1.Je huyu baba alikosea kumuoa mke ambaye hana kiwango cha elimu zaidi ya elimu ya msingi??
2.Je kwa nini huyu baba asimwendeleze huyu mama/mke wake kielimu kidogo ili aweze kuchangamsha akili kidogo?
3. Je ni vizuri mtu kuoa/kuolewa na mtu ambaye walau akili zenu zinaendena katika utendaji wa mambo hasa ukizingatia mipango na maono yako ya maisha?
4. Je huyu baba anafanya makosa kumfanya mpango wake wa kando mshauri wa mipango yake ya maendeleo zaidi ya mke wake?
Mwisho: Unamshauri nini huyu mama mwenye nyumba, ili aweze kuishi kwa furaha na amani katika ndoa yake?
Mbarikiwe!!!
LD: Cheers; thread imekaa vema na big up sana kuleta issue hii:
1. Elimu si Kigezo cha Ndoa wala mapenzi. Mke wangu alikuwa na Diploma wakati na muoa wakati huo mimi nikiwa na Diploma kadhaa; na Degree kadhaa. what i know naye hakuweza kumanage Biashara zote nilizomwanzishia au za familia nilizomkabidhi. So, nilichofanya, kikampelekea shule, kabiga Advance Diploma na sasa anapiga degree na akili yake imekomaa. Tunaenda sambamba katika mambo mengi ingawa si kwa level moja. Ninayo mifano mingine kadhaa kama hii. So, the guy was wrong.
2. Hili nawezekana na huyu Bwana ndiyo ilimpaswa kufanya. inawezekana labda mapenzi ya Mr yako zaidi kwa nyumba ndogo hivyo nyumba kubwa haina priority. By the way, huyu Bwana ana watoto na wanawake hao wote?
3. Kila inapowezekana muoe mtu ambaye mnalingana interest za maisha, na upeo wa kufikiri. mambo kama kufanana dini na tamaduni pia yanasaidia ingawa si sana. Kama mapenzi ni makubwa, factors hizo hazina umuhimu kwani mengine yote yanajengwa juu ya mapenzi. Shida yenu wanadamu, wengi mapenzi yanapungua with time na kubaki mazoea. katika stage hii kufanana upeo, akili na interest inakuwa ni kitu pekee cha kuzidi kuwaweka karibu na hivyo mnakuwa marafiki pia.
4. Anafanya makosa kijamii na kidini. Ilifaa kabisa amuendelezea Mamaa na pia kujenga zaidi mapenzi kwake na kumsaidia kwa kutumia mbinu mbalimbali. Kama nyumba ndogo ina akili ya kibiashara bado angwezeka kupewa kazi lakini chini ya uangalizi wa wote ili kuhakikisha mpango wa kando haufurukuti. Je huyu Mama, naye alifanya jitihada yoyote ya kutaka kujiendeleza?
Huyu mama mwenye nyumba afanye yafuatayo:
1. Amweleze mumewe anafyofanya si vema na haikubaliki
2. asposikia amuitie vikao vya wazazi au Machungaji
3. Afanye jitihada ya kujiendeleza kielemi na kujifunza ujasiliamali, hakuna kisichowezekana.
4. Ale sahani moja na Mr na kuhakikisha kuwa anatumia mbinu muafaka za medani ya Mapenzi kumrudisha mumewe ampende kama zamani.
Allien.