EveningStar
JF-Expert Member
- Nov 14, 2018
- 262
- 162
Habari zenu wakuu,
Mimi ni kijana wa kiume nina umri wa miaka 28, nina elimu ya shahada ya kwanza katika sayansi ya chakula na teknolojia kutoka SUA. Ni hivi tokea nimalize masomo nimeangaika kutafuta kazi sehemu mbalimbali pasipo na mafanikio yoyote yale huku muda ukizidi kwenda. Kutokana na hayo nimepata wazo la kufanya biashara huku nikiendelea kutafuta kazi taratibu kuliko kukaa kusubiri ajira hali ya kuwa muda unazidi kwenda.
Sasa katika wazo langu la biashara nimefanikiwa kupata kiasi cha Tsh.300,000/= kama mtaji. Nimepanga kufanya biashara mojawapo kati ya hizi, nafaka, nazi,maharage,matunda n.k ili niweze kupata fedha za kujikimu huku nikisubiri ajira maana hali yangu ni mbaya. Kwahiyo kutokana na mtaji wangu huo kuwa mdogo nimejikuta nikipata changamoto ya kupata eneo la kufanya hiyo biashara hapa Dar es salaam, pia sina uzoefu katika masuala ya biashara maana sijawahi kufanya biashara yoyote hile hapo kabla.
Kwahiyo naombeni msaada wenu jamani ili niweze kujikwamua kiuchumi, kwa yoyote mwenye kutaka kunisaidia husisite kunitafuta kwa namba hizi 0758 106 501, Nipo Dar es salaam. Kwa upande wangu mimi ni mwaminifu, muadilifu na mchapakazi mzuri.
Ahsanteni sana na MUNGU awabariki wote wadau!