Naombeni Msaada wa kisheria Wakuu

Naombeni Msaada wa kisheria Wakuu

baba na baba

Member
Joined
May 31, 2024
Posts
27
Reaction score
33
Habari wakuu naombeni msaada wenu
Nilifukuzwa kazi nikapewa barua ya kufukuzwa na inaelekeza nitapewa madai yangu yote ndani ya siku kumi na nne (14)za kazi, ila Leo ni siku ya 16 sijalipwa chochote je naweza kuwashtaki waajili wangu.
 
Ndio unaelekezwa ndani ya siku 14 za kazi ntakupwa pesa zangu nazo dai ila sijalipwa
 
Rudi ukawaulize ama wasiliana nao ili ujie hatma ya madai yako.
Kama itaahindikana nenda ukawafungulie mediation CMA, kisha udai na fidia usumbufu, gharama za kuendesha kesi na kadhalika
 
Rudi ukawaulize ama wasiliana nao ili ujie hatma ya madai yako.
Kama itaahindikana nenda ukawafungulie mediation CMA, kisha udai na fidia usumbufu, gharama za kuendesha kesi na kadhalika
Sawa mkuu Asante
 
Nilifukuzwa kazi nikapewa barua ya kufukuzwa na
Pole kwa changamoto iliyokukuta,sheria za kazi zinahitaji mtu pale anaposimamishwa au kuachishwa kazi kulipwa stahiki zake zote siku hiyohiyo,na inaposhindikana kwa malipo kufanyika kwa siku husika ina maana hiyo Termination haiwezi kuwa kamilifu na sahihi,vinginevyo kuwe na sababu za msingi zinazozuia malipo husika kufanyika katika siku hiyo ya kuachishwa kazi.
Kuachishwa kazi -inahusisha kupewa barua yako ya kuachishwa kazi,cheti cha utumishi na malipo au stahiki zako za kisheria,hivyo kama vitu hivyo havikufanyika ina maana haukuachishwa kazi kwa mujibu wa sheria na unaweza kugungua kesi CMA dhidi ya Mwajiri wako.

inaelekeza nitapewa madai yangu yote ndani ya siku kumi na nne (14)za kazi, ila Leo ni siku ya 16 sijalipwa chochote je naweza kuwashtaki waajili wangu.
Nafikiri ulichopewa ni Notice for Termination of Employment Contract/taarifa ya kuachishwa au kusitishwa kwa mkataba wa ajira,pia kama itakuwa vyema kwako unaweza kutuma au kuelezea content ya barua husika,au kutafuta mwanasheria atakayeweza kukupa msaada zaidi juu ya hilo.


Swali: Naomba kujua kama bado unaendelea kazi kwa sasa?na ulishafanya handover?na ulipewa taarifa ya kuachishwa kazi kuanzia tarehe ngapi?je,ulikuwa na stahiki zozote ulizokuwa unadai kwa Mwajiri?Ulipewa Barua ya nyaraka zozote za kuonyesha kusitishwa kwa Mkataba na Mwajiri Wako?
 
Mkataba unaelekeza hivo. Na pia barua inaelekeza hivo ila malipo nimelipwa kidogo tofauti na ninavyo dai
mhh pole sana,nafikiri kuna kitu hakiko sawa mahali,jitahdi utafute mawanasheria akusaidie maana hakuna sehemu yeyote ambapo utaachiwa kazi na kisha kulipwa baada ya 14 za kuachishwa kazi
 
Habari wadau
Ninafanya kazi shirika fulani tukapewa likizo ya siku 28, siku ya moja kabla ya kurudi kazini nikapewa notice of termination ya siku 30, ikieleza shirika husika linapitia financial difficult na wanafanya wanafanya collaboration na shirika lingine.
Kwahyo nitafanya kazi kipindi cha notice.
Ila mimi nimestukizwa na sikupewa notice of intentions of retrenchment, wala hakukuwa na consultation, sikuitwa wala hatukujadili chochote zaid ya kapewa tu notice of termination.
Naomba msaada wenu kisheria imekaaje hapo au hakiyangu ni ipi?.
Mifano ya case zilizofanyika zitasaidia pia.
 
Back
Top Bottom