muafi
JF-Expert Member
- Oct 6, 2015
- 2,557
- 6,128
Naongea kwa niaba ya aliekujabkuniomba ushauri!
Nilikua kwenye mahusiano na kaka mmoja tangu 2014, mwaka 2016 tukaanza kuishi pamoja bila kufunga ndoa lakini ukweni tulitambulishana, wakati huo mimi nilikua nina kazi yeye bado hajapata mishe ya maana, tumekaa hvo hvo mpaka nikajifungua mtoto wa kwanza,
mwaka 2020 nae akapata kazi, basi tukachanga hela mimi nikatoa milion moja yeye akatoa laki tisa tukanunua kiwanja!
sasa baada ya kupita mda nikawa namwambia twende kuangalia kiwanja chetu maana kiko mbali kidogo na tunapoishi akawa anakataa nisiende,
siku moja nikaamua kwenda mwenyewe nikakuta kwenye kile kiwanja tayari kuna nyumba inajengwa imefika kwenye Renta, nikarudi nyumbani nikamuuliza kwann anajenga nyumba mpaka inafika hatua hiyo bila kuniambia akaanza kusema alitaka tu anisapraizi na nimemuharibia kwendako,
basi ni nikaa kimya sasa imepita miezi nikamuuliza vp nyumba imefikia wapi nataka niendeko akasema hapana usiende bado iko pale pale kwenyw renta,
but mimi juzi nikaamua kwenda na mwanangu kufika kule site nikashangaa nyumba imeshakamilika kila kitu mpaka Rangi
cha kushangaza mule ndani ya nyumba kuna dada anaishi mule,
dah nilipigwa butwaa nikamuuliza yule dada mwenye nyumba wako mna mahusiano gani, akasema ye huyo ni mtu wake na wanamahusiano tangu zamani😥
niliumia sana ikabidi nikamuulize kuna mama mmoja jirani ambae ndie alituuzia kiwanja yule mama akaniambia eti mume wangu alimleta huyo dada hapo akasema eti ni mdogo wangu mimi
sasa nikarudi nyumbani jion nikamuuliza baba mtoto kua nimeenda site nimekuta nyumba imeisha na mtu anaishi humo je huyo mtu ni nani?
akasema kwamba ni mpangaji, nikamuuliza hivi inawezekanaje nyumba yako upangishe halafu sisi tupange pia , wakati nyumba ipo karibu basi hapo akaanza kunitusi kanitukana sana kwakweli
nina uchungu sana mpaka sasa roho inaniuma, since 2016 niko nae hana kazi na mtoto tumezaa, kiwanja tumechanga tena mimi nilitoa milioni yeye laki tisa, leo hii ananigeuka hivi?
naombeni ushauri jamani nianzie wapi?
nyaraka za kiwanja zinaonyesha jina langu na lake