Naombeni msaada wa kitiba, mwanangu anatatizo la mgolo (bawasiri)

Naombeni msaada wa kitiba, mwanangu anatatizo la mgolo (bawasiri)

implicit memory

JF-Expert Member
Joined
Nov 14, 2024
Posts
806
Reaction score
926
Habarini wanajukwaa hili,

Kama mada inavyojieleza ni kwamba mwanangu wa kiume umri mwaka 1 na nusu kwa mwezi sasa anasumbuliwa na mgolo kutoka nje, kila anapojisaidia haja kubwa.

Nilimpeleka hospitali lakini nilimshangaa Daktari anaonekana kutotambua ugonjwa huu.

Baada yakumwelezea,bpia mtoto anasumbuliwa na mafua na kikohozi, hakunipa dawa ya bawasiri (ndo maana nimeona uenda haujui ugonjwa huu).

Alinandikia tu syrup za kikohozi na mafua,bnakushauri nimpe maji mengi yakunywabpamoja na juisi na vyakula laini laini baasi.

Naomba mwenye kujua anisaidie hili tatizo.

Asanteni.
 
Jaribu tiba ya mgagani,unafikicha kisha unamuwekea huko nyuma,pia apunguze kula vitu vyasukari ndizi n.k
20241223_161948.jpg
 
Pole Sana
Changamoto Niliona Sehemu Moja Mtoto Akitiwa Kama Mdau Aliyosema Kuna Majani Yanapikichwa Anadondoshewa Baada Ya Hapo Hutasikia Tena Shida Hiyo

Wapo Wazee Mtoto Kama Huyo Akiguswa Korodani Wanajua Huenda Akiwa Mkubwa Atasumbuliwa Na Henia Anapewa Dawa Akiwa Mdogo Tatizo Linakwisha
 
Pole Sana
Changamoto Niliona Sehemu Moja Mtoto Akitiwa Kama Mdau Aliyosema Kuna Majani Yanapikichwa Anadondoshewa Baada Ya Hapo Hutasikia Tena Shida Hiyo

WWapoWazee Mtoto Kama Huyo Akiguswa Korodani Wanajua Huenda Akiwa Mkubwa Atasumbuliwa Na Henia Anapewa Dawa Akiwa Mdogo Tatizo Linakwisha
Sasa mkuu ni wapi naweza wapata hao wazee?,
 
Kwanini usiende hospitali nyingine mkuu?
Au huko ulipo hospitali ni moja tu!
Kwa kiasi fulani nimekata tamaa kwenda hospitali nyingine, maana nimeona hospitali unawaambia dalili na ugonjwa.

Lakini wao hawana dawa hasa ya kutibu wanakwambia tu mpe maji mengi chakula laini, matunda, mara mtoto asikae sana sehemu moja (wakati mtoto mara nyingi hawezi kaa sehemu moja kiiivyo!!,nijuavyo si watu wazima ndo ukaa sehemu moja kwa mda mrefu, labda tokana na kazi tufanyazo).

Nionavyo mkuu huu ugonjwa unatibiwa na dawa asili zaidi na mjibu wa maoni ya wengi, ngoja nijaribu uko zaidi, ahsanteni
 
Habarini wanajukwaa hili,

Kama mada inavyojieleza ni kwamba mwanangu wa kiume umri mwaka 1 na nusu kwa mwezi sasa anasumbuliwa na mgolo kutoka nje, kila anapojisaidia haja kubwa.

Nilimpeleka hospitali lakini nilimshangaa Daktari anaonekana kutotambua ugonjwa huu.

Baada yakumwelezea,bpia mtoto anasumbuliwa na mafua na kikohozi, hakunipa dawa ya bawasiri (ndo maana nimeona uenda haujui ugonjwa huu).

Alinandikia tu syrup za kikohozi na mafua,bnakushauri nimpe maji mengi yakunywabpamoja na juisi na vyakula laini laini baasi.

Naomba mwenye kujua anisaidie hili tatizo.

Asanteni.

Pole sana!

Mtoto wa mwaka mmoja kuwa na bawasiri si kawaida, labda ni sehemu ya haja kubwa ndiyo inayotoka nje (rectal prolapse).

Mpeleke hospital kubwa tatizo lake linatibika tu.

Kila la kheri.
 
Tusiandike sana, nenda hospitali kubwa wacheki inaweza isiwe bawasiri kwasababu ni nadra saaaaaana kwa watoto wadogo. Ndio maana hospital ukienda wanakupa matazamio ya kufanya kuepuka matokeo hayo, kukohoa sana kuharisha au kunya kinyesi kigumu kinaweza kufanya tatizo kuwa kubwa, ndio maana wanakushauri hvo vyakula and not else wise.

KUMBUKA, UGONJWA RAHISI KUINGIA MGUMU KUTOKA KWENYE MWILI WA BINADAMU.

There after zipo hizo dawa umeambiwa za kufikicha, huwezi ambiwa kokote bali kama unaishi vijijini, watu wanazitumia na kupona.
Nina mifano mingi sana, hata watu kutoka ulaya huja tanzania kuzitumia. Huponya kabisa.
Pole sana
 
Back
Top Bottom