!
 
Kwa mtaji huo, huna haja ya kutafuta eneo là biashara, we nunua bidhaa kama nguo, urembo, mwaga barabaran siku hizi machinga wameruhusiwa.....au fanya biashara ya kuuza kahawa inalipa sana
 
Mkuu, huwezi fanikiwa bila kujitoa akili.

Kwanza kabisa rudi morogoro. Kwasababu wewe ni mwenyeji Kule utapata unafuu.

Kodisha shamba walau nusu ekari.(lililo karibu na vyanzo vya maji)

Nunua mbegu za nyanya, spinach na mboga nyingine zenye uhitaji.

Fanya kazi katika shamba kwa bidii. Utapona matokeo baada ya miezi mitatu.

CHUKUA HATUA SASA HIVI.
 
Nenda pale Karume sehemu ya mitumba , nunua nguo za watoto na wanawake . Piga pasi na tembeza kwa bei ya mara mbili uliyo nunulia uwe na kauli nzuri . Usiangalie makunyanzi chapa mwendo
 
Kama uko tayari kufanya biashara ya nguo za mtumba pale boma...yani unakuwa unafungua balo unatafuta wasaidizi wawili wa kupiga kelele..kazi yako inakua kupokea pesa tu..
 
Habari zenu wakuu,

Mimi ni kijana wa kiume nina umri wa miaka 28, nina elimu ya shahada ya kwanza katika sayansi ya chakula na teknolojia kutoka SUA. Ni hivi tokea nimalize masomo nimeangaika kutafuta kazi sehemu mbalimbali pasipo na mafanikio yoyote yale huku muda ukizidi kwenda. Kutokana na hayo nimepata wazo la kufanya biashara huku nikiendelea kutafuta kazi taratibu kuliko kukaa kusubiri ajira hali ya kuwa muda unazidi kwenda.

Sasa katika wazo langu la biashara nimefanikiwa kupata kiasi cha Tsh.300,000/= kama mtaji. Nimepanga kufanya biashara mojawapo kati ya hizi, nafaka, nazi,maharage,matunda n.k ili niweze kupata fedha za kujikimu huku nikisubiri ajira maana hali yangu ni mbaya. Kwahiyo kutokana na mtaji wangu huo kuwa mdogo nimejikuta nikipata changamoto ya kupata eneo la kufanya hiyo biashara hapa Dar es salaam, pia sina uzoefu katika masuala ya biashara maana sijawahi kufanya biashara yoyote hile hapo kabla.

Kwahiyo naombeni msaada wenu jamani ili niweze kujikwamua kiuchumi, kwa yoyote mwenye kutaka kunisaidia husisite kunitafuta kwa namba hizi 0758 106 501, Nipo Dar es salaam. Kwa upande wangu mimi ni mwaminifu, muadilifu na mchapakazi mzuri.

Ahsanteni sana na MUNGU awabariki wote wadau!
Nikiangalia huu uzii kwa jicho la tatu, naona niko naelekea huko huko, maisha baada ya chuo sio mazuri hata kidogo, Mungu akufanyie wepesi mkuu
 
Kama unastrugle kupata eneo la kufanyia biashara.uza bidhaa kwenye minada.

Kuna mnada hapo dar huwa unazunguka, mi nafahamu mmoja huwa unafanyika kila jumapili yombo machimbo.

Vinginevyo jaribu njia ambayo ameelezea mdau post #4,#5 na #2
 
Nikiangalia huu uzii kwa jicho la tatu, naona niko naelekea huko huko, maisha baada ya chuo sio mazuri hata kidogo, Mungu akufanyie wepesi mkuu
Anza maandalizi sasa hivi mzee, tafuta kabiashara kakuanza nako uende taratibu.
 
Back
Top Bottom