Naombeni Nifunge Mwaka kwa post hii: Spiritual cleansing and Healing (Kuitakasa, kuisafisha na kuiponya roho na nafsi)

Naombeni Nifunge Mwaka kwa post hii: Spiritual cleansing and Healing (Kuitakasa, kuisafisha na kuiponya roho na nafsi)

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
NAOMBENI NIFUNGE MWAKA KWA POST HII; SPIRITUAL CLEANSING AND HEALING (KUITAKASA, KUISAFISHA NA KUIPONYA ROHO NA NAFSI YAKO)

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli
Kuhani Katika Hekalu Jeusi.

Nataka uuanze Mwaka 2025 roho yako ikiwa Safi umeitakasa ili mambo yako yakuendee. Usijesema Mtibeli ni mchoyo. Oooh! Dunia watu wanaficha Siri. Mimi Mtibeli, kuhani Katika Hekalu Jeusi nitakupa Siri hii Wala hutogharamia chochote isipokuwa bando lako tuu.

Niite Taikon Master, Teruso aliyekimbia upanga wa vita ya MIUNGU.

Roho ya mtu ni energy, nishati yenye utashi inayoishi katika mwili wa binadamu.
Hii ni kusema, zipo Roho zisizo na utashi na zipo zenye utashi.

Roho yako inapochafuka mwili na nafsi navyo huchafuka.
Kwenye Ujenzi, Roho tunaweza kuifananisha na MSINGI. Nafsi ni kama Boma na Mwili ni kama Paa la nyumba na Finishing ya Nje ambayo watu huiona kwa haraka.

Roho huchafuka kwa namna nyingi. Mojawapo ya mambo yanayochafua Roho yako ili iwe chafu;

1. Mawazo Machafu.
Mawazo Machafu kama kuwaza, ngono chafu, kama usagaji, ufiraji, threesome, Kulala na wanawake wengi,
Kumfikiria mwingine Mabaya au kujifikiria Mabaya kote huchafua Roho.
Kwa sababu Mawazo Mabaya hualika Mapepo Machafu au Roho chafu zije kutawala akili na mwili wako.

Kuna Jambo Moja unatakiwa kulijua.
Viumbe wa rohoni hawana miili. Hivyo hawana nguvu ya kufanya chochote pasipo kutumia mwili wa binadamu.

Hii ni kusema Pepo mchafu au Majini hayana nguvu yoyote kama hutayaruhusu kutumia mwili wako. Au yatumie Mwili wa Mtu mwingine.

2. Matendo na Maneno Machafu.
Life style yako. Utamaduni wako. Maneno yako.
Chakula na vinywaji vichafu huchafua Roho yako.
Kuna vyakula ukila vinavuta Mapepo Wachafu kama vile ilivyo kuna vyakula ukila vinaweza kukusababishia Magonjwa ya mwili.

3. Mazingira Machafu.
Mazingira Machafu hualika mawazo Machafu, Roho chafu ambazo huchafua Roho na nafsi yako.
Huwezi ishi sehemu inajalala, huwezi ishi nyumba ina tandabui kila Kona, huweziishi nyumba ina nzi na mende wa kutosha au panya wakutosha. Alafu Roho yako isichafuke.
Mazingira Machafu huchafua Roho na nafsi

Huwezi ishi sehemu kuna vichaka na mapori yanayoficha wadudu na viumbe Hatari alafu nafsi na roho yako ikawa Safi.

4. Mwili Mchafu.
Huogi Wala kujisafisha. Unanuka mavi mwili mzima Kisa hujui kutawaza, unanuka mdomo Kisa hupigwi mswaki. Kwapa linanuka, uvungu wa korodani linatoa uvundo.

Mwanamke hujui kutawaza, hujui kujisafisha vizuri hata ukiwa Period. Lazima Roho ichafuke.

Unapoenda kwa Mganga au Kuhani unaenda kufanyiwa Spiritual Cleansing and Healing ili mambo yako yaende. Wengine wanaita kusafisha Nyota, wengine kuondoa Gundu, basi majina yapo Mengi.

Leo nitakupa mbinu chache ambazo unaweza kuzifanya wewe mwenyewe pasipo msaada wa Mtu yeyote. Yaani huhitaji Mganga Wala kuhani Wala Sisi kina Taikon kukusaidia katika Hilo. Wala huhitaji kina Mwamposa au Kiboko ya Wachawi.

Elewa, Usafi mwingine ni suala personal nani privacy. Kama vile ukienda kuoga unaoga bafuni watu wasione uchi wako vivyohivyo na katika mambo ya Kiroho kuna mambo ya Siri ambayo ni wewe mwenyewe unatakiwa kuyajua.

Kuna waganga wasiowaminifu unaweza kwenda kwao wakachukua zawadi na tunu ulizopewa na Mungu kwenye ukoo au kizazi chenu ukabaki mweupe peee!

Zifuatazo ni Njia au mbinu za kujisafisha kiroho na nafsi yako ili mambo yako yaende;

1. Kuwa na Mawazo Chanya, mazuri, waza Mema.
Usiwaze matusi, usiwaze ushenzi, usiwaze takataka.
Mawazo Mabaya huvuta negative energy kwa wale wasioamini mambo ya Mapepo ila kisaikolojia ipo hivyo kuwa ukiwaza Mabaya Mabaya hukujui na ukiwaza Mema Mambo Mema huja.
Kwa sababu Mawazo Chanya huvuta Nguvu Chanya, nguvu Chanya huleta matokeo chanya.

So Njia pekee ya kusafisha Mawazo yako ni kama ifuatavyo;
a) kufanya Meditation, ndio tahajudi.
b) kusoma vitabu vyenye Mawazo Chanya.
c) kufanya Kazi. Muda mwingi tumia kufanya Kazi. Usikaekae.
d) Nenda kwenye michezo kama Kuogelea, kucheza game, kuimba, kucheza muziki WA heshima
e) kuepuka mzaha kibaya

2. Safisha mazingira unayoishi Muda wote yawe Safi.
a) Kila siku nyumba usafishe juu na chini, pasiwe na tandabui Wala mende, Wala nzi, Wala Panya.
b) mazingira ya Nje yawe Safi, ikiwezekana panda maua, Hakikisha panakuwa pazuri panavutia.
c) vitu vikuuvikuu vilivyochakaa huna haja ya kuviweka ndani ya nyumba vitupe au vichome au vigawe. Usikae na makorokoro yaliyochakaa ambayo huyatumii. Yanavuta negative energy.
d) Hakikisha Nyumba yako inukie harufu nzuri

3. Safisha Mwili wako.
a) Kila unapokula Hakikisha unasafisha kinywa chako. Hii itamaanisha usilesile hovyohovyo. Uwe na Muda maalum wa Kula
b) Kula chakula kisafi na kilichoandaliwa kwa Usafi wa Hali ya juu
c) unapokula usile sehemu chafu au yenye wadudu wachafu.
d) Hakikisha unaoga Walau mara mbili kwa Siku.
e) Hakikisha ukienda chooni iwe Haja kubwa au ndogo unajisafisha vizuri.
f) Hakikisha Nywele zako unaziweka Safi.
g) Hakikisha unavaa nguo Safi na zenye heshima.
f) Hakikisha mwili wako hujachora vitu usivyovielewa kwa kuigaiga.

4. SAMEHE
Moja ya mbinu ya kusafisha nafsi na roho yako ni kusamehe waliokukosea.
Usikae na Kinyongo.

IBADA ZA KUJISAFISHA ROHO (SPIRITUAL CLEANSING)

Sasa Roho yako ishachafuka au imechafuliwa. Aidha umefanya zinaa na wanawake hovyohovyo huko wamekuchafulia Nyota (Roho yako). Au umetoa Mimba na kuchafua Nyota yako, au umefira au kufirwa, au umesagwa au kusaga au umefanya Jambo lolote ambalo Roho yako imechafuka. Na Moja ya dalili ya kwamba Roho yako imechafuka ni wakati unapofanya mawasiliano ya Kiroho unakuwa unajihisi hatia, kwamba hutosikilizwa, hutojibiwa na wakati mwingine matendo Mabaya uliyoyafanya yanapita kichwani mwako. Maombi hayafiki mwisho. Au umeua. Basi hizi ni ibada za kujitakasa Roho yako;

1. Kujibatiza au kubatizwa kwenye Maji ya asili kama Mto, Bwawa, ziwa, bahati, visima vya asili,
Hii ni Njia ya kawaida ambayo inatumiwa na watu wengi.
Nenda kwenye Maji Mengi ya asili, hakikisha Maji hayo yawe ya asili.
Lakini kabla ya kwenda Hakikisha siku tatu au Saba kulingana na jinsi Roho yako ilivyochafuka kutokana na makosa uliyoyafanya.
Siku hizi tatu au Saba unaweza kufunga au kuomba huku ukitubu kwa makosa uliyofanya.
Kisha siku ya Tatu au Ile ya Saba unaenda kwenye Maji Mengi, unaingia Majini, kisha unajizamisha Majini mwili mzima sehemu zote za mwili zimezwe na Maji.
Kama ulijiandaa mara tatu, utajizamisha mara tatu Majini. Kama ulijiandaa mara saba utajizamisha mara saba Majini.
Utaomba kwa miungu ya kwenu.
Itapendeza zaidi ukiomba kwa Lugha yako Mama.

Kama utahisi mchakato hautafanikiwa, tafuta mtu unayemuamini akuongoze kufanya hivyo.

2. Njia ya Kufukiza.
Njia hii huambatana na kuchoma baadhi ya mimea itoe Moshi unaovutia ambao ni sumu kwa Pepo Wachafu waliokuingia na kuvutia Roho Wasafi.
Kufukiza kuko kwa Aina mbili,
Kufukiza kwa kuchemsha Mitishamba kisha kujifukizia kwa kufunika na shuka maalumu.
Na Kufukiza kwa kuchoma mitishamba ambapo Mitishamba hiyo hutoa Moshi yenye sumu ya Kufukiza Mapepo Wachafu na kurejesha Roho Wasafi kwenye mwili au kwenye nyumba.
Njia hizo zinaambatana na maombi na dua maalumu kulingana na kile mlengwa unachotaka kifanyike.

3. KAFARA.
Kuna Kafara kubwa na Kafara ndogondogo
Kuna kiwango cha Roho ikichafuliwa itahitaji Kafara ya damu. Kafara ya Damu ndio Kafara kubwa kuliko zote. Hii itahusisha uhai WA kiumbe kingine kwaajili ya Usafi wa roho yako.

Mara nyingi Usafi huu humaanisha Roho yako imeugua Magonjwa makubwa ambayo hayaponi zaidi na ili yapone itahitaji Spare ya Roho nyingine.

Kwa mfano, Ukiua Mtu asiye na hatia au ambaye amekukosea lakini adhabu yake sio ya Kifo ila wewe ukamuua hiyo itamaanisha roho yako nayo inatakiwa iuawe. Hivyo hakuna Njia yoyote ya kuiponya nafsi yako zaidi ya kumwaga damu yako au ya mtu mwingine.

Ndio maana muuaji ni muuaji tuu. Pindi atakapoua mtu Mmoja kwa kukusudia, huyo maisha yake yote ataendelea Kuua na Kuua.

Kafara za watu zina Kanuni zake pia. Huwezi lipia deni la Roho ya mtu mwingine kwa Kuua Kikongwe au mtu mwenye Nyota iliyochafuka.
Kuna Kafara za Kuua watu wenye Nyota Kali, na kina Kafara za Kuua vyakula vya Majini, au viumbe vya Kiroho.
Sio kila mtu anaweza kutolewa Kafara.

Kuna kuchinja Kuku, mbuzi au Wanyama Fulani kwaajili ya kusafisha Roho iliyochafuka kwa kiwango cha Kati.

4. TAHAJUDI (MEDITATION)
Tahajudi ni ibada ya kusafisha Roho iliyochafuka kwa Njia ya mawazo Mabaya.
Tahajudi ni Njia ya kufuta mawazo Mabaya na kumbukumbu mbaya katika akili na nafsi.
Zipo Njia nyingi za kufanya tahajudi.

Aaaah! Nimechoka!
Acha nipumzike sasa.

Nawatakia Kheri ya MWAKA Mpya.
Mungu awe Salama Kwenu.
Mungu awe Upande wenu.
Mungu awe kiongozi wenu.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Back
Top Bottom