Ushimen
JF-Expert Member
- Oct 24, 2012
- 40,828
- 99,523
Kwanza ikifika asubuhi anatoa nguo zake nimnyooshe ili avae kwenda kazini na kinacho niuma zaidi wamekua na desturi ya kwenda kuoga bafuni (public bathroom) na mkewe (dada yangu), na wanapokua bafuni wanachelewa sana kutoka.
Na wiki hii nimemuona ameanza tabia mpya ya kuwa ananiamrisha nioshe gari lake kila anapotoka kazini, na juzi aliniangalia sana wakati wa dinner nilipopakua mboga yote hadi nikanywa mchuzi uliobakia kwenye hot Pot.
Kwanza nilishamwambia dada kwamba waache tabia ya kujifungia na shemeji kila wakati wanapotoka kazini, na tabia ya shemeji kuwa anafungia remote ya TV chumbani kwake mimi sipendi.
Wakuu, naombeni ushauri kabla sijamsemea shemeji kwa mama.