Naombeni msaada wa haraka, NMB wamenikalia kooni

Dah..kwahiyo wanamaliza lini deni?
Nadhani bado unaweza kuongea na meneja wa benki pamoja na mwajiri wako ili kutatua tatizo hili. Sheria inataka mwajiriwa abaki na 1/3 ya mshahara. Kama wanakata hela yote, ni kwamba hutawezakuishi na kazi za mwajiri hazitafnyika kwa ufanisi kwa sababu ya stress. Kuna jamaa mmoja alienda kutia nia lafu serikali ilipozuia mishahara ya watia nia, alipata tabu kama yako, alikuwa na mkopo CRDB, basi wakawa wanamkata fedha zote kwa miezi miwili. Kwa kweli ni ukatiri wa hali ya juu.
 
MREJESHO:

baada ya kukomaa nao mwishowe nikaamua kama mbwai na iwe mbwai nikaenda kwa wakili mmoja ambaye baada ya kumsimulia akawafuata then tukakaa mezani wakakubali kukata 70k
Badala ya mshahara wote,

Huyu Mwamba alikataaa kuchukua chochote hata hela ya Soda alinisaidia tu!

Hivyo rasmi kesi imeisha
 
Hongera saana ndugu
 
iz benk kuna cku ua sjui znachnganyikiwa sku moja nkatoa mshahara kuchek balnce iko vle vle nkavuta tena kuchek balanc iko vle vle na hela inatoka nkasema apa nkto tena awa jamaa watanlaza njaa miez kadhaa kurudsha mzgo wao
 
Mkuu Heshima Yako Aisee.

Nimekusoma na kukuelewa mno.
Shukran Sana Umedadavua Vyema
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…