Hapa nilipo baba yangu mkubwa alifariki miaka zaidi ya ishirini iliyopita akamuacha mama mkubwa na watoto wake saba.Pia katika kipindi hicho baba mkubwa alizaa watoto wawili kwa mama tofauti,akawachukua na kuwaleta kwa mama mkubwa ndiye aliyewalea wote!Hivi sasa watoto hao ni mama wazima na wana familia zao.Sasa kilichotokea wamekuja wanataka urithi wao.Wanadai nyumba iuzwe ili wapate haki yao!Ila huyo mama mkubwa ambaye aliwalea bado yuko hai na anaishi hapo!Naombeni ushauri nini kifanyike kwa mujibu wa sheria?Pia,pamoja na mume wake kufa,inamaana huyo mama hana haki yoyote kwenye hizo Mali hasa ikichukuliwa kuwa aliishi na mumewe toka 1970 hadi umauti unamkuta 1993?.Naombeni ushauri wadau maana mama mkubwa ana mawazo sana hasa ikichukuliwa kuwa hata umri wake umesonga.