Naombeni tafsiri ya Kiswahili ya neno 'Stationery'

Ndo maana ninadhani kiswahili hakijitoshelezi, si unaona hata duka la dawa sio 'madawa' kumbe nalo halina neno moja, inabidi tuseme DUKA LA DAWA wakati wenztu wanasema tu phamarcy.

DUKA LA DAWA" sio sahihi, inatakiwa iwe DUKA LA MADAWA".
 

Ni sawasawa maelezo yanajitosheleza katika kufafanua tofauti ya haya maneno mawili.

Kama nilivyosema neno la kwanza la stationary linamaanisha kusimama kwa maana ya kungoja kuendelea na kitendo cha kusogea.

Na hio la stationery ndio kwa maana ya vifaa vya kiofisi.

Ni namna mtu anavyoweza kuelezea maana na tofauti ya maneno haya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…