Naombeni ushauri biashara ya magari ya mchanga 20cbm FAW, HOWO

Naombeni ushauri biashara ya magari ya mchanga 20cbm FAW, HOWO

tradewithUrio

New Member
Joined
Jun 2, 2026
Posts
1
Reaction score
5
Naombeni ushauri kwa wawekezaji kwenye hii sekta mikataba kwa siku dereva analeta kiasi gani kwa boss kwa gari ambayo ni mpya ,mikataba inaenda kwa miaka mingapi maintainance nzima za magari na mfumo wa uendeshaji kwa biashara hii ya magari ya mchanga ,Dump Trucks !!
 
Biashara inategemea na eneo ulipo, na tonne za gari, ama ujazo. Pia inategemea na bei uliyonunulia gari, na roho yako kama ni nzuri ama ya kikatili.

Gari ya tonne 2 hesabu 50k
Gari ya tonne 4 hesabu 100k
Za huko juu kuanzia 250k hadi 550k kutegemea tonne za gari na eneo gari inapofanya kazi.

Pia saivi gari unafunga G.P.S kila route inakuwa nabpesa yake unakula wewe tajiri, utajua jinsi ya kulipana na dereva.

Kuna maboss dereva akija kuchukua gari anatoa kwanza pesa ya hesabu ndo akafanye kazi.

Hii kazi haina kipimo constant cha mapato. Kuhusu mikataba sio mzoefu.

Pia kuna kipindi gari haitafanya kazi, kazi zinaenda kwa msimu.
 
Naombeni ushauri kwa wawekezaji kwenye hii sekta mikataba kwa siku dereva analeta kiasi gani kwa boss kwa gari ambayo ni mpya ,mikataba inaenda kwa miaka mingapi maintainance nzima za magari na mfumo wa uendeshaji kwa biashara hii ya magari ya mchanga ,Dump Trucks !!
Anza kufatilia eneo unalotaka gari ifanye kazi utapata majibu mazuri. Huu unaweza kuwa ushauri mzuri.
 
Changamoto kubwa ya malori ya mchanga ni service nyingi kila siku kulingana na barabara mbovu yanamopita, pia hata madereva nao siku izi ni kubahatisha tu wengi wao pasua kichwa hawana uchungu na gari lako!, jitahadi dereva asikuzoee sana hakawii kukugeuza mfanyakazi yeye anajipa ubosi akutawale!, lakini upande wangu bora hata ungepata mende au flatbed uwe unapiga route ndefu za mikoani japo lori linaenda umbali mrefu ila kuna uafadhari kwenye service kulingana na barabara kuwa nzuri tofauti na huko kwenye machimbo ya mchanga.
 
Hesabu ni laki 5 au 6 kwa siku. Changamoto ni madereva,kuna kipindi kazi zinapungua,njia mbovu, ufuatiliaji wa karibu. Gari ukichukua mpya miezi 6 ya mwanzo service ni ndogo za kawaida baada ya hapo andaa bajeti ya dharura muda wowote unaweza pata simu ya spare au marekebisho. Kama una long term plan ajiri mafundi wawili au upate gereji ya kuaminika kwa ajili ya service.
 
Naombeni ushauri kwa wawekezaji kwenye hii sekta mikataba kwa siku dereva analeta kiasi gani kwa boss kwa gari ambayo ni mpya ,mikataba inaenda kwa miaka mingapi maintainance nzima za magari na mfumo wa uendeshaji kwa biashara hii ya magari ya mchanga ,Dump Trucks !!
Haya madude kama una roho ndogo nakushauri achana nayo kabisa mkuu, utakuja kufa siku si zako!, tena ukishaingia kwenye biashara ya malori kuwa mshirikina na kutembea unaongea pekeako barabaran wala sio mbali kwa stress zilizopo huko!.
 
Nikutie moyo ndugu,ninayo mawili, nunua mpya kabisa,@170ml, zero km,
Gari hizi huja kulegea baada ya miaka 3-4.

Mpaka kulegea,huwa imeshajilipa vizuri sana na unakula faida au unaelekeza fedha UTT AMIS.
BAADA YA MIAKA MITANO IUZE 70ML
CHUKUWA MPYA,NDIYO KAZI HII ILIVYO MKUU.TAMU SANA.
Note to forget;- comprehesive insurance ambayo huwa ni 10ml.
 
Biashara kichaa investment kubwa sana return ndogo say manunuzi 186mil mapato 550k/day

%Marejesho ya mtaji ni =500k/186mil=0.27% yaani kwa siku una recover 0.27% ya hela uliyoweka, ni hatari, hata 1% haijafika
Jengo uliojenga kwa 150ml,ukakodisha kwa 700,000/- kwa mwezi... 🧠!?..
(Maisha yana mapito mengi sana)
 
Back
Top Bottom