Naombeni Orodha ya vifaa vya umeme kuanzia biashara

nyumbamungu

JF-Expert Member
Joined
Mar 3, 2017
Posts
1,033
Reaction score
895
Wadau, Mafundi na wenye uzoefu wa biashara ya vifaa vya umeme wa majumbini naomba mnitajie orodha ya vifaa vinavyohitajika na vinavyotoka haraka kibiashara zaidi.

Nimepata fremu ndogo ya biashara, kwa mazingira ya mtaa huo hakuna duka la vifaa vya umeme kwa maeneo ya karibu, hivyo nimeona endapo nitafungua duka kama hilo kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu naweza nikapata riziki.
 
[emoji3516]
NITAJIE HILO ENEO,
ILO KESHO NIHAMISHIE DUKA LANGU LA VIFAA VYA UMEME HAPO.
 
Sio mtaalam sana ila:
Wire 1.5 na 2.5 mwingi kama atleast 200 meters @ , hizi zinaenda zaid
Wire 4 na 6 kidogo
Taa mbali mbali kama zote, energy savers na Led sana sana changanya za Pin ziwe nyingi na za tred kidogo, weka pia za rangi mbalimbali
Switch, ila za njia moja nyingi zaid kuliko nyingine
Sockets pia zinatumika nyingi kwenye nyumba weka njia moja ziwe nyingi zaidi kama 3/4
Conduit pipes weka pia hata 100 au 50 na trances kwaajili ya wiring ya surface
Junction box na switch box pia weka nyingi kama 200
Lamp holders hata 100 hivi
Socket za coocker hata 5 kuanzia nahis zinatosha
Earth roads hata 10 changanya og na fake, pamoja na wire wa earth
Wire za spika hizi hata 100m
Extension cable kadhaa hata 5
Tape pia ka bandle hivi

Nafkiri wadau watajazia zaidi ila pita kwenye maduka ya umeme ufanye ukachero kidogo
 
Nakushukuru sana njoo ibox kiupendo kuna vocha ya 1000.00
 
kaka upo maeneo makongwe au upo kwenye site mpya??
Site mpya ila ni katikati ya makazi pia zipo huduma za kibinaadamu Shule, msingi na upili, ofisi ya wakala wa serikali "brela" hospitali, chuo hotel management, msikiti hizo ni baadhi tu, sasa hako kagoli kapo katikati...
 
Site mpya ila ni katikati ya makazi pia zipo huduma za kibinaadamu Shule, msingi na upili, ofisi ya wakala wa serikali "brela" hospitali, chuo hotel management, msikiti hizo ni baadhi tu, sasa hako kagoli kapo katikati...
Vp Mkuu ulifanikisha
 

Ongezea square box Za Single na double
Socket breake za single fezi
Main switch za njia 2 , 3, 4 ilq njia 4 inatumika sana
Tranking
Na Single wire 1.5 na 2.5
Earth wire
 
Natumae mleta mada ulipata muongozo...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…